Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu……. !

Kuna watu wanajifanyaga kuwa wao wanajua jinsi ya kufanya maamuzi mazuri kuliko wenzao, wako wepesi sana kusema matatizo ya watu na kuhukumu wengine kwa maamuzi wanayo fanya! Sasa ikatokea maamuzi uliyofanya hayakuzaa matunda mazuri mbona utakoma! Lakini ikiwa yeye ndio  kafanya maamuzi ambayo siyo sahihi atatafuta kila njia ya   Ku justify hayo makosa na kutumia gharama zote kuficha makosa yao. Sasa huyu Tamar Braxton ni mmoja ya watu wenye tabia kama hizo. Yani huyu alikuwa mwepesi sana kusema dada zake kuwa wamechagua wanaume wasiofaa  na ndio maana ndoa zao zina matatizo. Msikilize hapa ?

Kuna siku pia alimuita Ex husband wa dada yake kuwa ni "baby sitter" kwamba hana faida yoyote kwa dada yake wala watoto zaidi ya kuwa kama mfanyakazi wa kulea watoto. Dada yake alichukia sana na kuwambia kuwa Andre anaweza asiwe mume mzuri lakini ni baba mwema sana kwa watoto wao na hato weza kumvumilia kuona anamdhalilisha baba wa watoto wake. Tizama hao ?

Sasa leo hii yamemkuta matatizo kwenye ndoa yake mpaka anadai talaka sasa amekuwa MBOGO! Hataki hata kuongea na familia yake kuwaelezea ukweli kuwa ndoa yake naye ilikuwa ni mbovu tu kama yao ila alikuwa anaficha. Yamemkuta yale yale aliyokuwa akiwaambia dada zake, kwa aibu anashindwa hata kuwaambia dada zake kuwa amekwenda mahakamani kudai talaka. Dada zake wamejua kuwa mdogo wao amekwenda mahakamani kudai talaka  baada ya kusoma  kwenye mitandao.  Halafu dada zake wanapotaka kumuuliza ili wajue ukweli anakuwa mkali kama pili pili!  Majibu ya shortcut huku akitumia Mic kama "defensive" mechanism! Embu mtazame hapo ?

Unajua kama hayajakufika kama hujui ku sympathize na matatizo ya watu basi ni bora ujifunze kunyamaza kuliko kuhukumu wenzio unafanya wajione  like something is wrong with them! Wakati jambo kama hilo au tatizo lolote lile linapokukuta unakuwa mkali hutaki kuulizwa  wala husikii kitu!

Nasikia Tamar amekuwa very sensitive na ame withdrawal kutoka kwa familia yake. Yupo very protective kulinda image ya mume wake.

Masikini Vince anatia huruma! Anataka ku fight for his marriage. Nafikiri ni vile anajiona yeye ni yatima na amekuwa kwenye Braxton family karibia miaka 20 na zaidi. Kumbuka Vince alikuwa Manager wa Toni Braxton kwa takribani miaka 10. Mkataba wake wa umeneja ulisitishwa baada ya kuamua kumuoa  Tamar kwani Toni alisema hawezi kuchanganya undugu na kazi akimaanisha Vince amekuwa shemeji yake. Wakati huo huo kunatuhuma za domestic violence kati ya Vince na Tamar ambazo zimetolewa na mama yake Tamar. Kama asemacho mama mkwe wake  ni ukweli basi nitakuwa nimeshangaa sana!! Kupiga mwanamke?! No! big No!

Mmh! Wishing her the best, nimefurahi sasa atajifunza kutokana na makosa. Maybe she will learn to put her ego down because she learned her lesson in a very hard way!

Leave a Reply