Malkia wa nguvu 2017: Hongera sana Mwanaidi Mayowela, pongezi kwa Clouds TV!

Nilikuwa sijapata muda wa kuwapongeza washindi na waandaaji wa sherehe za “Malkia wa nguvu” hivyo naomba nichukue muda huu kuwapongeza!…………Kwakweli kama kuna kitu ambacho kimenivutia sana na kunigusa kwenye TV za Bongoland; basi ni hii sherehe ya Malkia wa nguvu. Sababu kuu yakunivutia nikuona kuwa waandaaji walichukua muda wao kufanya kazi ya kujua nani anastahili kupewa tuzo hiyo ambapo imekuwa tofauti sana na events /awards nyingi sana za “Wabongo” wengi kwani mara nyingi ni zakujuana juana. Yani authentication ya awards inakuwa haipo kabisa!!

Hongera sanaaaaaa Clouds TV mmenifanya niangalie hii event mara zote mlikuwa mkiirusha hewani! Natumaini na wengine wataiga mfano wenu. Pia hongera sana dada Mwanaidi Mayowela kwa kulitwaa taji kwani unastahili kwakweli! Ubarikiwe sanaaaaaa wewe na familia yako! Nawashindi wengine wote pia nanyi nawapongeza sana. Mungu azidi wabariki.

Malkia wa nguvu; Mchapa Kazi, Mbunifu,  Jasiri!

Leave a Reply