Kesha la asubuhi: Karama ya uponyaji

                  *Kesha la asubuhi*

                         *Juma Tatu* 

                           *9/7/2018*

                  *Karama ya Uponyaji* ?Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. Yakobo 5:14, 15./em>

?Uwezo wa Kristo wa kukomesha maradhi umedhihirishwa katika siku zilizopita kwa namna ya ajabu. Kabla ya wakati ambapo tulibarikiwa kwa taasisi ambamo ndani yake wagonjwa wanaweza kupata msaada kutoka katika maradhi, kwa matibabu ya uangalifu na maombi ya dhati ya imani kwa Mungu, tulishughulika kwa mafanikio na wagonjwa ambao walionekana kutokuwa na matumaini ya kupona. Leo Bwana anawaalika wanaoteseka kuwa na imani kwake. Hitaji la mwanadamu ni fursa kwa Mungu.

?Akatoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao; wanafunzi wake wakamfuata. Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jamaa zake, na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazunguka-zunguka katika vile vijiji, akifundisha.” (Marko 6:1-6).

?Pamoja na matibabu yetu yote yanayotolewa kwa mgonjwa, maombi sahili ya dhati yanapaswa kutolewa kwa ajili ya baraka ya uponyaji. Tunapaswa kumwelekeza mgonjwa kwa Mwokozi mwenye huruma, na uwezo wake wa kusamehe na kuponya. Kupitia katika majaliwa yake ya neema wanaweza kurejeshwa. Waelekeze wanaoumia kwa Mtetezi wao aliye katika nyua za mbinguni. Waambie kwamba Kristo ataponya wagonjwa, iwapo watatubu na kuacha kuzihalifu sheria za Mungu. Yupo Mwokozi ambaye atajidhihirisha mwenyewe katika vituo vyetu vya tiba ili kuwaokoa wale ambao watajisalimisha kwake. Wale wanye maumivu wanaweza kuungana nanyi katika maombi, huku wakikiri dhambi zao, na kupokea msamaha.-Manuscript Releases, vol. 8, uk. 267, 268.

Leave a Reply