Simulizi za maisha ya mzee Igogo kwa maneno yake mwenyewe!

MATUKIO YA LEO 19.02.2020 KWA MFADHILI:- 1. Bi Mole Akungo, mjane wa marehemu Akungo fundi magari, aliyekuwa Mwajiri wa Mkurugenzi John Orwanda. Anaumwa kisukari na kasikia tuna dawa ya Jufeel, pamoja na kukosa uwezo wa kujikimu.

2. Dada yangu wa kihindi Bi. Dirishan mlemavu wa Kibiongo aliniita kumtembelea kwake, ndiye aliyekuwa mwenye ofisi ya mtaa wa mshihiri na eneo la kurasini, nilipoanzia kampuni ya Utegi. Walinisaidia mno nilipokuwa naanza kampuni.

3. Rafiki yangu Bi. Zainabu Mbuguni, mlemavu wa macho (KIPOFU KABISAA), Aliniletea zawadi ya kazi ya mkono wake, kikapu cha ukiri, aliyoitengeneza mwenyewe kuanzia kusuka ukiri na kushona kapu hilo, ili nimpelekee mama Igogo kwendea sokoni, pia kaniletea zawadi ya miwa anazolima shambani kwake huko Kibamba.

Pichani yupo na Mwanasheria Asha Nassoro Mwanasheria wangu, na Maria Patrick Kagose, Mfadhili wangu nilitumia tiketi yake ya Bus na treni akiwa mdogo, kuijia jijini Dar, kwa upendo wa Mama yake, Dada Theresia Olung’a Igogo, aka Mama Maria.

***Imeandikwa na Sir O.O Igogo na kuleta hapa na Alpha Igogo (Blogger)***

Simulizi za maisha ya mzee O.O Igogo kwa maneno yake mwenyewe!

Za asubuhi marafiki wapendwa. Natumai soote tumeamka salama na hao wadogo wasiyoweza kuwasiliana kwenye group. Jana ilikuwa siku yangu ya kumbukizi ya mambo ya ujanani, kama alivyosema Mama ni kweli niliwahi kushiriki kanywaji kati ya mwaka 1972 hadi 1979. Nilishuhudia matukio mengi ya kuchekesha na kuhuzunisha ndani ya kipindi hicho. Nakubaliana fika na Rais Mstaafu wa Nchi ya Merekani OBAMA, alichokiandika kwenye kitabu chake kilichompa Umaarufu kiitwacho THE DREAM FROM MY FATHER. Aliota njozi toka Baba yake, na wala siyo ndoto!!!Nami mwaka wa 1979, nikiwa kazini wilaya ya Geita enzi hizo, kwenye machimbo ya dhahabu Nyarugusu, nikiwa Msimamizi wa Ujenzi wa mitambo hapo mgodini na Shirika la NECO Ltd. Nilienda kijiji cha jirani kumtembelea Mama yangu mdogo, aitwaye Leokadia Ombwa Olwengo, mdogo wake Rhoda Nyolwengo. Yeye na Vijana wake walikuwa wachimbaji wadogo wadogo. Nilikuwa na gari la Shirika na ikawa shangwe ya hali ya juu nilipofika hapo kwake. Kuku wawili walipoteza uhai ghafla kuwa kitoweo rasmi. Mama alikuwa mtengenezaji maarufu wa pombe ya kienyeji iitwayo APELO, yaani CHANG’AA🙆🏻 Ile furaha ya kukutana na ndugu zangu, nao kuniona nimekuwa Bosi naendeshwa na gari la Shirika, ikazua unywaji wa kilevi Apelo bila kipimo. Nilivyorudi kambini na kuingia chumbani sikujuwa. Ila usiku huo wa tarehe 7/6/1979, nilijiwa njozini na Marehemu Baba yangu Mzee William Olung’a Igogo. Aliniita kwa sauti ya juu sana nami nikamuitikia, nilikuwa napepesuka kwa ulevi, manano aliyoniambia ni:- MBONA UNAHARIBIKA KWA POMBE?? ACHA ULEVI, UNAPOTEA!! ACHA KABISA👏

Asubuhi yake nilipoamka, nilikuwa hovyo, hovyo kweli, kweli!!! Nilijikuta nimelala kwenye matapishi yangu yanayonuka kama taka teke teke ya chooni. Mchovu kupindukia, kichwa kinawanga na kugonga kama nyundo!! Ilinilazimu kujifanyia usafi huku nikiitafakari hayo maneno ya njozini, niliyohaswa na Marehemu Baba!! Sikuweza kwenda kazini siku hiyo, ilipofika mchana nilipata mlo kwenye kantini ya hapo Camp, na hatimaye nikaamwambia dereva anipeleke Geita mjini, nilikwenda moja kwa moja kwenye duka la Vitabu, na kununua kijitabu kidogo cha Agano Jipya. Nikaanza kuisoma msitari kwa msitari, kurasa hadi kurasa ifuatayo hadi mwisho, na nikairudia mara kadhaa.Ni kweli tangia siku hiyo hadi leo hii, zaidi ya miaka arobaini sijaweka kinywaji cha aina yoyote kinywani mwangu. Naamini bila mashaka ya aina yeyote kwamba Maandiko matakatifu isemavyo kwamba Baba na Mama yako ndiyo Mungu wako wa Duniani, ni kweli haswaa.

Mzee Igogo na mjukuu wake Cecilia Chaulo

***imeandikwa na mzee O.O Igogo (muhusika) na kunukuliwa hapa na Alpha O.O Igogo (blogger)***

“Life can be a rollercoaster and you will never know where you’ll end UP.” >>> Zari the Bosslady

Life can be a rollercoaster and you will never know where you’ll end up

From studying my Cosmetology course in the UK ( which hasn’t helped me) while doing house girl work to pay my accommodation (yes I’ve been a maid before) to running through buses to get to my next stop woodgreen where I worked as a Cashier and sometimes as an Isle packer in Sainsbury. Friend, I started out early wasn’t even sure why me. But the inner voice in me wanted better.

My dad had left, my mom was doing tailor jobs day and night I couldnt stand seeing her struggle I couldn’t stand her pain. I was living with my aunt in the UK who treated me like a step child. Gooosh🙄
Been through boutiques, long economy flights to china in between building a school and having babies. My music and tv career is a story for another day. Phew😪 All I’m saying, consistency is key. Doesnt matter where you are or what you do. Just do it.

I am the author of my life, my story, don’t rewrite it for me.! Let me be the one to tell it.
Throwbacks are good, reminds us of where we’ve come from and I think that kinda keeps you grounded.

William Ernest Mjee Oucho: Ndoto yangu ya kua Engineer

William Ernest Mjee Oucho
Napenda nishee na nyie story ya safari yangu ya kutafuta kuwa muhandisi tangu nimekua na mpaka sasa nilipofika. Twende sambamba utajifunza kitu hapa.

