MOYO ULIOJERUHIWA DAWA YAKE NI FARAJA

Mr and Mrs Ridhiwani, wamependeza sana! ?
MOYO ULIOJERUHIWA DAWA YAKE NI FARAJA kama huwezi kuwa faraja kwa mwenzi wako basi ujue husitahili kupewa nafasi hata ya kumwambia HABARI... Maana halisi ya mahusiano ni wawili kunia mamoja, Huwezi kuwa MUME wake kama huwezi kuwa rafiki kwake, Kuifikia heshima ya MUME ipo ngazi inayokubidi kuipanda nayo ni "HURUMA" Mtu ambaye hana huruma hawezi kujuwa vile mwenza wake anaumia, Mtu asiye na huruma hawezi kujikosoa, Mtu asiye na huruma hawezi kujifunza maumivu ya mwingine, Mtu asiye na huruma hajui kabisa KUHESHIMU! Na mtu huyo hata mwenza wake akilia mbele yake yeye hufurahia na kujiona mshindi, Mtu asiye na HURUMA NI KATILI tena amejawa dharau na majigambo, ni mwenye kujihesabia haki muda wote... lakini pamoja na yote hayo MWANAMKE NI MVUMILIVU wala asiyekata tamaa akijenga tumaini kuwa MUMEWE ATABADILIKA wakati huo akiendelea kuumia na kulia kila kukicha, Baadaye unakuta Mwanaume huyo amemuolea Mwanamke mwingine lakini mwanamke huyo anahamia kanisani kumlilia MUNGU ili amrejeshe mumewe, Lakini mumewe hubeza na kumwambia anapoteza muda huko makanisani mnakwenda kujifunza umbea, Still Mwanamke huyo yupo tu! MOYO wa Mwanamke ni MTAMBO... Wallah wakiungana wanawake wanne kwa uvumilivu wao ni KIWANDA???

** Writen by: Elista Relief Heart ..........Picha ya Ridhiwani na mkewe haihusiki na story hii! Nimependa tu! **

Leave a Reply