“Kwetu pazuri nimesha pakumbuka”

FB_IMG_1452475294620-1“Nyumbani kwenu ni nyumbani kwa baba yako ni kwako!”…………karibuni niwape tour ya nyumbani kwetu Utegi, Rorya, Mara. Kwenye picha ni dada yangu mkubwa, yeye ndio mimi namfatia. Hapa ni wiki iliyopita alikuwa amekwenda kusalimia ndugu na jamaa huko kijijini. Yeye anaishi mkowa wa Geita na familia yake. Hapo aliposimama ndio entrance ya nyumba ya mama yangu. FB_IMG_1452475331708Hapa ni eneo la mbele ya nyumba yetu. Naona matengenezo yataanza hivi karibuni kabla ya kumpokea wifi yetu toka Tanga ? can’t wait ? FB_IMG_1452456925691Hapa ni kwa pembeni karibu na mlango wa kuingilia jikoni. Nimekumisije sasa ?? IMG-20151118-WA0001Kwakweli sijafahamu kwanini, ila mimi sijahi kulala kwenye hii nyumba japo imejengwa zaidi ya miaka 20 iliyopita ?? wakati bibi yangu mzazi baba yupo hai nilikuwa nikifika Utegi na lala kwenye nyumba yake. Baada ya bibi kufariki sikuhizi nalala kwa mama yangu mkubwa (mke wa marehemu baba yangu mkubwa ambaye kijana wake anatarajia kuoa yule wifi yetu kutoka Tanga). ??? IMG-20151118-WA0002???? nicheke mimi, watu wanatoka mbali sanaaaaaa!  Hiyo nyumba  yenye kidirisha cha rangi ya “blue” ndiyo nyumba ya kwanza kabisa ya baba yangu. Hapo ndipo alipokuwa anafikia yeye na mama wakati wakienda kijijini ?? what a memory! Naona hata kubomoa hawataki inatumika kama storage…….. Halafu hiyo nyumba nyeupe pembeni yake ni mji wa marehemu baba yangu mkubwa hapo ndio huwa nafikia sikuhizi. Nakule kwenye gari ya pick-up ndiyo nyumba ya marehemu bibi yangu ilipo……..haya basi ukifika Utegi usisahau kupitia kwetu ni njiani kabisa. And let all the glory and honor be to God ?

One thought on ““Kwetu pazuri nimesha pakumbuka””

  1. Ni muhimu sana kuonyesha hualisia kwamba unatoka wapi na tupo wapi,kusudi vizazi vinavyokuja wajue nyumbani halisi ni wapi.

Leave a Reply