KIIZA TUNDU LISU BASIGYE KOROKONI- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)Ipo siku masikio yata ona badala ya kusikia na macho yatasikia badala ya kuona. Wakati ambapo utatamani ujifiche chini ya milima lakini haitawezekana, wakati ambao wanawake wengi wataomba kuitwa kwa jina la mwanaume mmoja huku wakijilisha na kujivisha wenyewe.

Kwa sasa namfananisha Tundu Lisu na mwanasiasa mkongwe wa vikwazo kutoka kwa jirani zetu Uganda Mh. Kiiza Besigye. Kwa hivi vikwazo vya kuwekwa korokoroni na kupewa kesi nyingi za uchochezi kwa Mh. Tundu Lissu huku akiendelea kuwa jarisi na mwenye kutetea ukweli na hata kutenda na kuheshimu sheria. Sasa ninaona umuhimi wa Tundu Lisu kuwa Raisi wa TLS maana kwa sasa tunahitaji viongozi wanao hoji mifumo kandamizi bila uoga ili kulinda maslahi ya Taifa na watu wake. Kwa courage aliyonayo Mh. Tundu Lissu katika siasa za kweli, naamini hichi ni kipindi cha watu kama akina Lissu kunyanyuka na kuungwa mkono kwa makusudi.

Ningekuwa ni mwanasheria, ningemchagua Lissu kuwa Raisi wa TLS. By the way hiyo TLS na majukumu yake nimeifahamu kipindi hiki kupitia Lissu na inawezekana sio mimi tu, tupo wengi.

Asante Lissu, Go go go go Lissu

Leave a Reply