Kesha la asubuhi: Utii

*KESHA LA ASUBUHI*

```JUMAPILI MACHI 25, 2018```

*UTII*
_Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote. 1 Petro 1:14, 15._

? Mungu anahitaji nini? Ukamilifu, ukamilifu usio na upungufu wowote. Lakini ikiwa tunataka kuwa wakamilifu, ni lazima tusiweke imani yetu katika nafsi. Kila siku ni lazima tujue na kuelewa kwamba haifai kuitumainia nafsi. Tunahitajika kushikilia ahadi za Mungu kwa imani thabiti. Tunahitajika kuomba kupewa Roho Mtakatifu huku tukitambua kikamilifu hali yetu ya kutojiweza. Kisha, Roho Mtakatifu akitenda kazi hatutaipa nafsi utukufu.

? Kwa uzuri, Roho Mtakatifu atauchukua moyo katika hifadhi yake, huku akiuletea mionzi angavu ya Jua la haki. Tutatunzwa na nguvu ya Mungu kwa njia ya imani.
Tukiwa chini ya utawala wa Roho wa Mungu kila siku, tutakuwa watu wenye kuzishika amri. Tunaweza kuionesha dunia kwamba utii wa amri za Mungu unakuja na thawabu yake, hata katika maisha haya na katika maisha yajayo baraka za milele.

? Bila kujali kukiri kwetu imani, Bwana ambaye anapima matendo yetu, anaona jinsi tulivyopungua katika kumwakilisha Kristo. Ametangaza kwamba hali ya namna hiyo ya mambo haiwezi kumtukuza.Kuamua kukabidhi nafsi kwa Mungu kuna maana kubwa. Inamaanisha kwamba inatupasa tuishi na kutembea kwa imani, siyo kwa kuitumainia au kuitukuza nafsi, bali kumtazama Yesu kama Wakili wetu, kama mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu.

? Roho Mtakatifu atafanya kazi yake kwenye moyo uliotubu, lakini kamwe hatafanya kazi kwenye moyo unaoweka umuhimu katika nafsi, unaojitafutia haki yake. Katika hekima yake mwenyewe, mtu wa namna hiyo hujaribu kujirekebisha mwenyewe. Huwa anakuwa akiingilia kati ya nafsi na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atafanya kazi kama nafsi haitaingilia kati.

? Tunaegemea wapi? Msaada wetu uko wapi? Neno la Mungu linatuambia: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yohana 14:26). Roho Mtakatifu yuko tayari kushirikiana na wale wote watakaompokea na kufundishwa naYeye. Wale wote wanaoishikilia ile kweli na kutakaswa kupitia katika ile kweli huwa wanakuwa wameunganishwa vizuri na Kristo kiasi kwamba wanaweza kumwakilisha Yeye katika maneno na matendo. – Manuscript Releases, kit. 12, uk. 52, 53.

*MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MFALME*

Leave a Reply