Mwanasheria mahiri Lau Masha “atua mtungi” wa Chadema!

Imenibidi niblog wapendwa maana siyo kwa ‘breaking news’ hizi 🤣🤣🙈…… Yule Mwanasheria mahiri msomi wa kimataifa Mh. Lawrence Masha ambaye alikuwa mwanachama wa CCM na kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya chama hicho na serikali zake baadaye akahamia Chadema. Sasa si aliubeba mtungi wa Chadema kwa ngata nene na ndefu ili uonekane hata kwa nchi za mbali?! Sasa basi leo hii ameamua kuutua “mtungi” wa Chadema kwenye kichwa chake yeye mwenyewe kwa hiyari yake!! Kwani ni mzito wakati hauna sababu yoyote ya msingi ya kuufanya uwe mzito kiasi hicho 🤣🤣 Nafikiri Mh Masha hakujua kuwa debe tupu haliachi kupiga kilele 🙈🙈 just kidding, wanachadema msinimeze.  Anyway mie siyo mwanasiasa hivyo sina cha kumshauri zaidi ya kumtakia kila la kheri katika kila kitu!

Leave a Reply