Mtu kwao!

Mtu kwao jamani! Namshukuru sana Mungu kwa kumfikisha mama salama Tanzania. Aliondoka siku ya Jumapili na sasa yupo Bongoland akifurahi na ndugu zake na familia yake. Hapa ni akipiga soga na shemeji yake (baba yangu mkubwa) Mzee Charles Olung'a Igogo nyumbani kwake baba mkubwa. Mama yangu huwa anasafiri lakini mara nyingi baada ya siku kadhaa au wiki anakuwa amerudi nyumbani, hivyo kukaa kwake hapa U.S.A kwa miezi 3 na wiki mbili kumefanya iwe mara ya tatu kukaa nje ya nyumbani kwake zaidi ya mwezi. Mara ya kwanza ilikuwa 1998 ambapo alikwenda kwenye short course ya miezi minne (4 months) huko China, mara ya pili alikuja kunitembelea Kalamazoo, Michigan alikaa mwezi mmoja (1 month), na hii ya mwaka huu imekuwa mara ya tatu japo safari hii alikuja kimatibabu zaidi. Basi twasema asante kwa Mungu kwa mibaraka yote kwani jinsi mama alivyokuwa anaumwa halafu karibia  hospital zote ambazo zinaaminika hapo Dar es salaam wanachukua vipimo vyote majibu yanakuja  NORMAL ?? was a heartbreaking and a bit challenge to us kama tusingekuwa na uwezo wa kumleta hapa Marekani nani anajua sasa kama tungekua naye hai ?? hivyo tunakila sababu ya kumshukuru Mungu na kulisifu jina lake milele zote. Kwani wengi ni wagonjwa na hawana uwezo wa kwenda kutibiwa popote pale nje ya Tanzania au nje sehemu waishizo. Sisi ni nani Bwana!! Lihimidiwe jina lako milele zote. ??

Leave a Reply