Ni muda muafaka wa kuelimisha Watanzania juu ya ugonjwa wa Alzheimer na Dementia!

Reposted from @millardayo Kama tunavyofahamu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi @ally_hapi ameendelea kupiga kazi kwa kuzunguka sehemu mbalimbali za Iringa kukutana uso kwa uso na Wananchi kumaliza kero zao kwenye ziara anayoiita ‘Mahakama ya Wananchi’.•Kwenye hii video ni wakati alipokwenda Ipogolo, akajitokeza huyu Bibi na kusema Mtoto wake na Mjukuu wake hawataki kuishi nae, wamemfukuza na wamemuibia laki tatu zake.•Pamoja na kwamba Bibi alikua anaelezea matatizo yake, Watu waliohudhuria walijikuta wakicheka kwa jinsi Bibi alivyokua anahadithia. (? @ayotv_ ) – #regrann

Nimekua nikiona video hizi ambazo watu wanakua wanacheka au kuwazomea au kuwaita wachawi wazee ambao wanakua kama wanatatizo la kujielezea vizuri! Hili swala naona hata viongozi wetu wanahusika sana katika kuendeleza hii tabia ya unyanyasaji juu ya wazee! sina huwakika kama wanajua kuwa huwenda kunatatizo kwenye ubongo ambalo linawasababishia kuwa katika hali hiyo? au huwa hawafahamu? Au wanafahamu lakini ujinga (ignorance) imetawala akili zao! Yani unatazama kiongozi anaongea na mtu mzima mwenzake au saa nyingine amemzidi umri lakini jinsi anavyo ongea naye unabaki mdomo wazi na hasira juu!

Yani mara nyingi utakuta hawa viongozi wanapenda kuongea na watu kwa hasira (sauti za kufoka) kana kwamba wanaongea na mtoto wa miaka 2! yani hawana sauti (tone) ya kuonyesha compassion and respect kwa watu wengine! Utafikiri kwenye seminar / training zao za uongozi hivyo ndivyo walivyo fundishwa kua kiongozi ni mtu wa kufoka foka kama pombe ya “wanzuki”, kukunja uso na kutoa maneno ya dharau! ?? Lakini napo ninesikia wengi wakisema Watanzania walio wengi bila kumgombeza na kutoa maneno makali hakuna linalo fanyika ??‍♀️??‍♀️ na hii tabia wanaileta hata wanapokua kwenye mahusiano yani ni full ubabe tu! ?? Ukitaka kujua tabia ya jamii husika angalia viongozi wake utapata jibu.

Marehemu bibi yangu mzaa mama, Mrs Valeria Cornel Awiti alifariki March 12th 2014, akiwa na umri miaka 88

Turudi kwenye mada yetu, naamini ni muda muafaka sasa kwa serikali chini ya wizara husika inayo shughulikia mambo ya wazee pamoja na ustawi wa jamii kuchukua jukumu la kuanza kuelimisha Watanzania juu ya magonjwa au mabadiliko ya ya akili yanayotokana na uzee au msongo wa mawazo (severe depression). Kuna magonjwa kama ALZHEIMER na DEMENTIA ambayo mara nyingi yanawakuta wazee japo sio wote ! Nimesema mara nyingi kwani kuna wazee ambao hawakumbani na haya matatizo na pia kuma watu ambao wana umri wakawaida (average age) na wamepatikana na Alzheimer na Dementia. Binafsi nimeshuhudia mtu wa 55 na 51. Hivyo hatuwezi sema kuwa kwa 100% ni magonjwa yanayo wapata wazee! Mimi si Doctor hivyo siwezi kuelezea katika lugha ya kitaalamu zaidi ili watu waelimike. Ila nimeshawahi kufanya kazi na watu wenye matatizo kama hayo nikiwa kama muhudumu wa afya (Nurse Aide) katika Nursing home pamoja na sehemu ya kuwaangalia wazee; kwa maana hiyo nina ufahamu kiasi juu ya Alzheimer na Dementia.

