Kesha la asubuhi: Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo

                *Kesha la Asubuhi*

        *Ijumaa : Tarehe 27/4/2018*

*Kuweza Kubainisha Ukweli Kutoka Katika Uongo* ?Maana watu kama hao ni mitume wawawe uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza  mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 2 Wakorintho 11:13, 14.*

?Ukweli ni madhubuti na kupitia katika utii uwezo wake huwa unaubadili moyo uwe na sura ya Yesu. Ni ukweli kama ulivyo katika Yesu ambao unahuisha dhamiri na kubadilisha moyo; kwani moyoni huwa unaambatana na Roho Mtakatifu. Wapo wengi ambao, huku wakipungukiwa utambuzi wa kiroho, huchukua tu herufi za Neno, na kukuta kwamba haliambatani na Roho wa Mungu, kwamba halihuishi nafsi, halitakasi moyo. Mtu anaweza kunukuu kutoka Agano la Kale na Jipya, anaweza kujua amri na ahadi za Neno la Mungu; lakini Roho Mtakatifu asipouweka ukweli moyoni, akiangazia akili kwa nuru ya kimbingu, hakuna nafsi itakayouangukia Mwamba na kuvunjika; kwani ni wakala huyu wa kimbingu anayeunganisha nafsi na Mungu.

?Bila kuangaziwa na Roho wa Mungu, hatutaweza kuutambua ukweli toka katika uongo nasi tutaanguka chini ya majaribu stadi na udanganyifu ambao Shetani atauleta duniani. Tumekaribia kufungwa kwa pambano kati ya Mfalme wa nuru na mfalme wa giza na muda sio mrefu udanganyifu wa adui utazijaribu imani zetu, zionekane ni za namna gani. Shetani atafanya miujiza machoni pa mnyama na kudanganya “wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama” (Ufunuo 13:14).

?Lakini japo mfalme wa giza atafanya kazi kuifunika dunia kwa giza, na kwa giza nene kabila za watu, Bwana atadhihirisha uwezo wake wa kuongoa. Sharti kazi ikamilishwe duniani inayofanana na ile iliyofanyika wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika siku zile za wanafunzi wa awali, walipomhubiri Yesu, Yeye aliyesulubiwa. 

Wengi wataongolewa kwa siku; kwani ujumbe utaenda kwa nguvu. Ndipo itakaposemwa: “Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu” (1 Wathesalonike 1:5). Ni Roho Mtakatifu anayewavuta watu kwa Kristo; kwani huwa anachukua mambo ya Mungu na kumwonesha mwenye dhambi. Yesu alisema: “Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” (Yohana 16:14). – Review and Herald, Nov. 29, 1892.

Leave a Reply