Mtarajiwa wetu katika pozi!

 Jumapili ndio siku yake kuu, hivyo naomba nitumie siku hizi mbili kwa ajili yake ?? Huyu ni dada yangu bwana na furaha sana kwa ajili yake. Yani nyie siku nikifunga harusi yani ni miezi mitatu picha zangu tuu ?? mtakomaje sasa ??
 Akikata keki iliyotenezwa kiumaridadi kabisa
Tulimpa zawadi chache lakini zauwakika! Ni zawadi ambazo atakuwa anatumia mara nyingi, ubora na viwango vilizingatiwa sana, siyo mambo ya buy one get one free hapana ? chezea sisi ?

Mwenyezi Mungu amuweke salama Jumapili tushuhudie akiapa kiapo kitakatifu mbele zake Mungu nasi wengine tukiwa mashahidi wa hapa duniani! ??

Leave a Reply