Nilisemaga huko nyuma na leo nasema tena!

Huko nyuma nilishasema kuwa, mzee Lowassa na mama Lowassa ukiwaangalia matendo yao utajua kuwa hawa watu ni wastarabu sana! Ni watu wako humble sana. Kila mtu anamapungufu yake lakini ukorofi wa kishamba usio kuwa na tija siyo style yao ya maisha wala tabia zao binafsi. Kuna watu tu wanataka kuwatumia hawa wazee vibaya lakini naona wako makini sana!! ……Ninayo yasema hapa siongelei kisiasa au makosa aliyoyafanya kwenye utawala wake hapana! Nawaongelea kama binadamu wenzangu raia wa hii dunia. Hayo yaliyotokea huko yalishapita tunaganga yajayo! …….. Kwakweli wameonyesha mfano nzuri sana kwa jamii ya jinsi KIONGOZI na raiya wa hii dunia inatupasa tuwe! Siasa si chuki jamani! Jana nilifarijika kuona Mayor wa Jiji la Dar ambaye ni mwana Chadema akimuongelea vizuri na kumsifia sana  aliyekuwa  kiongozi au former Mayor wa Jiji la Dar ambaye alikuwa ni mwana CCM (Dr. Didas Massaburi).  Ni mfano mzuri sana wakuigwa. ………anyway, ubarikiwe sana Mh. Lowassa.

One thought on “Nilisemaga huko nyuma na leo nasema tena!”

Leave a Reply