Kesha la asubuhi: Bado tunapendwa ijapokuwa tunakosea

           *KESHA LA ASUBUHI*

          _JUMAMOSI MAY 5, 2018_

     *Bado Tunapendwa Ijapokuwa Tunakosea* _Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 1 Yoh. 2:1._

✍? Wale ambao wako katika muunganiko na Mungu ni mifereji kwa ajili ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Iwapo mtu ambaye kila siku anawasiliana na Mungu atakosea njiani, iwapo atageuka hata kidogo na kuacha kumtazama Yesu kwa uaminifu, hiyo si kwa sababu anatenda dhambi kwa makusudi; kwa kuwa anapoona kosa lake, anarejea tena, na kukaza macho yake kwa Yesu, na ukweli kwamba amekosea haumfanyi kuwa na thamani pungufu moyoni mwa Mungu. 

✍? Anafahamu kuwa ana mawasiliano na Mwokozi; na anapokemewa kwa ajili ya kosa lake katika jambo fulani la hukumu, hatembei kwa kinyongo, na kumlalamikia Mungu, bali huligeuza kosa lile kuwa ushindi. Anajifunza somo kutoka katika maneno ya Bwana, na kuchukua tahadhari asije akadanganyika tena.

✍? Wale ambao wanampenda Mungu kwa kweli wanao ushahidi wa ndani kuwa wao ni wapendwa wa Mungu, kwamba wana mawasiliano na Kristo, kwamba mioyo yao inachochewa kwa upendo motomoto kwake. Ukweli kwa ajili ya wakati huu unaaminiwa kwa imani hai. Wanaweza kusema kwa uhakika wote, “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake. … 

✍? Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” (2 Petro 1:16-19). Maisha ya ndani ya roho yatajidhihirisha yenyewe katika mwenendo wa nje. Hebu acha Neno la Mungu libebe ushuhuda wake badala ya mjumbe ambaye kupitia kwake Mungu ametuma ujumbe katika siku hizi za mwisho ili kuwaandaa watu waweze kusimama katika siku ya Bwana. 

✍? “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!” (Isaya 52:7). Hekima ya wale wanaoitwa wasomi haiwezi kutegemewa, isipokuwa wamejifunza na kila siku wanajifunza masomo kutoka katika shule ya Kristo. Wanadamu, katika hekima yao ya kudhaniwa, wanaweza kupanga na kubuni nadharia na mifumo ya falsafa, lakini Bwana anawaita bure na wapumbavu. Bwana anasema, “Upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.”(1 Wakorintho 1:25). - Review and Herald, May 12, 1896.

*MUNGU AKUBARIKI MTOTO WA MFALME*

Leave a Reply