Mwaka 1993, Jumatano moja ya tarehe 09 mwezi wa Sita, mama angu alinizaa na kunileta duniani, na kunibarikia jina la William, ambaye alikua ni marehem baba yangu mkubwa. Nikaishi na wazazi wangu wote baba na mama, kaka yangu (JUMA SELA), dada yangu (Zainabu), na mdogo wangu Benadetha(R.I.P) katika kijiji cha Utegi, wilaya ya RORYA (kama mnavyoniita), mkoani Mara.

Familia ilikua ya hali ya kawaida sana. Ilipofika mwaka 2000, nilijiunga na shule ya msingi Utegi, iliyopo kwa kukadiria ni kama Km 4 kutoka home. Nikasoma na kuhitimu 2007. Nilianza kuonekana kama taa, baada ya kuwa nafaulu vizuri katika masomo yangu, na kupelekea kujulikana kwa waalimu na baadhi ya watu. Mwaka 2003, nikapewa uongozi (Kiranja) kwenye darasa la watu (188). Nikawakilisha vyema shule yangu katika uandishi wa Insha uliohusisha wilaya nzima ambao uliuletea shule yangu ya Utegi sifa nzuri. Walimu walianza kuniona mbali tangu hapo na kuniombea sanaa ndoto zangu zitimie.

Ilipofika December 10, mwaka 2004, baba yangu alifariki nikiwa darasa la tano. Akatuacha na mama na familia ya baba mkubwa (Olambo Oucho) kama baba yetu mlezi! Tulisikitika na kuhuzunika sana ila tuliyasahau na kumuona baba yetu mkubwa kama baba yetu mzazi. Mwaka 2006, nilihitimu shule pale pale utegi Primary school. Chakushangaza ni kwamba hata kufaulu sikufaulu, mbali na kujitahidi sana darasani (sijui nini kilitokea), ila mwaka huo (awamu ya kwanza) walifaulu wanafunzi 12! Nilikasirika sana, nikasema nitarudia shule na nitafaulu kwa alama za juu sana. January 8, 2007 nikarudi shule kurudia darasa la saba nijaribu bahati yangu tena. Haikuchukua muda sana March 01, 2007 matokeo ya awamu ya pili yakatoka nikawa nimo kati ya watahiniwa waliofaulu kwa alama za chini 159/250😢 na kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari PASTOR RAPHAEL ODUNGA, ilioko kijiji cha Buturi, umbali wa Km kama 18 kutoka nyumbani.

Sikua na namna nilitamani sana kusoma na wenzangu form One, nikamwambia mama yangu akatafuta njia kwa kushirikiana na baba mkubwa wakanihamishia NYANDUGA Secondary iliyoko kwenye Kata yetu. Jumatatu ya tarehe 07 March, nilianza shule nikiwa nimebeba jembe, ndoo ya maji, kwanja, rim paper (double A) na shilingi 26,000/= nikaanza masomo. Wiki iliyofuata Jumatatu ya tarehe 12/03/2007 tulianza mitihani ya mid-term test nikiwa na siku tano tuu shuleni, nilipata alama za kushangaza watu sanaa ndio ukawa mwanzo mzuri! Nilipenda sana Maths, Physics, Chemistry na Biology ndipo nikaona mimi naweza kuwa Engineer baadaye maana masomo hayo nayaweza vizuri.

Mbali na kwamba baba angu mkubwa alisomea uhandisi (Engineering) nlipomgusia kuhusu nia yangu mimi ya kusomaea fani hiyo pia alinitia moyo sana, na kuniambia nikazane kwani kuna chuo kipo Dar kinaitwa DAR TECH, wanachukua watu wanaopasua sana masomo kama hayo! Akanipa dondoo za raha ya chuo hicho; wanavyokula, chuo kipo katikati ya jiji la Dar, wanalipwa hela, hakuna kufanya usafi, 😂 basi nikaona huko ndo patanifaa, nikasema wacha nikomaeee na shule kwanzaa.

MAISHA YA NYANDUGA SEKONDARI:
Nilijitahidi sana kusoma na kukazania masomo ya sayansi nikijua nikimaliza naenda chuo cha Dar Tech. Baba mkubwa alituwekea hazina ya vitabu vya kujisomea, nikapambana hadi mwaka 2010 ilipo maliza form four hapo Nyanduga Secondary, matokeo yalitoka yakiwa mazuri kwangu, na kwa rafiki zangu wengine. Tuliofaulu na kuchaguliwa technical school tulikuwa watatu; David Kajode alipelekwa Arusha Tech, David Kimira alipelekwa Ubungo Maji na William Ernest Mjee Oucho.

Hutaamini, nilichaguliwa moja kwa moja kujiunga na CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA Dar es salaam (Dar Tech), kusomea Shahada ya Uhandisi mitambo kwa miaka mitatu.😂😂🤣🤣😂 ndoto ikawa imetimia kwa namna moja. Nilifurahi sanaa! Mama na kila mtu aliyejua walifurahia sanaa. Namshukuru hata Mbunge wangu wa jimbo (MH. LAMECK O. AIRO, Lakairo) aliniona kwa jicho lingine na kunitia moyo na kuniahidi kushikamana nami bega kwa bega mpaka nitakapofika.

SAFARI YA KUJA DAR:
Ilifika siku ya kutoka nyumbani kuanza safari ya kuja chuo, nikiwa mwenyewe kwa mara ya kwanza 🤣 nilipofika tuu Tarime Km 14 kutoka home nikaibiwa pesa zangu zote, na nikarudi home tena kutafuta pesa nyingine. Nikapata pesa nikaanza safari kwa mara nyingine na kuja mpaka Dar. Nilipofika Dar nilipokelewa na mama mkubwa (Mrs. Cecilia Igogo), kisha kunipeleka nyumbani kupumzika. Kesho yake asubuhi mama alinisindikiza chuoni kufanya usajili na baadaye kuhamia chuoni kwani nilikua natakiwa nikae chuoni. Mama mkubwa ni mama mwema sana, alikua akipita kunisalimia na kuniombea kwa Mungu, alinambia niamini katika ninachofanya nitafanikiwa. Nilitii na nikamuahidi sitamuangusha. Nilisoma na hatimaye 2014, nikahitimu.

William na mama yake mzazi wakati wa sherehe za kumaliza chuo, Dar Tech

Ikawa furaha nyingine kubwa kwangu, kwa mama yangu, baba yangu mkubwa na kila mtu aliyetamani kuniona nafika hapo.
Nilitamani kuunganisha kuendelea kusoma ila kuna somo moja lilinifanya nisiweze kuunganisha, kwani matokeo yetu yalicheleweshwa kupelekwa NACTE, ikanibidi nikae mtaani kwa miaka miwili. Katika kipindi hicho cha miaka miwili nilitumia kupata uzoefu wa kile nilichosomea, ambapo baba yangu mkubwa (Mr. Otieno O. Igogo) aliniona na kunipeleka kiwanda kimoja cha kutegeneza juice cha (U-fresh food), Tegeta. Nilifanya kazi pale kama fundi mchundo wa mashine hizo. Baadaye milango ya kazi ilifunguka na kujiunga na moja ya kampuni kubwa hapa nchini ya Kuzalisha Umeme na Kusambaza gesi (Songas Power Plant), iliyopo Ubungo. Nilifanya kazi pale huku nikiwa najitegemea sasa, naishi kwenye chumba changu cha kupanga.

