“Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.” Dina Marios

Naomba niongee na wale ambao tumeajiriwa.Pamoja na kuwa tupo katika ajira tujitahidi kuestablish biashara au mradi wako nje ya ajira yako.Angalia katika mazingira yako vitu gani unaweza kufanya ili kuongeza kipato cha pembeni.Kuna wazee wetu ambao labda wanasoma hapa wameshapitia hizi hatua za maisha.Ila wapo vijana wenzangu humu ambao bado hujastuka au kujipanga sawa sawa.

Binadamu unaouwezo wa kufanya mambo mengi sana ukiamua.Hivyo usijibane sana spread your wings hata kama unalipwa mshahara mkubwa ofisini.

Kazi ya kuajiriwa ni nzuri lakini sio yako ni ya mwajiri wako.Mwajiri wako anaweza kudai kazi yake au hata kuifuta wakati wowote na ukabaki unambwela mbwela tu usijue la kufanya.Mpaka uanze kutafuta kazi sehemu ingine hali inakuwa ngumu lakini kama una miradi na biashara zako zingine wakati unasubiria kupata ajira ingine unaendelea na shughuli zako tena na ukaamua kabisa No kuajiriwa.Nakuomba usijisahau unapokuwa kazini ukamfanyia kazi muajiri wako tu na ukaacha kuanzisha jambo lako mwenyewe.Unaweza kuwa na shamba,biashara yako,ufugaji au una talent fulani ukaitumia.

Kuna dada ameajiriwa lakini hodari sana wa kutengeneza pilipili.Ana biashara ya pilipili/chachandu ambayo inamuinguzia kipato.Tena wateja wakubwa ni ofisini kwake na maofisi mengine jirani.Zipo supermarkets kadhaa na min supermarkets.Ananiambia kwa jinsi anavyopata pesa kwenye pilipili hata mshahara wake ana muda hajaenda bank kuugusa.

Huo ni mfano tu Mungu amekusudia kukufanikisha katika mambo yote.Hivyo kujibana katika kazi hiyo tu ni kumuwekea Mungu mipaka ya baraka alizokupangia.Na Mungu mwenyewe anasema usiogope. Jitahidi kabla upepo haujageuka ukaja kukumbuka shuka kumekucha.Maana huwa vinageuka kwa kushtukiza hata kujipanga hujajipanga na kila siku ulikuwa unasema kesho kesho.

Nashukuru Mungu hata mie nje ya ajira nina biashara yangu ya mafuta ya nazi.Dina Marios baby coconut oil bidhaa ambayo naamini miaka kadhaa ijayo itakuwa brand kubwa ya mafuta ya nazi ya watoto.Nina projects nyingi za wanawake na watoto sijatulia kwa sababu Mungu amenipa uwezo na lazima niutumie Sifa na Utukufu ni kwake yeye aliye juu.

Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu,bali shamba langu mwenyewe sikulilinda…wimbo uliobora 1:6

Kila la heri!

Leave a Reply