Mlee mtoto katika njia impasayo!

  Kwanza naomba mniwie radhi wapendwa wangu ambao ni Waislam. Mimi ni Mkristo hiyo mambo mengi nikiongea nita refer to the Holy Bible kwani hicho ndicho kitabu nakijua na pia sipo hapa kwaajili ya dini hivyo sitokaa ni compare Quran na Bible! Sasa Biblia katika kitabu kile cha Mithali 22:6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa  mzee! Hizi picha za birthday ya Nillan ambazo zinaonyesha wako mezani wakila chakula na kunywa zimenifanya nikumbuke hilo fungu la Mithali 22:6!  Hivi wazazi wangapi mnawalea watoto wenu kwa kuwafundisha kuwa chakula ni kitu cha kuheshimiwa hivyo ukila lazima uwe na nidhamu?! Kuwa hupaswi kutembea huku unakula kama mkimbizi au mtu aliye vitani!! Unamfunza mtoto kuwa ni lazima ukae chini / mezani wakati wa kula napia ni marufuku kuongea nachakula mdomoni!!  Kama wewe ni mzazi unaye ishi katika mazingira mazuri na ungependa mtoto wako aende mbali zaidi ya hapo ulipo wewe, je umemwandaa mtoto wako kukabiliana na mazingira hayo?! Kwamfano, ungependa mtoto wako awe na uwezo wa kwenda naye kwenye 5* hotel nakula chakula mbele za watu nilazima umfunze mwanao kukaa mezani wakati wakula na atulie mpaka atakapo maliza chakula. Nilazima umfunze mtoto kutumia visu, uma, na kijiko tena umfunze mara kwa mara ili azoee kuvitumia kama Zari alivyofanya kwa watoto wake. Hao watoto kukaa mezani kwa utulivu hivyo nakula kwa ustarabu si kitu ambacho wamefanya mara moja, hapana! Hao watakuwa wamefunzwa na wamezoea! Ni malezi mazuri sana haswa kwa karne hii ya 21 ambapo dunia imekuwa kama kijiji  huwezi jua ni wapi na nani mwanao atakutana naye hivyo lazima kujua jinsi ya kumudu mazingira!  Nilipokua nyumbani Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu, watoto wake mdogo wangu walikuja kunitembelea. Sasa wakati wakula mie nikamwambia dada wa kazi kuwa haina haja ya kuweka chakula mezani aweke mkeka tukae chini tule! Tuliokulia kwenye mikeka utatujua tu ???  mwe! Kwani hao watoto waliweza kula?! Mara namuona yule mdogo anaangaika kuvuta kiti karibu na mkeka  na mkubwa  wa kike kalalia tumbo huku akijaribu kula ?? Nikawa nashanga, ndio mama yao akasema unajua wanangu hawajui kula huku wakiwa wamekaa kwenye mkeka!! Akasema "Wakenya hao wanajua kula ni mezani tu" ?? mbona yalinishuka ikabidi tuhamishie chakula mezani, basi wakawa na amani wakala kwa furaha!  Mdogo wangu alipoona hizi picha za Tiffah akanitumia na kusema kama mtoto wake angepiga picha hiyo ambayo ameshikilia glass ya juice baada ya picha za birthday ya Nillan kutoka basi baadhi ya watu angefikiri kuwa ameiga kumbe hivyo ndivyo alivyo walea watoto wake!...... Wazazi embu achaneni na kuwapa watoto glass za plastic kwanza zinaleta Cancer ??  honestly, bora umpe mtoto kikombe cha bati kuliko plastic! Nunua zile glass ngumu mfundishe mtoto kushika na kutumia bila kuvunja ili siku ukiwanae 5* hotel upati shida kwani kazoea! #Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee!!

""* Picha zote za Tiffah nimezitoa kwa Instagram page ya princess_Tiffah***

Leave a Reply