“kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu,”~~~~ Zamaradi Mketema

Katika maisha ya kawaida zawadi huja zikiwa zimefungwa bila kujua kilichomo ndani, na kwakuwa ZIMEFUNGWA unaweza jikuta unalidharau Box la hovyohovyo ambalo huenda ndio lenye kitu cha thamani ndani, ama ukalipapatikia box kubwa lililofungwa vizuri ambalo ukija kulifungua unakutana na mauzauza. Na ndio hata BARAKA ZETU zinavyokuja pia, sio mara zote MUNGU huziweka wazi mwanzo, ila huzifunga kwasababu yake maalum, na mpaka unapokuja kutambua hiyo ni ZAWADI ambayo MUNGU amekutunukia kuna mengi yanaweza kuwa yamepita ambayo yanaweza kukujenga ama hata kukufunza kuithamini. Mara nyingi NJE kuna uongo mwingi, Kwenye kila jambo yatupasa tuangalie vitu kiundani zaidi na sio juujuu, iwe ni kazi, mapenzi, maisha ama chochote kile, Nje kunaweza kukawa kwa kupendeza lakini uhalisia usiwe kama panavyoonekana, kumbuka BOX ni rahisi kulipata popote, ila cha thamani ya kukaa ndani ya Box ndio kigumu, na mara nyingi nje panapendezeshwa na wengi kwa MAKUSUDI sababu ndio panapoonekana hivyo usiamini sana NJE NA PICHA YAKE, huwa zinatengenezwa kukuvutia, Hivyo kwenye kila jambo jifunze kuangalia kwa picha ya mbali, kutokudharau kitu na kuwa na subira, usije ukatupa zawadi ya thamani kwa kuhangaika na mabox ya nje yanayogeuka dissapointment baada ya kufunguliwa.

Leave a Reply