Hadithi ya dada yangu Grace-AnyangoNyoyoo!

FB_IMG_1451949046500-1??? acha nicheke kwanza lol! Je kwenye familia yenu mlishawahi kufanyiwa surprise ambayo kidogo iwatowe roho?! Basi huyu dada yangu alishawahi kufanya hivyo. Ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa ambaye alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya bibi yangu mzaa baba. Huyu dada yangu anaitwa Grace (official name), Anyango Nyoyoo (Jina la kilugha alipewa la bibi yake mzaa mama yake). Kwa sisi wa nyumbani tumezowea kumuita Anyango, waliosoma naye wanamwita Grace. Jina la utani ni Yondo sister (alikuwa anacheza sana muziki wa Yondo sister).  FB_IMG_1451949046500Sasa siku moja tuliamka tukakuta yupo ndani ya magazeti kuwa ameshinda kuwa “Miss Kibaha” ??? kipindi hicho alikuwa “modo” kweli kweli! Hiyo picha juu ni last month ambapo ana watoto wawili teyari na wote wako above 18 (Hakuwaambia kuwa ana watoto)! Basi surprise hiyo ilitokea nafikiri ilikuwa miaka kati ya 94-95 kipindi hicho bado wazazi wengi walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu mambo ya modeling na u-miss! Jambo hilo lilishtua sana wazazi haswa ukizingatia kuwa amezaliwa, kulelewa, na kukulia katika mazingira ya “conservative Sabato” hivyo was a big shocking  news to all of us! Masikini si wazazi wakamkatalia kuendelea na mashindano. Kwahiyo ndoto zake za “umodo” zikaishia hapo ??

Hapa kitu cha kujifunza nikuwa wazazi tusiwe too strict kwa watoto wetu! Si kitu kizuri sana. Kila kitu  ni kizuri kikiwa na limit na siyo extremely! Ni bora ujuwe mtoto wako kama anapenda mziki, au mambo ya umodo n.k kuliko kupata surprise kwenye magazeti au watu baki. Najua wazazi wetu walilelewa katika mtazamo tofauti na yetu hivyo mambo mengi kwao waliona kama ni uhuni au anasa. Yani maisha ya mtoto yapo so “structured” to the extent mtoto hapati nafasi ya kuwa mtoto na kupita hatua za ukuwaji ambazo anastahili kupitia. Malezi hayo ndiyo yanasababisha watu wengi kutoka Africa wanafanya vitu kinyume na umri wao. Yani mambo ambayo alitakiwa kufanya akiwa “teenager” anafanya akiwa mtu mzima  na familia yake! Vile vile imefanya watu wengi haswa Watanzania kuwa very judgemental! Yani watu wanaishi maisha ya “kukariri” na “ku-fake”kwa sana! Yule ambaye anaenda tofauti na the “normal route” anaonekana kuwa amepotea au hana maana yoyote! Wazazi na watu wengi wa nashindwa kuelewa kuwa kila binadamu ni unique hatufanani! Kwamaana hiyo hatuwezi wote tukafata na kufanya mambo ya aina moja! Wazazi msibane sana watoto wapeni uhuru kidogo wa kupumua, kutafakari, na kuchangia katika maamuzi ya maisha yao. Wasaidie kuishi kwa kutimiza ndoto zao nasi zenu wazazi! Ilimradi havunji sheria au hamkufuru Mungu basi wewe msapoti tuu! Kila mtu anawito wake hapa duniani inawezekana ikatofautiana au ikafanana yote ni sawa tuu! Basi hiyo ndiyo hadithi ya dada yangu kipenzi  Grace-AnyangoNyoyoo!

3 thoughts on “Hadithi ya dada yangu Grace-AnyangoNyoyoo!”

Leave a Reply