“Mimi nimejifunza kutonung’unika sana kwa kila linalotokea”Jacqueline Mengi

Umeshawahi kulia na kusononeka kwa mfano kwasababu ya kukosa maelewano na mwenzi wako mpaka ikapelekea kuachana halafu baada ya muda kupita ukagundua kuwa kilichotokea ilikua ni njia ya kukufungulia mlango mpya wa baraka? Kama binaadamu tungekua tunajifunza kutokana na historia hata kama sio yetu binafsi tungeepusha masikitiko mengi sana. Mimi nimejifunza kutonung’unika sana kwa kila linalotokea maana kila nililoliona ni tukio baya baada ya muda niliona jinsi ambavyo ilikuwa ni njia ya kuruhusu baraka ziingie kwenye maisha yangu.Everything happens for a reason therefore be grateful for everything. Asubuhi njema…..

Leave a Reply