Kesha la hasubuhi: Umoja

KESHA LA ASUBUHI

JUMAPILI- MARCH 18, 2018

UMOJA

“Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.” Yohana 17:20, 21.

▶Upatanifu na umoja unapokuwepo kati ya watu wenye tabia mbalimbali ni ushuhuda wenye nguvu zaidi uwezao kuonesha kwamba Mungu alimtuma Mwana Wake duniani kuokoa wenye dhambi. Ni fursa ya pekee ambayo tumepewa kudhihirisha hili. Lakini, ili tulifanye hili, ni lazima sisi wenyewe tujiweke chini ya agizo la Kristo. Ni lazima tabia zetu zitengenezwe kuwa katika upatanifu na tabia yake, nia zetu ni lazima zisalimishwe kwa nia Yake. Hapo tutatenda kazi pamoja bila hata wazo la kugombana.

▶Kudumu katika tofauti ndogo ndogo kutatufikisha katika kutenda yale yatakayoharibu ushirika wa Kikristo. Tusimruhusu adui apate nafasi dhidi yetu kwa namna hiyo. Hebu na tudumu kumkaribia Mungu na kukaribiana sisi kwa sisi. Ndipo tutakapokuwa kama miti ya haki, iliyopandwa na Bwana na kumwagiliwa na mto wa uzima. Nasi tutaweza kuzaa ajabu! Je, Kristo hakusema; “Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana” (Yohana 15:8)?

▶Moyo wa Mwokozi umeelekezwa kwa utimilifu wa kusudi la Mungu unaofanywa na wafuasi wake katika urefu wake na upana wake wote. Inawapasa wawe wamoja na Mungu, japo wawe wameenea duniani kote. Lakini Mungu hawezi kuwafanya kuwa wamoja katika Kristo wasipokuwa tayari kuchukua njia yake badala ya njia yao.

▶Sala ya Kristo itakapokuwa imeaminiwa kikamilifu, maelekezo yake yatakapokuwa yameingizwa katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu, umoja katika matendo utaonekana katika jamii zetu. Mtu atashikamanishwa na mwingine kwa kamba za dhahabu za upendo wa Kristo. Roho wa Mungu pekee ndiye awezaye kuleta umoja huu. Yeye aliyejitakasa mwenyewe, anaweza kutakasa wanafunzi wake. Wakiwa wameunganishwa naye, wataunganishwa kila mmoja na mwingine katika imani iliyo takatifu sana. Tunapopambana kwa ajili ya umoja huu kama ilivyo shauku ya Mungu kwamba tuutafute, utatujia. – Testimonies, kit cha 8, uk. 242,243.

Leave a Reply