“mpenzi yoyote yule anayekupiga kuna siku ATAKUUWA TU sio mtu wa kumchezea”

Regrann from @lemutuz_superbrand  -  LIVE STRAIGHT TALK: FACTS The Art of Love and Hate takwimu zinaonyesha kati ya Mwaka 2016 na leo 2018 Jumla ya Wananchi 341 wameuliwa na Wapenzi wao kati yao ni Wanawake ndio waliouliwa zaidi yaani Wanawake 247 na waliobaki ni Wanaume waliouliwa ni 94 wote wamekufa kwenye mapenzi na hasa ndoa inasikitisha sana ...kinachosikitisha sana ni the fact that Jamii imenyamaza kimya Wabunge wetu hawana hata habari na Wanasiasa wetu ndio wamekuwa mabubu kabisa sababu? ni Maadili yetu zaidii ya kuficha mapungufu ya Ndoa kwa Mwanaume kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mke wake ni Aibu sana na Mwanamke kulalamika kwa jamii kuwa hamuelewi mumewe pia ni Aibu ya kuahindwa kuficha mambo ya ndani ya ndoa na matokeo yake ndio haya Taifa limepoteza Nguvu kazi ya Wananchi 341 ...nani anatakiwa kuhusika na afanye nini? ndipo tunapokwama na ninarudia tena na tena kwamba huu ni wakati muafaka Serikali ikaanza kulitupia macho hili tatizo ambalo chanzo chake ni Mapenzi na hata kwenye kuua huwa wanajiamini kwamba wanafanya kitu sawa kwa niaba ya mapenzi yao kwa wanaowaua ...tunatakiwa kuimarisha our Social Welfare Services ziwe na Professionals wanaoweza kusuluhisha matatizo ya Ndoa mara wanapoarifiwa tu na hata wapewe nguvu za kisheria za kuwaweka Rumande Wanaume na Wanawake waanaonekana kuwa chanzo cha matatizo ya kufikia kupigana katika ndoa au mapenzi ....ninasema hivi hatuwezi kuwa na Viwanda imara kama hatuna Wananchi Imara na sisi wananchi its about time sasa tukaanza kuamka usingizini hakuna mapenzi ya kupigana pigana mpenzi yoyote yule anayekupiga kuna siku ATAKUUWA TU sio mtu wa kumchezea I mean mpenzi anayepiga ni hatari sana ni most of the times ni kwa sababu amekulia kwenye ndoa ya Mama yake kupigwa na Baba yake au Baba yake kupigwa na Mama yake guys usicheze na mpenzi wa aina hiyo cause atakuuwa ....ndio maana USA watu wa namna hii wakifungwa jela huwa hawachiwi maana hakuna Therapy wala Rehab inayoweza kuwasaidia isipokuwa kuishi jela tu ...kwa mnaopigwa na Wapenzi wenu please take action now kama hawezi kuacha muwache cause ataishia kukuuwa! - @lemutuz_superbrand  - #regrann

Leave a Reply