Ilipofika mwaka 2016, nikasema lazima nijiunge kumalizia masomo yangu ya Shahada ya kwanza. Nilifanikiwa kufanya hivyo, nikapata chuo kile kile, fani ile ile, na nikaanza masomo rasmi ya kuitwa Engineer. Nilianza masomo yangu ya shahada ya kwanza mwaka 2016, na nikadumu kwa miaka mitatu, hadi kufikia june 10, 2019 nilipohitimu rasmi na kuweza kufaulu na kupata nlichokua nakitafuta kwa muda mreeefu! New Mechanical Engineer in Town.

Changamoto kila mtu anazo ndio maana hata sijaziongelea hapa, msije mkadhani nilikua nasona kwa raha raha, weee! 🤣😂😂😂 Ila natumia fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu wa Mbinguni, muumba wa Mbingu na nchi kwa upendo na uhai alionikirimia. Pia napenda kushukuru kila mmoja kwa nafasi yake alivyoshirikiana na mimi kuniwezesha mimi kuwa hapa. Wanadarasa wenzangu, kuanzia darasa la kwanza hadi chuo Kikuu, 🤣!

🍾 Mama yangu mzazi kapambana sana na mimi, kuhakikisha sikati tamaa, hata kama Inakuja gharika gani.

🍾Baba yangu mkubwa, Kwa kunionyesha njia na kutupatia elimu hakika, aliweza kutupa vitabu na sasa tunaona raha yake.

🍾familia ya Mr &Mrs Otieno Olung’a Igogo, mbarikiwe mpaka shetani aje awaulize mmewezaje wezaje🤣🙏🏼

🍾 Lameck O. Airo, Erasto Airo bro asanteni kwa kila kitu kwa kipindi chote nilivokuwapo skuli.🍾Mbogi yangu ya Rorya, Robhin Edson, Edina Ziporah, Kajode, Mary, Triza, Omara, Vicky, Triza Wuod nam, Emma Lucas, na wengineo wengi ambao sitamaliza kuwataja hapa tumeshikana vyema na tuendelee hivi hivi💐

Niwakaribishe katika mahafali ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza ya uhandisi Mitambo, tarehe 28/11/2019 katika viwanja vya chuo chetu, tufurahie kwa pamoja maana nikishinda nanyi mmeshinda…NB: wanaosoma au una mpango wa kusoma, tia bidii sanaa utafanikiwa tuu, Mungu ni mwema na ni wa kwetu sote.NAWAPENDA SANA WOTE. 🍁 THE END🍁

Golden BBQ point- nyote mnakaribishwa!

Tafadhali jumuika nasi kwenye ukurasa wetu wa Instagram na karibuni sana Golden BBQ point kwa BBQ zenye ladha na ubora wa kimataifa, vyakula vitamu vilivyo pikwa kwa umahiri mkubwa sana, mazingira mazuri na bora ya kula huku akili ikiwa imetulia, huduma nzuri sanaaaa, na gharama zake ni nzuri mno.
Private Barbeque service can be arranged. Tupigie tuje tukuchomee kwenye sherehe yako. Tupo Masaki, Bains Avenue, Off Mwaya Road, Msasani Peninsullar, Masaki, Dar es Salaam, Tanzania, nyote mnakaribishwa 🙏🏿

“Inawezekana mno ukiamua” ~~ Zamaradi Mketema

Reposted from @zamaradimketema – Unaweza ukawa na rafiki au jamaa unaemuamini sana au mlietengeneza Bond kubwa lakini ukaja gundua kuna mambo anafanya nyuma yako yasiyofaa dhidi yako/sio mtu mzuri ila UKASHINDWA KUJITOA KWAKE.

kwa kuogopa kumpoteza ukajikuta unajitafutisha hata sababu mwenyewe za kukataa ubaya wake alioufanya, na hata kugoma kuuona (kutafuta excuses/kuwa In Denial) kutokana na ile Bond iliyopo kati yenu.

Zamaradi Mketema, TV / Radio presenter

Na watu wa namna hii mara nyingi unakuta ni mtu ulieshare nae vingi, anakushauri ama ana siri zako nyingi sana hivyo inakutanda hofu ya kumpoteza bila kujali ule ubaya wake ambao unaweza kuwa na athari kubwa mbele.

Kwanza kabisa fahamu hakuna sababu yoyote kati ya hizo juu zinazotakiwa kukufanya ukeep mtu mbaya, kama hofu yako ni SIRI ULIZOMPA mwache ajue azimwage na kuzitangaza, hakuna jipya Chini ya jua, na ni bora kukata kuliko kumpa nafasi ya kujua mengine asiyostahili, na jiulize una uhakika gani kwamba hajamwambia hata mtu mmoja hivi hivi mkiwa mnaongea, hivyo usiendelee kuwa mtumwa wa mtu kwa kuogopa eti atatoa siri zako, mwache atoe tu, sidhani kama litakuwa jambo jipya Duniani.

Kuhusiana na swala la BOND YENU, Ukishaona mtu ni mbaya train yourself not to associate with them katika namna yoyote ile kwa kujifunza kusolve matatizo yako mwenyewe kidogo kidogo, itakuwa ngumu mwanzo lakini utaweza, itafika kipindi utaona kabisa humuhitaji tena, na usiendeshwe sana na hisia unapokumbwa na kitu, maana inaweza kutokea jambo na ukaona kabisa yeye ndio anaeliweza na huenda ni kweli lakini kumbuka ni kwakuwa tu uliamua kuamini hivyo, yes utamkumbuka lakini kumbuka tatizo ni la siku moja linapita, sasa kwanini tatizo la siku moja linalopita likufanye uendelee kumkeep mtu asiefaa milele, maana the more unavyoendelea kumshirikisha ndio the more utakavyoshindwa kujitoa kwake, usijiendekeze.

Na zaidi angalia MADHARA yanayoweza kutokea kutokana na ubaya alionao, kisha kubali kuwa huyo mtu hakufai, na hii inapaswa ianze na wewe, kumbuka HAUPOTEZI kama unaempoteza ana hasara zaidi kuliko faida, hivyo Kata, na jifunze kudeal na vitu mwenyewe, inawezekana mno UKIAMUA. – #regrann

Zari amekosea sana!

Kumpenda mtu siku zote utakuwa mkweli kwake hata kama yeye mwenyewe hapendi ukweli wako! As much as I Iove Zari, but I have to tell her this beater-truth! Kuwa Zari kwa hili umekosea sana!

Kwanza nianze kwa kusema simsapoti Diamond kwa udhalilishaji wake anao wafanyia wanawake kila siku! Hii ya Zari ni series ya matukio mengi ambayo amewafanyia wanawake ambao wamekuwa kwenye mahusiano naye.Amegeuza wanawake ndio mtaji wake wa kuongeza nguvu kwenye kazi zake! Which is very very wrong! However, despite all the evilness he has done, when comes to this issue ya kumdhalilisha Zari, personally I kinda understand where his pain is coming from! But again it doesn't justify what he did.

Kwanini nasema Zari amekosea? Ni kwasababu moja kuu ya kuamua kufanya udhilishaji kwa baba wa watoto wake bila kufikiria kuwa the real victims here are her own children! Tendo alilofanya Zari linamuweka level moja na Diamond, yani hakuna tofauti kati yao and two wrongs can't make it right! ..Kitendo cha Zari ku-move on na maisha yake ni kizuri sana! Tena sana! Nampongeza kwa hilo. Lakini kitendo cha yeye kuleta mwanaume mwingine kwenye nyumba ya mwanaume mwingine ni kukosa heshima sio tu kwa Diamond kama baba wa watoto wake bali pia kawakosea heshima watoto wake!
Zari, The Bosslady

Ule mji ulinunuliwa kama mji wa familia.That’s a place where her children as long as they live they will always remember and call it home! Home is small sanctuary, Zari has dishonored her children sanctuary! Hivi unajua ipo siku watakuwa wakubwa na sidhani kama watakuwa so impressed with their mom decisions! Haswa Tiffa, unajua jinsi watoto wakike walivyo na baba zao, Mungu atupe uzima kushuhudia yajayo!..Sijui kama Zari anajua anachofanya ni kosa au ndio maisha ya u-celebrity yamemuingia kwani hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo. Tunaona hata alipo achana na marehemu Ivan Ssemwanga alikua anamleta Diamond kwenye nyumba ya watoto zake! Na marehemu hakufurahishwa na hili! 🤔🤔 wanasema malipo ni hapa hapa duniani eeh! So Diamond got what he deserves!!.. Inajua mimi nashindwa kuelewa sijui ni Usabato wangu au ujaluo ndio unanifanya nishindwe kuelewa hii celebrity lifestyle!

Hivi wanawezaje kuleta mtu mpya kwenye nyumba au chumba ulichokuwa unatumia na your Ex-girlfriend / boyfriend? Nashindwa kuelewa haswa kwa wanawake! Majasho ulioweka kwenye makochi na mwanaume mwingine ndio hapo hapo unamleta mpenzi wako mpya 😳 Dah! Mie sielewi hii lifestyle! Labda ushamba umenizidi can’t think right 🤷‍♀️🤷‍♀️

Diamond ni mwanaume mshezi tu (sorry to say that) lakini hapa Zari kampa sababu na nguvu ya kumdhalilisha kwa kitendo cha kuleta mwanaume mwingine kwenye nyumba yao ambayo walinunua kwaajili ya familia. Ndio maana nimesema naelewa hasira za Diamond japo sifurahii alicho kifanya! Hii imekuwa ni desturi yake kudhilisha Exs wake toka wakina Penny, Wema n.k wote kawafanyia huu ushenzi! Ila amini usiamiani Tanasha anatmnyoosha Diamond wewe weka macho yako utayaona!

Mama Tiffah, the Bosslady

Kama kweli Zari anataka amani na kuishi maisha yake bila bugudhi yoyote basi Zari, you need to move to your own house, period! Let those men who desperately need you move to your house ili wakikuletea ujinga unamwomba aondoke kwenye mji wako. Lakini kitendo cha kuendelea kuishi kwenye mji wa wanao ambao baba yao kawanunulia haitakupa uhuru ambao unautaka! Just get your own place hata kama ni kubaya kama kwangu lakini ni kwako! Ni chakwako hakuna wakukwambia kitu! Please!

Halafu, I don’t know about you Zari maybe because you’re living that “celebrity lifestyle” but a man who dishonors his fellow man’s home like that?! Ain’t a man for me! Because it comes down to his morals and ethics! I hope he won’t turn around to be like the one you just dumped or even worse!..Hapa ndipo Tanasha kawazidi, unaona ametaka nyumba mpya kabisaaa ambayo hakuna Ex-girlfriend yoyote wa Diamond amewahi kulala wala kufika hapo! Msichana wa Kijaluo akili kwa kichwa 👏👏 Nani anataka kulalia vitanda au kukalia makochi yenye majasho ya mikosi ya mtu mwingine? 😂

Anyway, just prepare for the worst and hope for the best 🙏🏿 I saw somewhere you said you are about to say ‘I do’, my advice to you is take your heart with you but don’t forget your brain!! And prayer is key to every battle! Otherwise wishing you the best in everything you do! ❤

Dina Marious: Je, marafiki walio tuzunguka ni wa aina gani?

Reposted from @dinamarious – Leo nimeamka kichwa kiko mbio maana zimebaki siku 4 tu niwe nawe katika Maisha Class Seminar.

Lakini nimemkumbuka rafiki yangu mmoja wa toka udogoni.Hatuonani sanaa ila tunaongea sana kwenye simu.Nikakumbuka namna walivyokuwa wakiishi maisha mazuri sana.Wao ni miongoni mwa watu wa kwanza wazazi kuporomosha mijengo huku Mbezi beach.Miaka ya 90 wana hadi boat ya kucruz kwenda visiwa hivyo vya bongoyo sijui mbudya ambavyo sie ndio twaenda leo.

Dina Marious; Mtangazaji, Mfumbuzi na Mkurugenzi Mkuu wa Dina Marious Coconut Oil, Founder of Mwanamke wa Shoka and Kitchen Party Gala

Mama yao aliwazaa mapema sana na baba yao akafariki mapema pia.So walilelewa zaidi na mama.Mama alikuwa na pesaa alikuwa mrembo sanaa na alikuwa na marafiki wengiii mno.Na pia alikuwa mzuri wa sura na wa roho kujitolea kwa marafiki na ndugu sanaa.Wadogo zake kama watatu aliwawezesha kwenda kuishi nje.Yeye safari za nje ya nchi kama sijui kitu gani.Party za babakyu na marafiki safari na marafiki za kula bata nyumbani kwake palikuwa hawakauki watu.
Yule mama alikuja akaanza kuishiwa akaanza pia kuumwa aliugua kwa muda kidogo na kwa wakati huo rafiki yangu na mimi tupo kidato cha pili.Ndugu walikula kona,marafiki ndio usiseme.Alibaki yeye na watoto wake tu na hadi anafariki alimfia mwanae huyo shoga angu mikononi hivi akimhudumia maana ndio wa kwanza.

Dina Marious; Mtangazaji, Mfumbuzi na Mkurugenzi Mkuu wa Dina Marious Coconut Oil, Founder of Mwanamke wa Shoka and Kitchen Party Gala

Kuna mengi yalitokea sanaa lakini hili jambo huwa silisahau.Maana mie ndio nilikuwa shoga ake namna ndugu zake walikuwa wakimfanyia nilishuhudia kwa macho.Na huwa namkumbuka sana huyo mama na sasa nimekuwa mtu mzima ishu hiyo huzunguka sana kichwani kwangu.

Je marafiki waliotuzunguka ni wa aina gani?una marafiki kweli au una wapambe?Ni wangapi katika mafanikio tunakuwa na marafiki wengiii ambao kiukweli wapo hapo kwa manufaa yao?Wapo na wewe sababu una nafasi fulani,wadhifa fulani kupitia wewe mambo yao yatanyooka?Kwa sababu una mkono wa kutoa labda utatatua shida zao,utasikiliza hofu na nyakati ngumu wanazopitia. Utawalisha,utawanywesha,utawapa pesa,nguo,viatu inshort unarahisisha maisha yao.Ngoja pesa ikate ndio wa kwanza kukusema umefulia na kukukimbia.
Ngoja cheo/nafasi uliyonayo ipotee ndio utawajua walimwengu au wali nyama!Sitasema sana ila Mungu atujaalie watu sahihi katika maisha yetu.

MaishaClass #NenoLangu – #regrann

**Imeandikwa na Dina Marious**

Unapokutana na mtu mwenye mafanikio usimuombe pesa. Muulize amefanyaje kufikia hapo alipo!

“When you meet a person with means, a person that is well-off you think is successful  that you always wanted to be; don’t go there asking  for money” Hayo ni maneno yake Comedian na TV host Steve Harvey kwenye Oprah Master Class. Master Class ni show ambayo watu wengi waliofanikiwa katika nyanja mbali mbali za maisha wanaelezea mafanikio yao kwa undani zaidi toka walivyokuwa wadogo mpaka walipo fikia. Changamoto zipi walipata, vipi waliweza kuvumilia, kumudu hizo changamoto, na hata kufanikiwa bila ya kukata tamaa. Unapopata nafasi ya kukutana na mtu au watu ambao unawaangalia kama  “role mode / icon”  katika maisha yako usiwaombe pesa waombe wakuelimishe nini walifanya kufikia hapo walipo. Watu wengi wapo wepesi wa kuomba pesa kwa mtu aliyejaliwa kuwa nazo kwa ajili ya kujikimu na hiyo shida aliyonayo. Nautakuta muda mwingi shida hiyo haiishi ni kaituliza tu kwa muda. Hii yote nikwasababu wengi tunapungukiwa hekima ya kujua kuwa ni kheri mtu akupe elimu ya maisha ya nini alikifanya mpaka kufika hapo ili uone kama na wewe unaweza tumia njia hiyo kufikia malengo yako au kujikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Au utakuta wengine tumepingukiwa hekima ya kuona mafanikio ya watu ni maovu mbele zetu nakuanza kutafuta njia ya kumuangusha bila kujua kuwa anguko lake ni maafa kwako pia. …….Hivyo tuwe waelevu kama nyoka na wenye hekima kama Solomon ili tuweze kujifunza kutoka kwa wengine haswa ambao tunaona wana tija katika maisha yetu. Pale watu wanapokukatisha tamaa wewe piga moyo konde usiwasikilize. Kwanza mimi kwa experience yangu binasfi watu wengi wenyekukatisha watu tamaa ni watu ambao hawajiamini na pia hawapendi kuonekana kuwa wao wameshindwa katika kufikia kile wakitakacho hivyo hamna la zaidi zaidi ya kupiga makelele ili uwe muoga. Wakati ukweli wanatamani wangekuwa na ujasiri kama wako. Utaona wanakuja na maneno mengi ya kejeli ikishindikana wataingilia personal attack “hajaolewa”, “mnene”, “hana nywele”, “mbeba mabox” yani ukishaona mtu anaenda kwa personal attacks jua maumivu yamemuhelemea 😂😂 . . Nasiku hizi social media, basi watatafuta kila event au tukio lenye viongozi waende kupiga picha ili warushe kwa Facebook / Instagram basi tu ufikirie kuwa there really happy and making it, wakati rohoni wanatamani wawe na kipaji au nafasi kama yako. 🙈🙈 Wanasaikolojia wanasema mara nyingi watu wanao ongelea wengine vibaya muda wote huwa kuna mambo ambayo hayopo sawa kwa upande wao sasa kwasababu hawataki watu wajue huo upande wao hauwapendezi, basi dawa inakuwa ni kugeuza attention kwa wengine! Na huo ndio ukweli! Wewe usikate tamaa na mapicha yao! Nawala usiache mashauzi yao yasio na kichwa wala miguu yakuumize au yakutoe kwenye malengo yako. Mimi nilivyoanza hii blog yangu nimetungiwa uzushi wa kila namna; ooh huyo muhuni anatafuta mwanaume, huyo FBI, huyo kada wa CCM (utafikiri walishaniona na kadi ya CCM au nimevaa gwanda la CCM 😂😂), mara anatafuta umaaharufu, mara mkabila, mdini, yani maneno mengi mno wengine wakadiri hata kwenda kwetu kuchunguza maisha ya kwetu nakuja kuongea kwenye magroup yao. Mara kazi yake kudhalilisha watu. Eti huyo anagombania mali za wazazi wake 🙈🙈 Wengine wakazunguka kuwaambia watu wasiweke picha zao kwa hii blog. Yani hayo yote walifikiri nitaacha kublog!! Lakini nipo hapa and I’m here to stay! Mimi najua ninachofanya na ninako kwenda hivyo sijali. Waliokua wanasema mimi kazi yangu ni ku copy and paste ndio hao hao wanakosa raha kwani wanatamani niwaweke humu kwa blog yangu nami hata habari nao sina 🙆🙆  Ni maumuvi makali sana wanapata. Wewe songa tu, wakikwambia huwezi wambie wewe ni nani hata useme hivyo! Kitu kingine usiamini kila rafiki. Yani ukiona mtu ambaye ni rafiki yako anachukia maendeleo au mafanikio ya mwingine achana na huyo rafiki mara moja. Kwani inamaana wewe ni rafiki yake Kwasababu haujamzidi kimaendeleo lakini siku ukitaka kunyanyuka atakuwa wakwanza kukuangamiza! Niamini nimeyaona! Siku zote kuna mtu mmoja ambaye atakuelewa na ambaye atakuwa yupo teyari kukusaidia kufikia malengo yako. Mungu huwa hamtupi mja wake! Kama nipesa basi huyo mtu anaweza kusaidia, kama ni mawazo yanini ufanye ili ufanikiwe basi huyo mtu atakuwa yupo tayari kutoa ushauri. It means that person believes in you and truly cares about you! When it looks like nobody cares trust me someone is out there who really cares about you! Muda ukifika Mungu atamleta kwako. Usikate tamaa!

**Imeandikwa na Alpha Igogo** **#TBT #Sept.2017**

Mwanamke ni mtu shujaa, mwenye hekima nyingi, na muerevu sana!

Embu leo tuongelee hichi kiumbe ambacho Mungu alikiumba baada ya kuumba kila kitu! Mungu aliumba vyote lakini akaona kuna mapungufu mahala yani kwa lugha zingine naweza sema hakuridhika na kazi yake ya uumbaji mpaka alipo muumba mwanamke akaona vyote ni mema sana na uumbaji wake ukaishia hapo!

Labda niseme kwa siku ya leo nia yangu si kuongelea uumbaji wa Mungu bali nataka kuongelea moyo au nguvu ya ushujaa, hekima, na uwerevu ambao mwanamke amepewa na Mungu mwenyewe lakini bado tunajiona wadhaifu, hatuwezi kufanya kitu bila nguvu ya mwanaume kwanini? Kwakweli hata mimi sijui sababu bado najiuliza kwani kitu ambacho wanawake karibia wote tuna “struggle” nacho hata mimi mwenyewe- hello! Yes, me too 🖐 Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Hivi umeshajaribu kutafakari kuwa Mungu baada ya kumuumba mwanaume akaona kuwa hajakamilika kuna kitu kinahitajika ili huyu mwanaume aweze kufanya kazi kamili na kuishi kama mwanadamu? Na kitu hicho ni mwanamke! Hivyo, ukitaka kulinganisha utagundua kuwa mwanaume anahitaji nguvu ya mwanamke zaidi ili kuwa kitu kamili lakini mwanamke anaweza akafanya kazi na kuishi bila kumtegemea mwanaume sana (mnaojua maandiko ruksa kunikosoa). Naomba nieleweke, sijasema mwanamke hamuhitaji mwanaume la asha! Kila kitu ili kifanye kazi vizuri lazima kuwe na nguvu za hasi na chanya (mkono wa kulia na kushoto) ambazo zimeunganishwa pamoja katika kuleta nguvu kamili! Lakini saa nyingine utakuta upande wa kulia hautoi joto / nguvu sawa na kushoto hivyo inailazimu upande wa kushoto kutoa nguvu zaidi ili kuweka balance!

Zari The Bosslady

Nguvu ya ushawishi na hekima ambayo mwanamke amepewa ni kubwa sanaaaa! Tukiacha kisa cha Eva alivyo mshawishi mumewe Adamu kula tunda la mti waliokatazwa na Mungu, embu tuangalie kisa ya Malkia Esther kwenye Biblia! Jinsi Esther alivyotumia ushujaa na hekima ya hali ya juu kumshawishi Mfalme (mumewe) mpaka kuokoa watu wakwao! Kutokana na sababu mbali mbali watu wote waliogopa kumfata mfalme, lakini Esther alipoambiwa akasema lazima nifanye kitu kwani alijua kunyamaza kwakwe kungetoa tafsiri ya kuwa ameunga mkono maadui. Esther akajua wakati ni sasa kama ni kufa basi acha nife lakini lazima nikamuone Mfalme na kuweza kuongea naye juu ya jambo hili. Esther akatumia uerevu wake na hekima kupanga nini cha kusema, mahali pakusema, na muda wa kusema! Namwishoe akashinda na kuonekana shujaa kwa watu wa kwao!

Labda nifupishe hii story kwa kusema kwanini nimeandika, nia yangu nikutaka kuwakumbusha wanawake kuwa sisi ni viumbe vya kipekee sana ambavyo tumebarikiwa sana na Mungu lakini muda mwingi tumekuwa tukijikatisha tamaa sisi wenyewe aidha kwa kujua au kuto kujua! Tumekuwa waoga wa kutoa sauti zetu zisikike mbele ya wanaume. Tumekuwa hatutaki kueleza hisia zetu halisi na kujikuta tunaishi maisha yasio na uhalisia na kile kilichopo moyoni mwetu! Tumeshindwa kutumia nguvu ya ushujaa na ushawishi ambazo tumepewa na Mungu kuleta mabadiliko mbali mbali ndani ya maisha yetu na katika jamii zinazo tuzunguka! Tumekuwa viumbe dhaifu wakati Mungu alituumba kama mashujaa mkombozi wa mwanaume!

Japo kwasasa wanawake wengi wanaanza kuamka na kutambua hii siri ambayo ipo ndani yetu lakini bado inabidi tuamke zaidi! Mapinduzi yakweli yataletwa na mwanamke! Si unaona jinsi Eva alivyoweza mshawishi Adamu kula tuna na dunia yote sasa wanawake wanazaa kwa uchungu na wanaume wanaishi kwa jasho lao 😂😂 Basi kama mnataka mabadiliko ya kuachana na siasa mbovu, kutokomeza ukatili wa aina zote, mazingira bora na salama ya kuishi n.k lazima muamke usingizini!

Usijione wewe hufai eti kwasababu unatabia kama za “Wema Sepetu” (sorry Wema I picked you), hapana! Mungu anapenda watu wote na anaweza mtumia mtu yoyote yule kufanya mabadiliko kwaajili ya utukufu wa jina lake! Kwa wale Wakristo kumbuka kisa cha Rahab au Ruth kwenye Biblia! Wanadamu tunatizama vitu kwa macho yetu haya ya dhambi hivyo nirahisi kuhukumu watu na kuona kuwa hawafai na hawana thamani lakini siku zote kumbuka kila mtu anathamani sana mbele za Mungu! Na kama Mungu ataamua kukutumia hakuna atakaye weza kuzuia! Kikubwa ni wewe kusikiliza ile sauti ‘ndogo’ inayo nena nawe kwa upole ndani ya nafsi yako kuwa badili njia zako!

Wanawake tunaweza kuibadilisha hii dunia kuwa mahala salama pakuishi tena kama hatuta waachia wanaume peke yao! Wanatuhitaji ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli! Siku zote kumbuka kuwa wewe ni shujaa, mwenyewe hekima, na muerevu sana!

****Zari’s picture has nothing to do with the story**

**Imeandikwa na Alpha Igogo

“Unakichaa mimi nakuita mwendawazimu”!

Hicho kichwa cha ujumbe / somo la leo nimetoa kwenye ule wimbo wa ‘Yamoto Band’ lakini sipo hapa leo kuzungumzia huo wimbo wala band. Nimeyachukua tu kwasababu yameendana na ujumbe wangu!

Unasema humpendi mtu fulani (labda tuchukulie Zari, the Bosslady) lakini anafungua FEKI AKAUNTI ya social media kila siku haipiti hata masaa sita bila wewe kuangalia ame post nini?! Wewe unakichaa na ninakuita mwendawazimu!! Haiwezekani mtu mwenye akili zake timamu anayejitambua akaishi maisha ya kujidanganya na kujiumiza hisia zake mwenyewe!! Wewe lazima utakuwa punguani!! I’m sorry, but no thanks!

My twin sister and I

Hivi unajua ni ngumu kiasi gani kuishi maisha ambayo yanaumiza hisia zako? Kuishi maisha yanayo kupa hasira na chuki na watu wengine tena ambao hata huwajui undani wao zaidi ya kile unachokiona kwenye social media! Sasa tabu yote hiyo yanini? Ni kitu gani kinakufanya unaishi maisha yanayo kutesa? Kumfatilia mtu kwa kila kitu afanyacho hiyo ni zaidi ya ajira? Na kwenye ajira kuna mapato mtu anatakiwa kupata baada ya kazi ngumu, sasa wewe ni mapato gani unapata baada ya kumfatilia? Maana sio tu unapoteza muda wako, bali pia umetumia fedha yako kulipia internet, umeacha kufanya jambo lingine ambalo kwa namna moja ama nyingine lingekusaidia kuona mbele zaidi, yote hayo hukujali ukaamua kumfuatilia mtu usiye mpenda?! Halafu bado utatoka hapo unapoteza muda kumsengenya na wendawazimu wenzako 😳😳 Wonders shall never end!

