Nilifundishwa…………..!

Soma Comments kwa Masomo Mengi zaidi......

Monica Joseph, Financial Expert
Nilifundishwa Kupenda: Nimejifunza kujipenda Mimi kabla sijatoa mapenzi kwa wengine. Mimi kwanza. Jipende na Utapendwa. Sio tu lazima Upende usikopendwa. Hata asiekupenda Mpende. 
Nilifundishwa kuheshimu Wakubwa, hasa baba na Mama: Nimejifunza Kuheshimu Watu wa aina zote, bila kujali umri, jinsia, Utaifa, Uwezo wa aina zote. Tajiri Masikini, Kila Binadamu Mpe Heahima yake. Lakini Pia Jiheshimu na Utaheshimiwa. 
Niliambiwa asiefanya kazi na asile: Nimejifunza kufanya kazi kwa Malengo, nikipata nile kwa malengo nikikumbuka kuna kesho. Nimejifunza kufanya kazi kwa bidii lakini pia kupumzika (kufanya kazi kwa Malengo) pia kutunza Akiba ya kesho.
Nilifundishwa kwenda Kanisani: nimejifunza kufanya Ibada, kushukuru Muumba kwa kila Jema analonifanyia na kila Baya kwangu naliona kama funzo, nimejifunza Ibada ya Sadaka , sadaka ya Kusaidia wasiojiweza, na pia nimejifunza nikitoa mkono wa kulia hata wa kushoto usijue. 
Wazazi walinifundisha Mengi Mazuri, Ambayo yalikuwa msingi wa mafunzo Dunia iliyonifundisha. Nikiandika yote hapa nitawachosha. Bado naendelea Kujifunza........Dunia inaendelea kunifundisha. Naahidi kuwa mwanafunzi Mzuri. Yepi Mazuri Dunia imekufundisha? Share na sisi hapa tuendelee kujifunza. PS: Asante @kikifashions kwa Gauni zuri la kitenge.. (Nilifundishwa kusema asante pia?)  
Imeandikwa na Monica Joseph, au Monifinance (Financial expert) 
Maoni ya wengine: 
 

 

Leave a Reply