Kwa lugha rahisi naweza sema Alzheimer ni tatizo linalohusiana na kupoteza kumbu kumbu kwenye ubongo ( brain memory loss), ambayo huja kwa stage au aina tofauti tofauti. Kuna wenye tatizo la kupoteza kumbu kumbu ya mambo yaliyo pita kwa miaka kadhaa. Kuna wenye tatizo la kupoteza kumbu kumbu ya kitu chochote kilicho tokea jana au ndani ya siku kadhaa (past 24 hrs or within72 ), kuna wenye tatizo la kupoteza kumbu kumbu ya kitu ambacho kimepita hata dakika moja! Hizi zote zina stage yake sidhani kama kuna mtu anaanza kwa kupoteza kumbu kumbu zote kwa mara moja, ila huwa ugonjwa unaanza taratibu huku ukizidi kuongezeka kwa kuwa na uwezo mdogo sana wa kutunza kumbu kumbu za matukio au jambo lolote lile.

Wakati Dementia ni ugonjwa unaohusisha kupoteza kumbu kumbu pamoja na uwezo wakuishi kama binadamu mwenye akili timamu. Yani mtu mwenye Dementia lazima ana Alzheimer lakini mtu mwenye Alzheimer peke yake basi hawezi kuwa na Dementia. Japo hatua za mwisho (last stage) ya Alzheimer huwa wanakutwa na Dementia. Hapa ndipo unakuta mtu hawezi kuongea vizuri, hawezi kufanya vile vitu ambavyo kwa kawaida angeweza kufanya mwenyewe kama kula, kuoga, kwenda chooni, n.k Mtu mwenye Dementia anakua hawezi kujua jema wala baya (can’t reasoning and make judgment). Yani anaweza akachukua chupi nakuvaa kichwani, anaweza sio tu kusahau majina ya watoto zake bali anaweza akawakana kabisa kuwa yeye hana watoto.

Sasa vitu kama hivi ni muhimu kwa jamii kuelimishwa ili kuweza kutambua, na kuwa teyari kukabiliana nayo. Hii hali ya Alzheimer na Dementia huwa ni very terrifying kwa watoto haswa pale unapoona mama yako au baba yako sio tu hakumbuki jina lako bali anakukana kabisa kuwa wewe sio mtoto wake na yeye hajawahi kuwa na watoto.

Kama hawa wenzetu ambao elimu ya haya magonjwa wanapewa na kuandaliwa (financially, psysociologically, emotionally, socially, na spiritually) pindi mzazi au ndugu anapoonyesha dalili za Alzheimer lakini bado unakuta inakua ni ngumu sana kwao sio tu kukabiliana na ugonjwa bali kukubali hali halisi kuwa huyo sasa ndio mzazi wake ambaye yeye alikua akimtazama kama hero / shero yupo kwenye hali hiyo ambayo hawezi kutofautiana chooni na jikoni! Anaweza jisaidia mahali popote pale. Tafadhali serikali ya Tanzania chukuweni jukumu la kulewa wazee kwa uzito na mapana zaidi.

Mimi nikiwa mgongoni mwa bibi yangu. Ilikuwa ni mwaka 2010, nikiwa kijijini Kowak ambapo mama yangu mzazi amezaliwa na kukulia hapo. Hiyo nyumba unayo iona ndio nyumba mama yangu amekulia na mahali yake hapo ndipo ilipotolewa. Nilikuwa nimekwenda likizo Tanzania nakama ilivyokuwa kawaida yangu ni lazima kwenda kutembelea bibi na babu zangu pamoja na shangazi zangu. Yani siwezi kurudi Marekani bila kwenda kuwasalimu; halafu watu wakiona unapewa upendeleo na Mungu wanakuchukia ?? jamani wengine tumetemewa yale mate yenye harufu ya kuku wa kienyeji yana bimaraka yale asikwambie mtu ?? Hapa bibi yangu alikua ameanza kuonyesha early stage ya Alzheimer. Saa nyingine alikua anasahau hata njia ya kurudi kwake akitoka kanisani. Bibi yangu na babu yangu mzaa mama wao walikuwa hardcore Catholic church believers.

