Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!

Hivi ule usemi wako wa “mtoto wa mwenzio ni wako” uliufuta baada ya kuvua kofia ya u-FirstLady!! Bado najaribu kukutafakari nia yako haswa ni nini?! Wahenga walisema “uchungu wa mwana aujuae ni mzazi” lakini mimi saa nyingine napingana na huu usemi kwani kuna watu hawajawahi onja machungu ya uzazi wala malezi lakini wanaumizwa na kuguswa na watoto wa wengine kuliko baadhi ya wanawake walio zaa! Hapa simuongelei  mwingine bali ni aliyekuwa mkuu wangu ya shule ya Kowak Girls Secondary school Sister Magdalena (R.I.P). 

Miaka 23 iliyopita, nilipopata ujauzito nilikuwa form 2 pale Kowak Girls Secondary school Wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara. Shule ilikuwa inaongozwa na wamishonari wa Catholic na huyu Sister Magdalena ndio alikuwa Headmistress (yeye alikuwa Mmarekani) na msaidizi wake alikuwa Sister Nyambosa  ambaye alikuwa Mtanzania. Sasa Sister Nyambosa kulingana na the so called “mila na desturi, sheria za Tanzania na dini” alitaka nifukuzwe shule!! Eti hiyo ndio adhabu yangu nikajifunze! But guess what?!! Sister Magdalena akasema NO! Hato hidhinisha hiyo barua ya mimi kufukuzwa shule kwani haoni logic ya hizo mila na desturi, pamoja na sheria za Tanzania. Yeye aliamini kuwa kitendo cha mimi kuwa mama kwa umri ule ni adhabu tosha! Pia nilikuwa mmoja ya wanafunzi wazuri pale shuleni hivyo hakuona kwanini aniharibie future yangu kwa kunifukuza shule ambayo technically angekuwa anaharibu future ya watoto wawili (mimi na kiumbe kilichokuwa tumboni mwanangu wakati ule).

Kufupisha story hii, wakafikia makubaliano yakunipa sick leave mpaka nitakapokua tayari kurudi shule basi wao walikuwa tayari kunipokea au kunipa uwamisho kwenda shule nyingine! Miezi sita baada ya kujifungua nilitafuta shule nikahamia, uhamisho wangu ulitumwa bila tatizo!! Shule niliyo hamia ilikuwa ni Nurulyakini Secondary school pale Mwembe Yanga, Temeke. Nilirudia form 2 kwani nilikuwa sijafanya mtihani wa form 2 nilipokuwa nimetoka Kowak. Wanaonijua vizuri wanaweza kushuhudia kuwa hata siku moja sijawahi kuwa ashamed kusema kuwa mimi nina mtoto. Kwani miezi mchache tu hapo shuleni nilianza kuwaambia wanafunzi wenzangu na hatimaye story zikafika hadi kwa walimu wote wa shule! Guess what?! Hakuna aliye jali wala kunifanya nijisikie vibaya kuwa mimi ni mama katika umri ule!! Walichojali ni academic records zangu! Tulipoingia form 3, nikachaguliwa kuwa Assistance HeadGirl, na nipofika form 4 wakanichagua kuwa HeadGirl na hiyo yote ni kwasababu ya jinsi nilivyo kuwa hapo shuleni walimu walipenda sana na kuniona as a blessing to their school.

Nakumbuka siku moja dada aliyekuwa ananiangalizia mtoto alikuwa anaumwa hivyo hakuweza kukaa na mtoto siku hiyo. Ilikuwa ni wiki ambayo tunafanya final exams review kwa ajili ya kuanza final exams za form 4!! Nilikuwa na 2 choices; ama nisiende shule nibaki nyumbani nimuangalie mwanangu au nimbebe mwanangu niende naye shule! Sikiliza mama, jinsi walimu wangu na wanafunzi wenzangu walivyo nifanya nijisikie wakawaida kama wao, yani wala sikufikiria mara mbili!! Nikamuogesha mwanangu nikajiandaa nikaendanae shuleni. Nipo darasani nasoma na mwanangu yupo pembeni yangu! Hakuna aliyeniona waajabu wala nini!  kila mtu alikuwa anamfurahiya mwanangu!! And for the records nilifaulu vizuri sana form 4!

Mama yangu sikiliza, tatizo lolote lile hata liwe kubwa kiasi gani ilikutafutiwa suluhisho la kudumu inategemea na attitude ya jamii husika na viongozi wake! Embu tafakari kama Sister Magdalena asingeweka msisitizo kuwa hato hidhinisha hiyo barua ya kunifukuza shule mimi ningekuwa wapi leo?!! Vipi kama walimu na wanafunzi wa Nurulyakini wangenibagua na kunitenga je mimi ningeweza endelea na masomo yangu?! Je, maisha yangu na ya mwanangu yangekuaje kama nisingepatiwa nafasi ya pili ya kufanya matengenezo?! Maana hivyo vyeti vyangu I mean my academic records ndio vilivyonileta hapa nilipo leo hii!! Labda nikwambie tu kuwa Nurulyakini ni shule ya Waislamu!

Hii tabia ya kutokutoa nafasi ya pili kwa “wakosaji” ndio inaleta matitizo mengi ndani ya Tanzania kama mambo ya vyeti feki, na forgeries nyingine! Viongozi wenye mtazamo kama wako ndio wanao changia matatizo kama hayo niliyo yataja katika jamii yetu!

By no means, siungi mkono maswala ya wanafunzi wa kike kupata mimba wakiwa mashuleni. Hata mwanangu analijua hilo kwani niliongenae mapema mno nilipo ona anaakili za kutosha kuelewa kile nitakacho mueleza. Lakini naomba uwelewe kuwa tatizo si kupata mimba, tatizo ni familia, jamii, na serikali imeshindwa kuelewa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuelimisha familia pamoja na jamii nzima kuhusu swala la kujamiiana na changamoto zake haswa kwa watoto wakike! Leo hii unasema waliopata mimba wasiruhusiwe kuendelea na shule, ok! Fine! Vipi wanao adhirika na magonjwa Kama HIV, gonorrhea, genital herpes, syphilis, n.k  hao mnawafanyaje?! Kwani hayo pia siyanatokana na ngono??! Hauoni kama kuna haja ya kuwataka madaktari wawataharifu shule mara tu wampatapo mwanafunzi anaugonjwa wowote wa zinaa ili nao wafukuzwe shule?? Mbona mnawaonea wanaopata mimba peke yao?! Ooh! Au mnaonaje muanzishe sheria ya watoto wakike kukagualiwa kama wako sexually active au bado kabla ya kuingia shule katika kila muhula?! Labda hiyo ingetoa fursa sawa kwa mabinti wote! Na wanaume je mgewafanyaje?!!! Acha ubaguzi na unyanyapaaji mama yangu?!

***ITAENDELEA……… ***

One thought on “Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!”

Leave a Reply