Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka 2018 na baraka za kufungua mwaka 2019!

Katika mwaka 2018 kuna mambo mengi sana yametokea, mengine yalikuwa mazuri sana, mengine ya kuhuzunisha na mengine japo yalikuwa ni changamoto za kutesa moyo na hisia lakini yamezidi kutuimarisha sisi kama familia. Shetani alitujaribu sana lakini ametukuta tupo ngangari imani yetu kwa Muumba wetu haitetereki. Kwajinsi tulivyo pitishwa kwenye hayo majaribu ambayo makali yake yalikuwa kama makaa ya moto nabado tukaishika imani yetu!? Basi nina kila sababu ya kusema kuwa kamwe imani yetu haitokaa kutetereka kwani tumeuona mkono wa Mungu hatuto uwacha milele! 

Kama nilivyo amua kuishi maisha yangu kwamba siku zote nita ipa nguvu mambo ambayo yananipa furaha na sio huzuni. Basi kwa mwaka huu wa 2018 vitu vingi sana vimenipa hufura lakini hivi ni vilinipa furaha zaidi. Kutembelewa na mama yangu mzazi, wadogo zangu, na mama yangu mdogo hapa kwetu Houston, Texas ni mbaraka wa peke sana. Nina kila sababu ya kusema Asante kweli wewe ni Mungu! Nitalisifu jina lako milele!
Jambo lingine ambalo limenifurahisha sana mwaka huu ni ujauzito wa my best friend, a sister near and deer to my heart. Mungu amembariki mtoto wa kike na amemuita jina Mercy sawa na jina la mwanangu mimi. Kwakweli namshukuru Mungu sana kwa huu mbaraka. Tunaomba amlinde na amkuze mwanentu. Atupe hekima na busara za kuweza kulea vyema watoto wetu ??

Leave a Reply