Kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu!

Kheri ya siku ya kuzaliwa mdogo wangu / jirani yetu Janet  a.k.a Mrs Samora! Mungu akuzidishie neema na baraka zake. Furaha na amani vikadumu ndani ya nyumba yenu, upendo ukaimarike zaidi ndani yako na familia yako. ......Asante sana kwa kuwa jirani mwema. Tumekuwa wote, nyumba zetu upande mmoja tuna share ukuta na geti moja, ufunguo wa geti mmoja unakaa kwenu mwingine ulikuwa unakaa kwetu kwa miaka mingi sanaaaaaa! Wewe na wadogo zako mmesoma shule moja na wadogo zangu toka #Vidudu pale Chang'ombe Nursery na primary school! Lakini cha ajabu mpaka dakika hii naandika huu ujumbe, sikumbuki hata siku moja sisi kama watoto kugombana, wala wazazi wetu sijawahi ona wakigombana!! Wala kukasirikiana! Tumeishi kwa upendo wa hali ya juu kiasi kwamba najivunia kusema wewe sio tu jirani bali ni ndugu yangu! Shida yetu ilikuwa yenu na shida yenu ilikuwa shida yakwetu!......Asante sana mdogo wangu kwa upendo na amani mliyo tupatia. Mungu akuongoze uzidi kuwa baraka kwa wengine wengi! Happy birthday! I ❤ you!

Leave a Reply