Kesha la asubuhi: Kutokuongozwa kwa hisia

                KESHA LA ASUBUHI 

                        JUMAPILI

                        22/04/2018

*_KUTOKUONGOZWA KWA HISIA_*
? *Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu. Zaburi 119:105.*

✍?Utakaso sio hali ya hisia ya furaha inayotawala kwa muda mfupi, sio kazi ya mara moja, bali kazi ya maisha yote.

Yeyote akidai kwamba Bwana amemtakasa na kumfanya kuwa mtakatifu, uthibitisho wa dai lake la kuwa na hiyo baraka utaonekana kwenye matunda ya upole, subira, uvumilivu, ukweli na upendo.

✍? Ikiwa baraka ambayo wale wanaodai kuwa wametakaswa inawaongoza kutegemea namna fulani ya mhemko, nao wanasema kwamba hakuna hitaji la kuchunguza Maandiko ili wapate kujua mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa, basi, hiyo baraka inayotajwa ni ya bandia, kwani inawaongoza wale walio nayo kuthamini mihemko na matamanio yasiyo takaswa na kufunga masikio yao dhidi ya sauti ya Mungu katika Neno lake.

✍?Kwa nini wale wanaodai kuwa wamekuwa na udhihirisho wa pekee wa Roho, na ushuhuda kwamba dhambi zao zimesamehewa zote, wahitimishe kwamba wanaweza kuiweka Biblia pembeni na kuanzia hapo watembee peke yao? Tunapowauliza wale wanaodai kupata utakaso wa ghafla, ikiwa wanayachunguza Maandiko kama Yesu alivyowaambia wafanye, 

✍?kuona kama hakuna ukweli wa ziada kwa ajili yao kuukubali, huwa wanajibu, “Mungu huwa anatufahamisha mapenzi yake moja kwa moja katika ishara maalum na mafunuo nasi tunaweza kuiweka Biblia pembeni.”

✍?Wapo maelfu wanaodanganywa kwa kutumainia mihemko fulani maalum na kutupilia mbali Neno la Mungu. Hawa hawajengi kwenye msingi ambao ndio pekee ulio salama na wa hakika – Neno la Mungu. Dini inayoelekezwa kwa viumbe wenye akili itaonesha vithibitisho vya kimantiki vinavyoonesha uhalisia wake, kwani kutakuwa na matokeo dhahiri moyoni na kwenye tabia. Neema ya Kristo itadhihirishwa kwenye mwenendo wao wa kila siku. 

✍?Bila wasiwasi tunaweza kuwahoji wale wanaodai kutakaswa, “Matunda ya Roho yanaonekana maishani mwako? Je, unadhihirisha upole na unyenyekevu wa Kristo na kufunua ukweli kwamba unajifunza kila siku kwenye shule ya Kristo, ukijenga maisha yako kulingana na mfano wa maisha yake yasiyo na ubinafsi?

??‍♂```Ushuhuda bora zaidi ambao yeyote kati yetu anaweza kuwa nao juu ya uhusiano wetu na Mungu wa mbinguni ni kwamba tunazishika amri zake.

??‍♂ Uthibitisho bora zaidi wa imani katika Kristo ni hali ya kutojitumainia nafsi na kumtegemea Mungu. Uthibitisho pekee wa kuaminika wa sisi kuwa katika Kristo ni kuiakisi sura yake. Kadiri tunavyofanya hivi, tunathibitisha kwamba tunatakaswa kwa njia ya ukweli, kwani ukweli unaoneshwa katika maisha yetu ya kila siku. – Signs of the Times, Feb. 28, 1895.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply