NITABAKI NA MAMA YANGU

         NITABAKI NA MAMA YANGUKijana mmoja daktari alikwenda kuposa kwa familia moja yenye uwezo wa kifedha na Mali zao .

Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Baada ya kujua kwamba daktari alimchukua mama yake aishi naye kwake baada ya kuona mama yake amekuwa ni mzee Sana.

Yule Binti Akamwambia chagua mawili kunioa mimi au kukaa na mama yako pale kwako ?? ,

kwa sababu ukinioa mimi sitokubali kukaa na mama yako pale kwako maana itakuwa ni kwangu sasa mama yako akae pale ili iweje?? !

Yule kijana daktari alimuelemewa. Hakujua la kufanya Kuhusu maisha yake na yeye yule Binti , Mke mtalajiwa , Uku akitafakari Binti anampenda Sana lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu kwakuwa alikuwa wanatoka wote kijiji kimoja pia Ndio kiongozi wake wa maisha yake.

Daktari alimwambia mwalimu :- 
Mwalimu kama nilivyokueleza awali kwamba nitaenda kuposa kwa yule kwa wazazi wa yule binti niliyekuambia yaani kwa Kweli moyo wangu unampenda mno yule binti siwezi Fikiria Mwanamke mwingine zaidi yake ,

lakini masharti aliyonipa ya yule Binti mke mtalajiwa ni kwamba nimfukuze mama yangu pale nyumbani kwangu ,,

kitendo ambacho kinaniumiza Sana Kichwa, mimi siwezi kuishi mbali na mama yangu maana amekuwa mzee.

Mwalimu sasa Nifanye nini na yule Binti nampenda vibaya mno ?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa yule kijana daktari , alimjibu kwa kumwambia:

Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao wa kukaa naye nyumbani kwako fanya mambo yafuatayo ,

Kwanza kabisa rudi nyumbani kwako , na leo usifanye chochote, ila Ukifika tu kosha mikono ya mama yako.

Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake.

Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya wasiwasi wowote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa, mikono kama mgongo wa kenge sasa ya kufanya kazi za sulubu wakati wa ujana wake.. ,

mama yake akamwambia mwanangu mikono yangu imegutaa kwasababu ya kufanya vibarua Ya kulima viazi na kupalilia mipunga ktk Mashamba Ya watu , Kwaajili Ya kutafuta Ada yako ya shule na uniform , 
Baba yako alifariki ukiwa mdogo Sana... 
Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, mashambani, kulima viazi, kukosha nguo, kufyeka barabarani na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea fedha ya halali bila ya kujali ugumu hiyo Kwaajili Ya kumtunza Mwanae .

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana maendeleo mzuri.

Yule kijana Daktari alilia sana akamwangalia viganja vya mama yake, akasema nakupenda mama yangu, nitakutunza kwa hali yoyote. .

Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia,

Mwalimu siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya huyo Binti msomi asiyejua thamani ya mama yangu.

Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi Mwalimu !

Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya Mwanamke msomi ambaye hajali thamani Ya mama yangu .. wakati mama yangu ameteseka maisha yake yote kwa ajili ya yangu.

Mwacheni aende tu akaolewe na mwanaume yeyote ampendaye mimi nitabaki na mama yangu

**Hadithi hii nimesoma kwa Ayo TV Facebook page**

Leave a Reply