Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!

Kama wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga usimdharau yule anayemiliki nyumba ya udongo! Hauna haki ya kufanya hivyo! Kwani wewe unayeishi nyumba ya kupanga hauna uwezo au nguvu ya kutosha kumiliki hata ardhi ya kujenga nyumba ya udongo. Nasiku ikatokea hauna kazi au ajali ya ulemavu ikakukuta ukashindwa kufanya shughuli za kuzalisha pesa inamaana utashindwa kulipa kodi ya pango na mwenye nyumba yake atakufukuza! Lakini yule mwenye nyumba ya udongo maisha yataendelea tu! Nyumba ya udongo inaweza isiwe na mvuto sana kwenye macho ya watu lakini inatoa matumizi sawa na nyumba ya matofali! Wakiitwa majina ya watu na mali zao mwenye nyumba ya udongo jina lake litakuwepo lakini jina la yule anaeishi nyumba ya kupanga itakuwa shida kwake! Usimdharau mwenye chake! Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!……..Anyway, hayo ni mawazo yangu asubuhi hii siku ya JumaTatu! Nawatakieni wiki njema na uzalishaji mwema!

Leave a Reply