Mother and daughter moment!

Mama na mwana wakiwa katika mazingira safi kabisa ya Kisumu International Airport, hapo nchini Kenya! Hii Airport kwa muonekano tu wa nje inaonekana ni safi zaidi ya ile ya kwetu pale Bongoland! Japo hii ipo nje ya mji wa Nairobi lakini inavutia kwa usafi sana........Ni nini haswa tatizo letu sisi Watanzania! Maana hata mazingira yatengenezwe mazuri vipi haichukui muda utashangaa jinsi yalivyo chafuliwa, na kuharibiwa! Saa nyingine tunailaumu serikali kwa mambo ambayo ni sisi wenyewe ni tatizo! Kweli aliyeturoga kafa!.........Picha hii imepigwa week na siku kadhaa sasa wakati mama Igogo alipokuwa amekwenda kwenye msiba kwa wakwe zake na binti yake!

Leave a Reply