Mimi binafsi sina muda wa kumfuatilia mtu ambaye ananikwaza, yani sikufungulii account fake hata mara moja nakupa block nasonga mbele! Embu nawe jaribu hii njia ninayo tumia mimi huwenda ikakusaidia. Hakuna haja ya kufungua account Feki kumfatilia mtu usiye mpenda! Maisha ni mafupi sana sasa usipotaka kuwa wewe katika hualisia wako ukaishi maisha yako sasa angali unapumua lini utaishi na watu wakakujua kua huyu ni fulani?!

Kamwe kataa kuishi chini ya kivuli cha mtu mwingine! Life is too short to blend in or to be someone else! Be real! Be you! We only live once!

Mtangazaji Maduhu aupa mkono wa kwaheri ‘ukapela’!

Beyonce sang it well “if he liked it he should have put a ring on it”! Basi ndivyo Mtangazaji maharufu toka Morning Star Radio ajulikanaye kwa jina la Maduhu alivyo fanya, he put ring and sealed it before God on Sunday April 7th, 2019.

Ndoa hii TAKATIFU ilifungwa katika kanisa la Wasabato la Nations Of Praise liliopo ndani ya jimbo la Houston, Texas inchini Marekani siku ya Jumapili majira ya saa kumi jioni saa za Marekani.
Mnaona neno “Takatifu” hapo juu ☝️ nimeweka kwa herufi kubwa na wino mwingi eh?! Nikuwakumbusha walevi na “mashakunaku” kuwa “alicho kiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe”!! Wale walevi wasiyo na haya huyu ni mke wa mtu muogopeni! Na wale mashakunaku wenye macho juu juu kama tunguli za mchawi nawakumbusha huyu ni mume wa Sule peke yake hachangii na mtu wala hamkodishi tafuteni wenu! 😍😍 kama nawaona mnavyo nisonya 🤣🤣🙈

Ndoa ilifungwa inchini Marekani kwasababu Bibi harusi yeye ni Mmarekani mwenye asili ya Kitanzania. Ambapo kule Tanzania anatokea maeneo ya Upareni.
Bwana na bibi harusi kwa furaha wenye nyuso za tabasamu baada ya kula kiapo kitakatifu!
Wapambe walikuwepo! Walipendeza sana.
Kwamara nyingine naomba niwapongeze sana Mr and Mrs Maduhu kwa kufunga ndoa takatifu! Wamesema wanaotaka ndoa za “mkeka” nyie fanyeni tu lakini sisi tunakwenda kula kiapo kitakatifu mbele za Mungu wetu aliye umba Mbingu na dunia! Mbarikiwe sana na nawatakieni furaha na amani isiyo na kikomo 🙏🏿

**Shukrani zangu za dhati ziwaendee wadau wote waliotuma hizi picha kwenye lile group la “Harusi tunayo”. Mbarikiwe sana 🙏🏿**

“Ukiomba mvua lazima ukubali kukutana na tope”-Isador Cakes

“Ukiomba mvua lazima ukubali kukutana na tope pia, hiyo ni sehemu ya mvua. Jana imepita hakuna ajuaye kesho, kitu pekee ulichonacho ni SASA ishi kutumia sasa kwasababu huna uhakika na kesho. Stay present.”

Vumilia Sassi: Mwalimu na Mjasilia mali
Pic by @pixelspro_films
Blazer @validcollection #machingawakiluo

Nimeupenda sana huo ujumbe toka kwa mjasilia mali na Mwalimu Vumilia Sassi. Ujumbe unamaneno mepesi sana lakini maana yake ni nzito! Wengi tunaomba Mungu atuletee mvua kwenye maisha yetu / mashamba yetu ili mbegu tulizopanda au tunazotaka kupanda ziote! Lakini wakati huo huo hatutaki kuona wala kujanyaga matope!

Hivi tutaombaje mvua halafu hatutaki kuona udongo umeloa? Sasa hizo mbegu zetu zitaingiaje chini ya aridhi na kuweka mizizi yake kwa chini kama udogo ni mgumu haulimiki! Ninachotaka kusema ni kwamba ukitamani na kulilia mafanikio yako binafsi basi lazima uwe teyari kukutana na changamoto mbali mbali. Jinsi utakavyo weza kudili na hizo changamoto ndio itakupa picha halisi ya mavuno yako (will determine your success). Kama hutaki kudili na matope basi usiombe mvua kwani hauko teyari kulima! Oprah Winfrey aliwahi kusema kuwa kama hauko teyati kuongelewa basi hauko teyari kwa maendeleo!

#Ukiomba Mvua Lazima Ukubali Kukutana na Tope

Wonder woman!

Wonder woman ni nani? Je, wewe ni wonder woman?! Wimbo huu ambao umetungwa na mwanamke mwenzetu Zamaradi Mketema na kuimbwa na kaka Chris Lunda ili kuwahamasisha wanawake wasikate tamaa pindi wanapo anguka.

Ni wimbo unaovutia nankusisimua mno! Binafsi nimeusikiliza kama mara kumi hivi, lakini kil nilipo usikiliza nikama ndio nausikia kwa mara ya kwanza na unagusa hisia zangu zaidi na zaidi.

Wimbo huu umenifanya nirudi hapa kuandika kama ilivyokuwa huko nyuma, wale waliokuwa nami toka mwanzo wanajua jinsi nilivyokuwa natoa maoni yangu mbali mbali isipokuwa SIASA! Nilikuwa nataka kujaribu kuchukua likizo ya mwaka mzima ili niweke nguvu zaidi kwa swala fulani. Lakini huu wimbo kwa njia fulani unenipa nguvu zaidi ya kufikiria upya na kusema mimi ni “Wonder woman” Simba niliye mbugani natafuta mawindo hivyo siwezi kutafuta mawindo sehemu moja nikaridhika!

Ninawasomaji wangu ambao wameni miss sana, hivyo kutokuandika kwangu kuna waumiza! Hivyo nimeamu kusikiliza sauti ya mwanamke mwenzangu, my fellow wonder woman! Narudi tena, kwa nguvu zote! Mimi ni wonder woman hakuna kukata tamaa 💪💪
Zamaradi Mketema, TV host, Song writer (Wonder woman), Philanthropist

Ngoja niseme kitu ambacho huwenda wengine wanakiona lakini hawajasema hadharani. Katika viwanda vya habari na burudani kwa muda mrefu sana vimetawaliwa na wanaume, nafikiri sasa ni wakati muafaka wa wanawake wa Tanzania kuendesha hii industry!

Katika wanaume wote hawa ambao wanashikilia hii industry marehemu Ruge Mutahaba ndio alikuwa anaakili ya kuogopesha wengi! He was the brainer of all! Huo ndio ukweli! Lakini nikiangalia kwa wanawake, naona pamoja na mapungufu yaliopo kuna wakina Ruge wengi tu kama tukiamua kushikana mikono na kusimama pamoja!

