Mrekebisha tabia: Vyovyote vile utamchukulia lakini kwa wengine wengi bado anakuwa hero

Regrann from @mrekebishatabia  -  Kuna watu humchukia Mange Kimambi kwasababu mbalimbali.. Wengine sababu binafsi,  wengine basi tu,  wengine misimamo yake nk.. Vyovyote vile utamchukulia lakini kwa wengine wengi bado anakuwa hero. .. Yes ni Shujaa! Vyama vya upinzani vimeshindwa kupanga wanachama wao.... Wanaharakati wengi wameishia njiani.. Wengine wamejikita kwenye vyama na kusahau wajibu wao nk nk... But Mange ameweza kufanya kitu hata wengine pamoja na umaarufu wao nchini hawajawahi kuwaza amekuwa na ushawishi mkubwa wenye kushtua nchi! -

Yes ni mtu mkubwa mno mwenye uwezo wa kutikisa nchi...kila mtu alikua anaongealea maandamano hata vijijini watu wasiokuwa na mitandao wanajua khs maandamano... -

Binafsi nadhan anafanya vizuri sana kwenye harakati humo ndo mahala pake sahihi na akiendelea namna hii ataakumbukwa kwenye historia ya nchi yetu... Ndo ukweli wenyewe ambao wengi wanaupinga!! -

Kwa wananchi nao hawajaogopa kuandamana au kudharau ni vile tu Tanzania tunapenda amani hatujazoea masuala ya vurugu kuona vitisho na mapolisi kila mara kutoa matamko kuonya,  watu kukamatwa,  kunyimwa uhuru wao na mapolisi kuonekana kona wengi wakaona why amani iondoke wakati wanaweza kufanya njia nyingine? Njia nyingine ipi?  Sijui but naamini Mange Kimambi na washirika wake hawajashindwa lengo Lao wamefanikiwa kwa asilimia 73%

Niseme tu binafsi... Huwezi kulazimisha watu wote mawazo yao yafanane... Tunawahitaji akina Mange Kimambi wengi zaidi ili kuwepo changamoto maana wawakilishi wetu hawawezi, wengine kutishiwa.... Watu wote hatuwezi kuwa wapole,  wote ndiyo.. Wote mawazo mamoja... Mungu ameumba watu mbali mbali.. Wenye tabia, vipaji, hulka, wachokozi, wadadisi, mitazamo, wenye uthubutu nk.. Na mmoja wa watu hao ni Mange Kimambi..na nadhani hata kama kuna kitu unamchukia basi utapata kitu cha kumkubali.  - #regrann

Leave a Reply