KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan ?? kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.

Leave a Reply