Kesha la asubuhi: Kando ya akina mama akiwaongoza watoto wao

                *KESHA LA ASUBUHI*

               _JUMANNE MEI 08, 2018_

_Kando ya Akina Mama Akiwaongoza Watoto Wao_  _Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko. 1 Sam 1:27, 28._

? Akina mama Wakristo wanapaswa kutambua kuwa wao ni watendakazi pamoja na Mungu wakati wanapowafundisha na kuwaadabisha watoto wao katika namna ambayo itawawezesha kuakisi tabia ya Kristo. Katika kazi hii watakuwa na ushirikiano wa malaika wa mbinguni; lakini ni kazi ambayo kwa masikitiko imepuuzwa, na kwa sababu hii Kristo ananyang’anywa urithi wake-washiriki walio wadogo wa familia yake. Lakini kupitia kwa ukaaji ndani wa Roho Mtakatifu, ubinadamu unaweza kutenda kazi pamoja na uungu.

? Somo la Kristo wakati wa kuwapokea watoto, linapaswa kuacha alama yenye kina juu ya mioyo na akili zetu. Maneno ya Kristo yanawahimiza wazazi kuwaleta watoto wao kwa Yesu. Wanaweza kuwa wakaidi, na kuwa na hisia kali kama zile za kibinadamu, lakini hii haipasi kutukatisha tamaa ya kuwaleta kwa Kristo. Aliwabariki watoto waliopagawa na hisia kali kama yake mwenyewe.

? Mara nyingi tunakosea kuwafundisha watoto. Mara nyingi wazazi wanawaendekeza watoto katika kile kilicho cha kibinafsi na chenye kuharibu maadili, na, badala ya kuwa na uchungu wa roho kwa ajili ya wokovu wao, wanawaacha kuzurura bila malengo wala mwelekeo, na kukua wakiwa na tabia potovu na mienendo isiyopendeza. Hawakubali wajibu wao waliopewa na Mungu kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hawaridhishwi na tabia za watoto wao, na kuvunjwa moyo wanapotambua kuwa makosa yao ni matokeo ya uzembe wao wenyewe, na kisha wanakatishwa tamaa.

? Lakini ikiwa wazazi wangelihisi kwamba kamwe hawawekwi huru kutokana na mzigo wao wa kuwaelimisha na kuwafundisha watoto wao kwa ajili ya Mungu, iwapo wangelifanya kazi yao kwa imani, wakishirikiana na Mungu kwa maombi na kazi ya dhati wangelifanikiwa katika kuwaleta watoto wao kwa Mwokozi. Hebu akina baba na akina mama wajitoe wao wenyewe, roho, mwili, na nafsi kwa Mungu kabla ya kuzaliwa kwa watoto wao. - Signs of the Times, Apr. 9, 

*TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI*

Leave a Reply