Mungu awe nawe Lulu a.k.a Elizabeth! Pole sana mama Kanumba!

Nimenyama na hili swala la Lulu siyo kwamba simpendi au namtakia mabaya, hapana! Hili ni swala sensitive sanaaaaaaa! Pia kwenye familia yetu right this very moment tunapitia kitu ambacho karibia kinafanana na hili swala la Lulu japo mdogo wangu haikuwa swala la mapenzi na bado hajafariki!!  Yupo kwenye koma wiki ya tatu sasa anapumulia mashine!! Hivyo, nimejaribu kuvaa viatu vya Lulu kwakweli vimenibada mno! Napia nilipojaribu kuvaa viatu vya mama Kanumba kwakweli vimekuwa ni vikubwa sana havinienei! Kwa maneno hayo, nimeamua kunyamaza na kuomba Mungu kuwa hekima itumike zaidi! Mungu ampe huyo Judge hekima na kuzingatia mambo yote kwani hata Lulu naye ni victim. Bila kusahau kuwa Lulu alisha kaa ndani / jela karibia miaka miwii, kama ataweza ampe hata kifungo cha nje! ………..Mungu awe nanyi nyote poleni sana.

Leave a Reply