Mwanamke ni mtu shujaa, mwenye hekima nyingi, na muerevu sana!

Embu leo tuongelee hichi kiumbe ambacho Mungu alikiumba baada ya kuumba kila kitu! Mungu aliumba vyote lakini akaona kuna mapungufu mahala yani kwa lugha zingine naweza sema hakuridhika na kazi yake ya uumbaji mpaka alipo muumba mwanamke akaona vyote ni mema sana na uumbaji wake ukaishia hapo!

Labda niseme kwa siku ya leo nia yangu si kuongelea uumbaji wa Mungu bali nataka kuongelea moyo au nguvu ya ushujaa, hekima, na uwerevu ambao mwanamke amepewa na Mungu mwenyewe lakini bado tunajiona wadhaifu, hatuwezi kufanya kitu bila nguvu ya mwanaume kwanini? Kwakweli hata mimi sijui sababu bado najiuliza kwani kitu ambacho wanawake karibia wote tuna “struggle” nacho hata mimi mwenyewe- hello! Yes, me too ? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Hivi umeshajaribu kutafakari kuwa Mungu baada ya kumuumba mwanaume akaona kuwa hajakamilika kuna kitu kinahitajika ili huyu mwanaume aweze kufanya kazi kamili na kuishi kama mwanadamu? Na kitu hicho ni mwanamke! Hivyo, ukitaka kulinganisha utagundua kuwa mwanaume anahitaji nguvu ya mwanamke zaidi ili kuwa kitu kamili lakini mwanamke anaweza akafanya kazi na kuishi bila kumtegemea mwanaume sana (mnaojua maandiko ruksa kunikosoa). Naomba nieleweke, sijasema mwanamke hamuhitaji mwanaume la asha! Kila kitu ili kifanye kazi vizuri lazima kuwe na nguvu za hasi na chanya (mkono wa kulia na kushoto) ambazo zimeunganishwa pamoja katika kuleta nguvu kamili! Lakini saa nyingine utakuta upande wa kulia hautoi joto / nguvu sawa na kushoto hivyo inailazimu upande wa kushoto kutoa nguvu zaidi ili kuweka balance!

Zari The Bosslady

Nguvu ya ushawishi na hekima ambayo mwanamke amepewa ni kubwa sanaaaa! Tukiacha kisa cha Eva alivyo mshawishi mumewe Adamu kula tunda la mti waliokatazwa na Mungu, embu tuangalie kisa ya Malkia Esther kwenye Biblia! Jinsi Esther alivyotumia ushujaa na hekima ya hali ya juu kumshawishi Mfalme (mumewe) mpaka kuokoa watu wakwao! Kutokana na sababu mbali mbali watu wote waliogopa kumfata mfalme, lakini Esther alipoambiwa akasema lazima nifanye kitu kwani alijua kunyamaza kwakwe kungetoa tafsiri ya kuwa ameunga mkono maadui. Esther akajua wakati ni sasa kama ni kufa basi acha nife lakini lazima nikamuone Mfalme na kuweza kuongea naye juu ya jambo hili. Esther akatumia uerevu wake na hekima kupanga nini cha kusema, mahali pakusema, na muda wa kusema! Namwishoe akashinda na kuonekana shujaa kwa watu wa kwao!

Labda nifupishe hii story kwa kusema kwanini nimeandika, nia yangu nikutaka kuwakumbusha wanawake kuwa sisi ni viumbe vya kipekee sana ambavyo tumebarikiwa sana na Mungu lakini muda mwingi tumekuwa tukijikatisha tamaa sisi wenyewe aidha kwa kujua au kuto kujua! Tumekuwa waoga wa kutoa sauti zetu zisikike mbele ya wanaume. Tumekuwa hatutaki kueleza hisia zetu halisi na kujikuta tunaishi maisha yasio na uhalisia na kile kilichopo moyoni mwetu! Tumeshindwa kutumia nguvu ya ushujaa na ushawishi ambazo tumepewa na Mungu kuleta mabadiliko mbali mbali ndani ya maisha yetu na katika jamii zinazo tuzunguka! Tumekuwa viumbe dhaifu wakati Mungu alituumba kama mashujaa mkombozi wa mwanaume!

Japo kwasasa wanawake wengi wanaanza kuamka na kutambua hii siri ambayo ipo ndani yetu lakini bado inabidi tuamke zaidi! Mapinduzi yakweli yataletwa na mwanamke! Si unaona jinsi Eva alivyoweza mshawishi Adamu kula tuna na dunia yote sasa wanawake wanazaa kwa uchungu na wanaume wanaishi kwa jasho lao ?? Basi kama mnataka mabadiliko ya kuachana na siasa mbovu, kutokomeza ukatili wa aina zote, mazingira bora na salama ya kuishi n.k lazima muamke usingizini!

Usijione wewe hufai eti kwasababu unatabia kama za “Wema Sepetu” (sorry Wema I picked you), hapana! Mungu anapenda watu wote na anaweza mtumia mtu yoyote yule kufanya mabadiliko kwaajili ya utukufu wa jina lake! Kwa wale Wakristo kumbuka kisa cha Rahab au Ruth kwenye Biblia! Wanadamu tunatizama vitu kwa macho yetu haya ya dhambi hivyo nirahisi kuhukumu watu na kuona kuwa hawafai na hawana thamani lakini siku zote kumbuka kila mtu anathamani sana mbele za Mungu! Na kama Mungu ataamua kukutumia hakuna atakaye weza kuzuia! Kikubwa ni wewe kusikiliza ile sauti ‘ndogo’ inayo nena nawe kwa upole ndani ya nafsi yako kuwa badili njia zako!

Wanawake tunaweza kuibadilisha hii dunia kuwa mahala salama pakuishi tena kama hatuta waachia wanaume peke yao! Wanatuhitaji ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli! Siku zote kumbuka kuwa wewe ni shujaa, mwenyewe hekima, na muerevu sana!

****Zari’s picture has nothing to do with the story**

**Imeandikwa na Alpha Igogo

Leave a Reply