Huyu ni babu yangu mzaa mama, marehemu mzee Cornel Awiti. Yeye alifariki 2011 akiwa na umri wa miaka 92. Hizi picha ndizo picha tulipiga mara ya mwisho kuonana (February, 2010). Kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa sio wazee wote wanapata Alzheimer basi ndivyo ilivyokuwa kwa marehemu babu yangu. Yeye mpaka anafikia hatua za kukata roho alikua na akili zake timamu na kumbu kumbu zake zote! Yani at age of 91 aikua ananitajia dawa zote anazo tumia tena kwa kingereza. Yeye alibahatika kupata elimu ya utabibu enzi za mkoloni, hivyo alikuwa na ufahamu juu ya magonjwa yake na dawa anazo tumia. Babu yangu alikuwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa na BP ambayo yalipelekea kifo chake R.I.P. babu yangu missing you dearly ??

Pichani ni marehemu bibi yangu mzaa baba, Rhoda-Nyakanga Olwengo Igogo, akiwa na binti yangu Mercy mwaka 1996. Mwanangu jina lake lingine ni Teddy (Theresia) alipewa na babu yake kumkumbuka dada yake wa pekee. Baba yangu kwao walikua wanaume 3 na msichana mmoja. Shangazi alikua mtoto wa kwanza na binti pekee kwa tumbo la bibi yangu, japo nina mashangazi wengi kwani babu yangu alikua na wake wengi.

Kama ilivyokuwa kwa babu yangu mzaa mama basi ndivyo ilivyokuwa kwa bibi yangu mzaa baba. Yeye naye hakuwai kupatwa na tatizo la kupoteza kumbu kumbu, tena alikua anakumbuka mambo mengi ya zamani mpaka baba anamshangaa! Nafikiri mimi nimepata hicho kipaji toka kwake na kwa babu mzaa mama. My brain memory is good I mean ridiculously good ?? Yeye naye moyo wake ulianza kuwa mkubwa in the early 80s. Alifariki akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 88. Bibi yangu asili yake ni Kenya.

Juu ni wadogo zangu Janeth na Magreth pamoja na bibi. Hizi picha tulipiga July 2013, na ndio ilikua mara ya mwisho kumuona bibi yangu akiwa hai. Mwaka uliofuata alifariki (March, 2014). Wakati huu tulipokwenda msalimia ilikua tofauti na 2010. Hapa alikua ana Alzheimer na Dementia. Yani Alikua hawezi hata kukaa mwenyewe bila mtu kumshika au kuweka mto kwa nyuma kumzuia asidondoke. Alikua hawezi kula mwenyewe wala kujihudumia kwa kitu chochote kile, hivyo kulikua na mfanyakazi pamoja na mama zangu walipeana zamu za kwenda kumuona. Nashukuru Mungu sana na siku zote nasikia faraja kuwa katika watu wote pamoja na watoto zake bibi yangu hakuweza kunisahau, yani alikuwa ananikumbuka jina langu ila nikimuuliza juu ya mama yangu anasema ‘Cecilia alikufa siku njingi’ halafu anaanza kumlilia ?? na mtoto wa Cecilia ambaye anamjua ni mimi tu ?? Nakumbuka alivyosema eti safari hii ukiondoka niachie hiyo suruali yako nataka na mimi nivae ??

Kwangu mimi ilikua rahisi sana ku adjust na hali aliyokuwa nayo bibi kwasababu nilisha ona hizo dalili toka anaanza kupoteza kumbu kumbu, na nikawa na jaribu kumuelimisha mama how to handle her na kukubaliana na hali halisi. Kitu ambacho mama hakukubali ni kununua depends / disposable underwears (zile diapers za wakubwa) kwa ajili ya bibi. Yani nilikua na mwambia itarahisisha usafi wa bibi lakini hakuweza kukubaliana nalo kwani kwake aliona kama nina m-degrade mama yake. Sikukasirika kwani nilijua yupo kwenye denial ya kuwa mama yake hayupo tena kwenye hali ya utuuzima (mama) japo ni mama yake.

Anyway, mimi huo ndio wito wangu kwa serikali na jamii kwa ujumla. Tuwajali na kuwatunza wazee wetu kwa kutambua mabadiliko ya kiafya ya mwili na akili wanayopitia. Tuelimishane na watu waache kugombeza wazee tunapo waona wapo katika hali isiyo eleweka. Tambua lazima kunashida mahala na tafuta msaada kwa madaktari. Tuache hii tabia ya kufokea watu wazima.

***Video shukrani kwa AyoTV***

Leave a Reply