Kesha la asubuhi: Kuweza kutambua nadharia za uongo

                    KESHA LA ASUBUHI 

                             ALHAMISI

                             26/04/2018

*_KUWEZA KUTAMBUA NADHARIA ZA UONGO_* 

? *Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Yuda 3.*

✍?Yuda analeta ujumbe huu ili kulinda waumini dhidi ya mivuto inayodanganya ya walimu wa uongo, watu wenye mfano wa utauwa lakini wasio viongozi salama.

 Katika siku hizi za mwisho, walimu wa uongo watainuka na kuwa watendaji wenye ari. 

✍?Nadharia za naomba zote zitawasilishwa ili kupotosha akili za wanaume na wanawake kutoka kwenye ukweli unaoonesha kile tunachoweza kukisimamia bila wasiwasi wakati huu, huku Shetani akifanyia kazi kwa nguvu washika dini, akiwaongoza kuwa na mfano wa kuwa wenye haki, lakini wakishindwa kujiweka chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu.

✍?Mafundisho ya uongo yatachanganywa na kila hatua ya uzoefu na kutetewa na bidii ya kishetani ili kushikilia akili ya kila mtu ambaye hana mzizi na msimamo katika ujuzi kamili wa kanuni takatifu za Neno. 

✍?Katikati yetu kabisa watainuka walimu wa uongo, watakaosikiliza roho zinazodanganya ambazo chanzo cha mafundisho yake ni Shetani. Walimu hawa watavuta wanafunzi wawafuate. Wakijipenyeza bila kuonekana, watatumia maneno ya kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa na kufanya mawasilisho yasiyo sahihi kwa ustadi huku wakitumia mbinu za udanganyifu.

✍?Tumaini la pekee la makanisa yetu ni kudumu kuwa macho. Wale wenye msimamo mzuri kwenye ukweli wa Neno, wale wanaojaribu kila kitu kwa “BWANA asema hivi” wako salama. 

Roho Mtakatifu atawaongoza wale wanaothamini hekima ya Mungu kuliko mafumbo yanayodanganya ya mawakala wa kishetani. 

✍?Hebu na pawepo kuomba kwingi, sio katika mtazamo wa kibinadamu bali chini ya uvuvio wa upendo wa ile kweli kama ilivyo katika Kristo Yesu. Familia zinazoamini ukweli yapasa zinene maneno ya hekima na akili – maneno yatakayowajia kama matokeo ya kuyachunguza Maandiko.

??‍♂ ```Huu ndio muda wetu wa kutahiniwa na kujaribiwa. Sasa ndio wakati ambapo washiriki wa kila familia inayoamini ni lazima wafunge midomo dhidi ya kunena maneno ya kushtaki ndugu zao. Hebu na wanene maneno yanayoleta ujasiri na kuimarisha imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha mioyo. – Kress Collection, uk. 5.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI NENO LAKE.*

Leave a Reply