Makamu wa Rais asherekea siku yake yakuzaliwa na watoto yatima!

Muheshiwa Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan siku ya Jana ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa. Katika kuadhimisha siku hiyo muhimuhi Makamu wa Rais alijumuika na watoto yatima wa kituo cha Mtakatifu Gaspar kilichopo mjini Dodoma na kula nao chakula cha jioni. 

Kwa kupita account yake ya Instagram Mh. Makamu wa Rais alisema  “Jioni ya leo nimejumuika na Baadhi ya Watoto Yatima wa kituo cha Mtakatifu Gaspar cha mjini Dodoma kwenye chakula cha jioni ikiwa sehemu ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa.”  Hayo ndio yalikuwa maneno yake ya shukran ya siku yake kuu. 

Nasi kwa Mara nyingine tuna mtakia kheri, baraka, na afya njema mama yetu. Mungu azidi kukuongoza na kukulinda ili uzidi kulitumikia taifa letu vyema!  Happy birthday mama! ??

Leave a Reply