Mmesikia? “Mke mzuri halindwi”!!

Wahenga waliyaona na kushuhudia kuwa ni ukweli haiwezekani, ndio maana wakatoa “angalizo” au muongozo ili vijana wanaokuja wajifunze bila kufanya makosa!……….Sasa Wahenga walitoa angalizo kuwa “mke mzuri halindwi”!! Mke nzuri anahitaji MATUNZO NA HESHIMA basi wala huangaiki naye anatulia ndani ya nyumba anapendeza kama waridi!! Sasa wewe unadai unamke mzuri halafu amani rohoni hauna umekuwa FBI wa penzi lako mwenyewe? Inahusu!?! Mke nzuri muwekee mazingira mazuri ya kuishi kama haya ya Jacqueline, kiyoyozi masaa 24, maji safi ya kunywa na kuoga unafikiri atatoka? Aende wapi?! Sasa wewe mke mzuri halafu unampangia chumba uwanja wa fisi karibu na “corner bar” utafikiri alikwambia yeye Bar Maid ??? halafu wewe ndio mkali mtu asipite karibu yenu ??  Jamani mke anahitaji matunzo nyie wanaume! Mke anahitaji heshima, sio kumchanganyia wanawake kila asubuhi!! Yani hata heshima kwa wanawake wenzake hapati kwasababu ya mumewe!! Embu muige mfano hapa!! Hata kama hauna hela ya kumjengea nyumba kama hii jaribu kumuonyesha thamani yake kwa kumuwekea mazingira fulani mazuri! Kha!……( tuache matani Jacqueline mzuri eeh)  That Foyer is one to die for kwakweli! Your house is beautiful! Safi sana!——–‘ Btw! Jacqueline, kwanini usinunue Miss Tanzania? Naamini wewe unaweza ukayapeleka na kuyapa hadhi yanayostahili kwani uwezo wa kupata sponsors wa uwakika unao! Embu tafakari Miss wetu! Ongea na Dr. Mwakyembe na Lundenga uyachukue mpendwa! ??

Leave a Reply