Kila mtu huwa anafikiria tumbo lake kwanza!

Kila mtu anafanya kazi kwa kufikiria tumbo lake kwanza! Awe mfanya biashara, mwanasiasa, muajiriwa wa mahala popote pale au mwanaharakati wa jambo lolote lile wote kwa ujumla wao wanafanyakazi kwa kufikira matumbo yao kwanza! Na hakuna ubaya wowote kwani hizo ndio njia zao za kujipatia kipato ili waendeshe maisha yao. Huu ni ukweli ambao hauwezi pingika, ndio maana hakuna mtu atajiita mwanaharakati wa jambo fulani akaamua kupigania hicho anachokiamini kwa kutumia pesa zake mwenyewe na muda wake bila kujali ananufaika na nini! Wote wana angalia maslahi binafsi kwanza!

Mwanasiasa ili aweze linda cheo na maslahi yake lazima afanye kazi yake ya kuwatumikia jamii kwa nguvu zote. Mwanaharakati ili apate pesa kutoka kwa sponsors lazima apige kelele nyingi sana kuwashawishi watu kua anachokipigania ni sahihi. Mfanyakazi aliye ajiriwa ili adumu katika kazi yake lazima aongeze elimu na ufanisi kazini. Mfanya biashara ili azidi kukua na biashara yake idumu lazima aangalie jinsi ya kuongeza faida! Hivyo, hakuna mtu hapa duniani atafanya kazi bila kufikiria tumbo lake kwanza. Hata Mungu amesema, asiyefanya kazi naasile! Hata Wachungaji wanalipwa mshahara!

Leave a Reply