Kesha la asubuhi: Kuzungukwa na ngao ya Mungu

*KESHA LA ASUBUHI*

*Alhamisi 03/05/2018*

*Kuzungukwa na Ngao ya Mungu*

Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. Zaburi 50:15.

?Majaribio yanapoinuka ambayo yanaoelekea kutoku-elezeka, hatupaswi kuruhusu amani yetu kuharibiwa. Hata tutendewe isivyo haki kiasi gani, hebu hasira kali isiinuke. Kwa kuendekeza roho ya kulipiza kisasi tunajidhuru sisi wenyewe. Tunaharibu imani yetu wenyewe kwa Mungu, na kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Kando yetu yuko Shahidi, Mjumbe wa mbinguni, ambaye atainua kwa ajili yetu bendera dhidi ya adui. Atatufungia ndani kwa miale angavu ya Jua la Haki. Shetani hawezi kupenya ndani ya miale hii. Hawezi kuipita ngao hii ya nuru takatifu.

?Wakati dunia ikisonga mbele katika uovu, asiwepo hata mmoja kati yetu atakayejidanganya kwamba hatutakuwa na magumu. Bali ni magumu haya haya ndiyo yanayotufikisha katika chumba cha uwapo wa Mungu. Tunaweza kutafuta ushauri wa Yeye asiye na kikomo katika hekima.

?Bwana anasema, “Ukaniite siku ya mateso” (Zaburi 50:15). Anatualika kumpelekea matatizo yetu pamoja na mahitaji ya lazima, pamoja na hitaji letu la msaada wa Mungu. Anatuambia omba haraka. Mara tu tatizo linapoinuka, tunapaswa kumtolea maombi yetu ya uaminifu na ya dhati. Kwa kuombaomba sana kwetu tunatoa ushahidi wa imani yetu kubwa kwa Mungu. Hisi ya uhitaji wetu hutuongoza kuomba kwa bidii, na Baba yetu wa Mbinguni anaguswa na kusihi kwetu. Mara nyingi wale wanaoshutumiwa au kuteswa kwa ajili ya imani yao wanajaribiwa kufikiri kwamba wameachwa na Mungu. Katika macho ya wanadamu wako upande wa wachache. Katika mwonekano wote adui zao wanaonekana kushinda juu yao. Lakini hebu na wasikiuke dhamiri yao. Yeye aliyeteseka kwa niaba yao, na kubeba huzuni na mateso yao, hajawaacha.

?Watoto wa Mungu hawajaachwa peke yao na kuwa bila ulinzi. Maombi hugusa mkono wa Mwenyezi. Maombi “hushinda milki za wafalme, kufunga vinywa vya simba, kuzima nguvu ya moto” – Tutaelewa kinachomaanishwa pale tutakaposikia taarifa za wafia dini ambao walikufa kwa ajili ya imani yao- “walikimbiza majeshi ya wageni” (Waebrania 11:33, 34). – Christ’s Object Lessons, uk. 171, 172.

*MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply