Mother and daughter moment

FB_IMG_1452434006782-1Mama na mwana! Dr Victoria Kisyombe na binti yake Janet Kisyombe. Ngoja niseme ni jinsi gani niliwafahamu mama na mwanaye…..

Janet na mimi tulikutana na kujuna miaka ya nyuma nilipohamia mji wa Wichita, Kansas. Alikuwa ni rafiki ya kaka yangu aitwaye Joseph. Sasa katika maswala ya kutaka ride kaka yangu alimuomba Janet anisaidie kwani mimi nilikuwa sina US driving license. Basi katika watu ambao walinisaidia na maswala ya usafiri Janet ni mmoja wao. Na siku ya leo naomba nimshukuru hadharani; asante sana Janet ubarikiwe zaidi ya hapo. Kwani ni wachache sana wenye moyo wa kusaidia wenzao bila kudai malipo yoyote. Kuishi hapa USA nimejifunza mengi zaidi kuhusu sisi Watanzania. Napia nimeelewa kwanini sisi Watanzania hatuendelei zaidi ya kuwa na chuki binafsi na watu bila sababu yoyote ya msingi. Anyway ipo siku nitaliongelea hili swala kiundani zaidi. FB_IMG_1452620273715Ok. Kuhusu Dr Victoria Kisyombe, yeye sijawahi muona uso kwa uso bali niliona mahojiano yake na CNN-Africa mwaka juzi. Lakini akili haikunijia kuwa anaweza akawa na undugu na Janet. Kwakweli niliguswa sana na story yake mpaka nikashare na mtu mmoja (ambaye by then nilifikiri ni rafiki mwema kumbe adui number moja, hivyo sasa siyo rafiki yangu tena). Sasa mwaka jana tuka connect na Janet Kisyombe kwa mara nyingine kupita Facebook. Sasa katika kuangalia picha nikaona picha za Dr. Victoria Kisyombe! Nikamuuliza Janet uhusiano wao akaniambia ni mama yake. What a small world?! Yani nilihisi kulia, nikamwambia mama yako ni mmoja ya watu ambao wameni inspire sana, na nilikuwa natamani siku moja kuonana naye. Wote wawili wakafurahi na sasa nashukuru Mungu tumeshakubaliana kuonana siku moja, tukae chini tuongee mambo mbali mbali. Dr. Kisyombe ni mama shujaa anayeguswa na maisha ya wakinamama walio katika mazingira magumu ya kujikwamua kiuchumi. Hivyo akaanzisha organization yake ya kusaidia wakina mama. Soma hapa 

Kwakweli inasikitisha sana kuona wakina mama au watu kama Dr. Victoria Kisyombe ambao hata inchi za wenzetu wanawatambua lakini hawapewi nafasi ya kusikika katika jamii ya Watanzania   kwasababu tuu wahakutoka kwenye familia za wenye “pesa” au kwenye zile familia ambazo wazazi na watoto wao wamesomeshwa na “kutanua” kwa kodi za Watanzania, au kwa kukosa connection ya watu wa “mujini”. Asante Mungu kwa kutuletea Dr. Magufuli, sasa hivi tutajua nani mwenye pesa halali / safi Tanzania na nani walikuwa na pesa za ufisadi. Enzi za mimi mtoto wa “fulani” hakuna tena sasa hivi ni  Enzi za #HapaKaziTuu …………..Kwa mara nyingine nasema asante sana Janet, and looking forward to meet your darling mother one day. Mbarikiwe sana. 

4 thoughts on “Mother and daughter moment”

Leave a Reply