“MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI.”~~~~~`Zamaradi Mketema

TV host Zamaradi Mketema

Kwangu mtoto kufanya hivi sio fahari ni Aibu, Hawa ndio aina ya watoto anakuwa anawaza kitu kimoja tu kichwani mwake, Kumridhisha mwanaume, juhudi zake atazielekeza kwenye kutafuta style mpya, bila kusahau vitu mbalimbali vya kupagawisha wanaume. Na wengi wa aina hii bahati mbaya waliowazunguka wanaendelea kuwatengenezea mazingira ya namna hii, wanakuwa wakiamini MAISHA NI MWANAUME TU, na ili uishi nae nguvu yako uilekeze kwenye KITANDA TU. Asilimia kubwa ya maongezi yao yamejaa hayo akiamini ndio UBORA, wanasahaulishwa kabisa kuwa kuna zaidi ya hayo kwenye maisha, wanabaki na mawazo mgando na kubaki kwenye dunia yao ya peke yao, ndio wale utasikia wanamtukana mwanamke mwenzao eti HUJAFUNDWA WEWE!!

Hapondiohuwainachekeshasababukwabahatimbayaufundajimwingiunaangaliasehemumoja tu and am sorry to say wengi WALIOUABUDU wanakuwa na mawazomgando mno yanayopeleke akuachwa na Dunia nyingine. Wadogozangu kitanda ni muhimu lakini haijawahi kuwasehemu KUU pekee ya UKAMILIFU wa mwanamke ama kumshika mwanaume, na kwa ulimwengu wa sasa kama unachojua ni kitanda tu.kunaathari nyingi utakazo kumbananazo hata katika hiyo ndoa unayoiabudu, na hakuna faida yoyote utakayo ipata, maishani zaidi ya kitanda. Mapenzi ni zaidi ya style mpya! Wamama tunaokuja tujitahidi kutotengeneza kizazi cha aina hii, tunaumiza watoto wetu, wanaishia kuwa malosers, washamba, akili ndogo, na hakuna cha maana kwenye maisha yao. Ninachoamini mtoto hafundwi siku moja, wiki moja, wala mwezi mmoja. Mtoto anaanza kufundwa tangu anazaliwa na katika ukuaji wake, MTOTO ANAFUNDISHWA NYUMBANI, Na ndio mafunzo mazuri au mabaya yanapotokea kulingana na imani unayomlisha, mazingira unayomkuza nayo na hata picha unayoionesha.

Hajawahi tabia mbaya alioishi nayo mtoto ndani ya miaka 13 au 14 ikabadilika ndani ya wiki moja za kumuweka ndani, hakuna!! Atawasikiliza tu lakini kama ana asili ya uchoyo ataendelea kuwa mchoyo, kama ana kaumalaya katakua, n.k Tuangalie RIGHT TIME ya kuwafunza hata hayo tulioamua kuwafunza kama ndio kudumisha mila na tamaduni, hakuna ubaya wa kumfunda mtu anaeingia kwenye ndoa lakini hakuna utamu wowote wa kumfunda mtoto wa miaka 12, 13, 14 au 15 ambae hana pa kuyapeleka hayo mafunzo, na hata hao wanaoingia kwenye ndoa kuna haja ya kuwapa LIFE SKILLS na sio kuwashibisha kimoja tu kisichokuwa na faida ya moja kwa moja katika ndoa yake!! Maisha yana changamoto nyingi sana, tusiwatengenezee utumwa wa akili na kuwafunga humo, kwanza angalia hata watoto ama wasichana wengi waliokulia kwenye imani ya kufundwa na kufundana katika hali ya kuabudu walivyo ama wanavyoishi kwenye jamii zao ama ndoa, kama hajaachika basi ana ndoa ya pili au ya tatu, wengi WANASHINDWA KULINDA NDOA ZAO na mpaka sasa nimefeli kujua kwanini!!

Walichokishiba wao ni kimoja tu. Hakuna bingwa wa malezi lakini mengine tunayatengeneza wenyewe, maana hapo utakuta mama yuko pembeni anashangilia na kupiga makofi huku akiona fahari mwanae anavyoyakata, jamani hata ukate mauno mpaka juu ya dari kama kuna vitu huna na hujielewi na kujitambua HAUTATHAMINIKA hata siku moja kwenye ndoa yako, na hao unaowaita wasiofundwa wataishia kukupiga bao tu kwenye maisha. TUAMKE.

Leave a Reply