Kesha la asubuhi: Upendano wa ndugu

*KESHA LA ASUBUHI*

```JUMANNE MACHI 20, 2018```

  *Upendano wa Ndugu*


Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. Warumi 12:10. ✍? Roho Mtakatifu anapoingia kwenye mawazo ya mtu, malalamiko na mashtaka madogo madogo baina ya mtu na watu wenzake yatatupiliwa mbali. Mionzi angavu ya Jua la Haki itang’aa kwenye vyumba vya moyo na akili. Katika ibada yetu kwa Mungu hakutakuwa na kutofautisha kati ya matajiri na maskini, weupe na weusi. Ubaguzi wote utayeyuka. Tunapomkaribia Mungu, itakuwa kama undugu mmoja. Sisi sote ni wasafiri na wageni, tunaoelekea kwenye nchi iliyo bora, ile ya mbinguni. Pale, kiburi chote, mashtaka yote, hali yote ya kujidanganya, vitakuwa vimekoma milele. Kila namna ya kificho kitaondolewa nasi “tutamwona kama alivyo” (1 Yohana 3:2). Pale nyimbo zetu zitachukua mada yenye kutia moyo nazo sifa na shukrani zitapanda kwake Mungu. – Review and Herald, Okt. 24, 1899.


✍? Bwana Yesu alikuja katika dunia yetu ili aokoe wanaume na wanawake wa mataifa yote… Yesu alikuja kueneza nuru kwa ulimwengu wote. Mwanzoni mwa huduma yake aliitamka nia yake: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:18, 19)…

✍? Jicho la Bwana li juu ya viumbe wake wote; anawapenda wote naye haweki tofauti kati ya weupe na weusi, isipokuwa kwamba Yeye huwa ana huruma maalumu kwa ajili ya wale walioitwa kuchukua mizigo mizito zaidi kuliko wengine. Wale wampendao Mungu na kumwamini Kristo kama Mkombozi wao, huku wakilazimika kukabiliana na majaribu na matatizo yanayokuwa njiani mwao, bado yawapasa wakubaliane na maisha kama yalivyo kwa moyo uliochangamka, wakikumbuka kwamba Mungu mbinguni anaona mambo haya, na kwa yale ambayo dunia inapuuzia kuwapa, Yeye atawalipa kwa fadhila zilizo bora zaidi. – Selected Messages, kit. 2, uk. 487, 488.

*UBARIKIWE MWANA WA MFALME*

Leave a Reply