KUWA NA SHUKRAN

KESHA LA ASUBUHI

IJUMAA

16/03/2018

*KUWA NA SHUKRANI*

? _Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 1 Wathesalonike 5:18._

✍?Kuna mashaka mengi sana yasiyo ya muhimu, wasiwasi mwingi kwenye akili za watu, juu ya mambo ambayo mtu hawezi kuyabadilisha. Bwana anatamani watoto wake wamtumainie Yeye kikamilifu. Bwana wetu ni Mungu mwenye haki na mwaminifu. Yapasa watoto wake watambue wema na haki yake katika mambo makubwa na madogo ya maisha.

✍?Wale wanaoendekeza roho ya wasiwasi na manung’uniko huwa wanakataa kutambua mkono wake unaoongoza. Wasiwasi usiohitajika ni jambo la kipumbavu; nalo hutuzuia tusisimame katika nafasi zetu halisi mbele za Mungu.

✍?Roho Mtakatifu anapotujia moyoni, hatutakuwa na hamu ya kulalamika na kunung’unika kwa sababu ya kutokuwa na kila kitu tunachokitaka; badala yake, tutampa Mungu shukrani inayotoka kwenye mioyo iliyojaa kwa sababu ya baraka tulizo nazo. Kati ya wafanyakazi wetu leo, lipo hitaji kubwa la kuwa na shukrani zaidi; na wasipofikia hatua ya kuwa na roho hii watakuwa hawajajiandaa kuwa na nafasi kwenye ufalme wa mbinguni.

✍?Kazi kubwa yapasa ifanyike kwa ajili ya kila mmoja wetu.
 Huwa tunaelewa kidogo sana kile Mungu anachokusudia kufanya kupitia kwetu. Inatupasa tujitahidi kutambua upana wa mipango yake na tufaidike kutokana na kila fundisho ambalo Yeye amekuwa akijaribu kutufundisha.

``` ??‍♀Hali ya kudhamiria mabaya ipo kwa wingi mawazoni mwa mioyo na akili zetu tunapojitahidi kuenenda kwa namna yetu wenyewe kinyume na sheria ya wema. Hapa ndipo wengi wanaposhindwa. Huwa hatujengi welekeo wa wema; tunataka kila kitu kitujie kwa namna iliyo rahisi.```

```??‍♀ Lakini swali lenye umuhimu mkubwa zaidi kwa kila mmoja wetu haipasi liwe juu ya namna tunavyotekeleza mipango yetu wenyewe dhidi ya mipango ya wengine, lakini namna tunavyoweza kupata uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo kila siku. Kristo alikuja duniani na kutoa uhai wake ili tupate wokovu wa milele. Anataka amzingire kila mmoja wetu kwa angahewa la mbinguni, ili tuweze kuupatia ulimwengu mfano utakaoiheshimu dini ya Kristo. – Loma Linda Messages, uk. 602.```

Leave a Reply