Mother’s Day 2018: Je, ungependa ku-share nasi hadithi / shukrani ya mama yako mpenzi?

Mother and daughter moment: Mother's Day inakuja ni jumapili ijayo, je umepanga kufanya nini au kumfanyia nini mama yako? Mimi binafsi nitakuwa Washington, DC niki enjoy kidogo na mama yangu! Kwani hii itakuwa Mother's Day ya kwanza kabisa kwa mama yangu kuwa hapa Marekani pamoja nami; hivyo nitaitumia nafasi hii vyema. Sasa basi tuambie kuhusu wewe. Je, ungependa kuShare nasi stori ya mama yako au kutoa shukrani zako kwa mama ukiambatanisha na picha ya mama yako? Basi wasiliana na alphaigogo.com kwa kutuma ujumbe kwa njia ya blog, Instagram DM, au Facebook nasi tutaweka ujumbe wako. 

**Zoezi hili linaanza rasmi leo hii mpaka JumaMosi.**
Asanteni 
Pichani ni mdogo wangu Janeth na binti yake Essy. #TBS 2017

 

Leave a Reply