LETS CHANGE OUR EDUCATION SYSTEM! – le Mutuz

LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of Ugly FACT ni kwamba 80% ya Vijana wetu wenye Degree HAWANA UJUZI WA KUAJIRIWA PAMOJA NA KUWA NA GPA KUBWA ni ukweli mchungu ambao kama Taifa tunahitaji kutafakari as JE KUNA MAHALI TULIKOSEA? au HATUJAWAHI KUPATIA KABISA!........ninakumbuka siku moja niliwaambia Wanafunzi wa Marketing pale UDSM kuwa kama wapo waliopo Mwaka wa Pili na hawana kazi au shughuli yoyote nje ya Chuo inayohusiana na Marketing then ina maana mbili aidha Wapo kwenye wrong Field au Hawaelewi masomo sawa sawa cause haiwezekani Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Marketing akawa hana cha kuonyesha as Practical nje ya Darasa!

Leo Vijana wetu wanahangaika sana baada ya kumaliza Vyuo vyetu kwa sababu sio tu kwamba hakuna ajira bali hata zikiwepo hawaziwezi kwa sababu hawana skills inasikitisha sana as what went wrong na our Education System?...Kama Wazazi we have failed our youths na kama Taifa pia like binafsi mpaka ninamaliza High School nilikuwa tayari ninauza Siagi so sikiwahi kuwa na idea ya kuajiriwa ever in my life na bahati nzuri sana nikaenda Majuu kule nikakutana na Education System ambayo ni Full Practical na Self Reliance kwa mfano nilipoanza College Belgium I was shocked kugundua kwamba kila Mwanafunzi Darasani alikuwa anafanya kazi Part Time mahali hakuwepo hata mwanafunzi mmoja aliyekuwa anakaa tuu nyumbani bila kazi analipiwa.

Hata nilipohamia USA nilipoanza College tena mambo yalikuwa yale yale nikajifunza kusoma na kufanya kazi na kujilipia mwenyewe my Education now for that kind of system ni vigumu sana kwa mwanafunzi kumaliza Shule akakosa ajira cause like me mpaka namalizia Degree ya Tatu tayari nilikuwa na kazi nzuri ambayo nilikuwa nimeifanya kwa muda mrefu huku ninasoma Shule so ulikuwa ni uamuzi wangu kuendelea nayo au kutafuta mpya inayofanana na Elimu mpya niliyoipata ...hapa Bongo ni tofauti kabisa Vijana wetu wanasoma wakisaidiwa na Wazazi huku wakisubiri ajira za Serikali wakimaliza Vyuo na Process ya kusoma haina kabisa anything serious cha kuwatayarisha kuingia kwenye ajira au hata kufikiria KUJIAJIRI.

Halafu Wabongo tunatumia muda mwingi kulumbana na mambo yasiyokuwa na Tija kwa Taifa LETS CHANGE OUR EDUCATION SYSTEM! - le Mutuz

Leave a Reply