Mpaka kifo kitakapo tutenganisha!…….. R.I.P Mr and Mrs Ngombale Mwiru!

 Pichani hapo juu ni sura ambazo naamini zinafahamika na watu wengi kwenye jamii ya taifa la Tanzania. Ni  marehemu mzee Kinguge Ngombale Mwiru na mkewe marehemu Peras Ngombale Mwiru! Wanandoa hawa walianza maisha ya ndoa wakiwa vijana na wamedumu kwenye ndoa yao mpaka kifo kilipo watenganisha kwa jumla ya siku 28! Sasa wote wapo kaburini wamelala usingizi wa mauti! What a journey! What a lovely love story to tell! Naamini hawa wazee wetu walifunga ndoa ya serikali kwani watu wanao wafahamu wanasema mzee Kinguge Ngombale Mwiru alikuwa hana dini! Sina huwakika kama alikua ANAAMINI MUNGU!? Kuna watu wanaamini Mungu yupo lakini hawana dini! Sasa Sina huwakika na hilo, japo mama yeye inaelekea alikuwa muumini mzuri wa dini ya Kikristu wa thehebu la Katoliki! ....... Natamani tungekuwa na video ambazo hawa wazee wanatueleza maisha yao ya ndoa yalikuaje, na nini walifanya  kuhakikisha ndoa yao inadumu haswa ukizingatia mmoja alikuwa hana dini napia mwanasiasa! Wakati mama yeye ni muumini wa Katoliki na ameishi maisha yake pretty much privately! ...... Yani tungetamani  kujua when things got heated in the house what did they do?! Walipiga magoti wakasali, au walimuita mganga wa kienyeji, au walitafuta cancellers?! ......... Hapa ndipo wenzetu wa nchi zilizoendelea  walipo tupiga bao! Wazee kama hawa wenye vitu fulani ambavyo jamii ingeweza kujionea na kujifunza toka kwao wangekuwa wamesha fanyiwa interviews kibao kuhusu maisha yao ya ndoa na familia mbali na siasa ili jamii inufaike! Marehemu naamini walibahatika kupata mtoto moja aitwae Kinjekitile kama mnavyo waona hapo pichani! ........ Poleni sana wanafamilia na wafiwa wote! Poleni sana Watanzania!  Bwana alitoa na Bwana ametwaa sifa na utukufu ni zake milele zote, Amen!

Leave a Reply