Nionyeshe marafiki zako nami nitakwambia wewe ni mtu wa namna gani!

Jokate Mwegelo (kushoto) akiwa na rafiki yake Sir. Theodora

Je, rafiki yako ni Nan?! Leo nimekwenda chungulia kwa mrembo wetu Jokate Mwegelo nikakuta kaweka picha za yeye na rafiki yake waliosoma wote secondary, nikafurahi sana moyoni kwani inaonyesha kuwa Jokate ni rafiki mwema. Pia nikaangalia rafiki yake huyo anamuonekano gani! Nikapata jibu, na hapa ndipo nikakumbuka ule usemi wa  wenzetu unaosema kuwa ‘nionyeshe marafiki zako nami nitakwambia wewe ni mtu wa namna gani’! “Show me your friends and I will tell you who you are”!  Watu unaokaa nao au kuongea nao kwa muda mwingi wana uwezo mkubwa wa ‘kukuambukiza’ tabia zao! Tabia zao zinaweza zikakujenga vyema au kukuangamiza! Pia kuna msemo wao mwingine unasema ” show me your friends and I will tell you your future” kwamba; nionyeshe marafiki zako nami nitakueleza maisha yako yabadae! Kwa mfano: kama wewe umezungukwa na marafiki waongo na wambea  basi wewe lazima utaishia kuwa mwanachama wa “SHILAWADU” ????? #Nionyeshe marafiki zako nami nitakwambia wewe ni mtu wa namna gani’! Choose your friends wisely! 

“Sr. Theodora nilisoma nae shule mmoja Sekondari. Alipokuwa Form 6 mimi nilikuwa F3. Ila saaa ndio mwalimu mkuu wa @stjchstz_official nilifurahi aliponialika kuongea na wanafunzi wake.” ~~~~~Jokate 

Leave a Reply