Kuna wanawake wengi sana nawaona wenye uwezo wa kufanya makubwa sana kama mtaacha hizi “pettiness” ambazo zinaleta mgawanyiko kati yenu! Ni wakati sasa waku-stop these “bullies” in media and entertainment industry! Sisi ni wonder woman hatushindwi!

The Millionaire’s Love Life: Happy Anniversary to them

🎶🎶🎤 (Dr Mengi) Mbona wanitazama, kisha waanza kulia?
Kama nimekukosea, naomba unisamehe

🎶🎶🎤 (Jackie) Hapana hujanikosea, mi nalia kwa furaha
Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata

Unaposogea karibu, unaponishika mkono
Unaponitazama machoni, nashindwa vumilia

Mapenzi unayonipa, sijawahi kupata najiuliza ni kwanini, hatukujuana mapema
Nimeishi na wasojua mapenzi, wasojua hata kunyenyekea

Nimeishi na wanaojua ku-force wasojua hata kubembeleza
Ninapokuwa na wewe, najiona ndio mwenyewe
Hata kama sina pesa, najiona tajiri
Hata kama sijala, najiona nimeshiba🎶🎶

***Happy Anniversary baba na mama wawili. Mbarikiwe sana***

“Kenyans in the diaspora and what they go through”

A better nuanced post by a better writer on Kenyans in the diaspora and what they go through.

By Odumbe Kute

Mercy’s picture has nothing to do with the article!

This is a myth that has been perpetuated for decades about life out in the Diaspora being more rosy than the suffering in Kenya. Whoever tries to convince you of that needs their head examined. Life is not a bed of roses out here. Forget the drama of Diaspora people who land in Kenya for holidays and flash the Queen’s shilling or Uncle Sam’s dollar. You have no idea what they went through to get that shit. I feel sorry for them personally, because what they have to come back to after splashing out in Kenya is a life of misery and debt.

See, there’s this assumption that if you’re in the Diaspora, you can pluck money from a tree and send it back home to do “development”. An assumption that Diaspora people are the best equipped to make sure that the hopelessness in Kenya is sorted out. There is an irony in that. For the last 11 years, Kenyans in the Diaspora have been remitting an average of Kshs 145 billion every year. And no, that’s not a typo. Diaspora remittances are the 2nd biggest revenue stream for the Kenyan economy.

The story that’s not told is what Kenyans in the Diaspora have to go through to deliver that shit. I can’t even begin to tell you the trauma this represents. There are people out here who are even scared of picking a phone call from home because they know it’s about demanding them to send money back home. A phone call is never about “How are you? How is life out there? Are you well? What about your family?”. The phone calls are about “Send us money now. If you don’t, we will die”. For school fees, for bills, for medical costs, for emergency, for saving someone’s life. The way it’s put, you’d think that if you don’t send money, someone is going to die immediately.

Alpha (blogger for alphaigogo.com) and her babysister Blessing

What people don’t know is that Kenyans out here have to hustle like a nonsense. Most do at least two or three jobs, or if they don’t, they’re working and trying to go to school at the same time. Money is not collected on trees as folk in Kenya believe. It’s hard sweat and graft, and even then, you’re just making ends meet if you’re lucky.

That doesn’t even take into account the stresses of life. Let me paint a picture for you, a picture that is common to most people in the Diaspora. You leave Kenya when your 18 or 19. Your objective is to go to school. You arrive out here and find out quick enough, that you have to hustle to pay school fees, you have to go to school at night because you have to work days and weekends, you have absolutely no time to yourself and the pressure eventually gets to you. If you make it out of that quagmire, you meet someone, you get hooked up, perhaps in a come we stay, perhaps in a marriage. You get a kid or two.

Now, out here, you can’t operate like you’ll get a house help from Kakamega or Kisii or something. Hell no, child care is so expensive, it defeats the object of working when you have a small child because you’ll be paying most of that salary for child care. Couples have to work around schedules to make sure children are taken care of. Many work shifts and don’t even see each other for weeks on end. The stresses this places on young families is unbelievable.

Consider that out here, we don’t have the same social network of close friends and family who would step in when things go thick. Under the circumstances, things most definitely go thick and we don’t have a way of coping with them. You have no one to turn to, no one to trust, no one who will give you guidance and counsel without judging the decisions you have made in life. Throw in the complexity of both of you as a couple having to hustle, the pressure both of you have to send money back home, the pressure both of you have to try and make a living and figure out what direction in life you both want to take.

But even within that, thousands have issues to do with immigration. Maratathi ni shida. A lot of people suffer in silence because they believe they can’t go to the police, or hospital or to the authorities because they don’t have papers. This despite the campaigning we did for years to eliminate immigration screening as a factor in DVP – Domestic Violence Protocol. The idea being that if you’re a domestic violence victim, you will never be asked about your immigration status. And I still can’t get this “African” thing used as an excuse by men. Someone once told me that in our community, if we don’t discipline our women, wata kuwa mang’aa.

Those who don’t have papers are very vulnerable. If there’s one thing I’ve learned, it’s never to judge someone’s situation or why they don’t have papers. It boils down to every individual trying to make a better life for themselves and their family, and no one has any right to take that away from them. But in particular, women are the most vulnerable if they don’t have papers. Many are stuck in abusive relationships because they have nowhere to go. You can’t get a job, open a bank account, rent a house, get a drivers licence or do anything meaningful if you don’t have papers. I know of women who have to trade sex to get someone with papers to act on their behalf to rent a house, or to get someone to let them use their bank details or to cover them for anything that requires papers.

Granted, there are people doing well out here. But that is the exception, not the rule. Hundreds more are suffering. Some will never tell you that. They’ll paint you a rosy picture of how “Majuu” ni poa sana. They’ll tell you that your salvation in life is to get out here in the Diaspora. What they won’t tell you is that out here, it’s ugly, sometimes even more so than Kenya. You barely can keep the lights on, and there’s so much pressure especially to send money back home.

It’s not even just about the pressure of sending money you don’t have back home. The trauma of making it day to day hits many people hard. In the last 15 years, I personally know 6 people who have committed suicide because they couldn’t hack it. Thousands more are suffering in silence and experiencing mental health issues that affect their ability to cope with life day to day.

Mercy and her mother- Alpha (Tanzanian Diaspora)

We really have to stop this myth that living out here aka “majuu” is the solution. We have nowhere to hide as Kenyans, we must confront and sort out our problems. In case you’re wondering what solution could ever get us out of the nightmare we have in Kenya right now, the answer is a revolution. But it’ll only happen when as a people, we get angry enough. Right now, we’re clearly not angry enough because we’re still tolerating the hegemony and corruption going on. We’re still very comfortable letting the bandit state, the politicians and the usual suspects oppress us. We’re happy to oblige, grabbing our ankles while they shaft us without the courtesy of lubrication as we sing to the tune of “Najivunia kuwa Mkenya”.

Magreth Nyasungu sendoff party

Magreth Nyasungu’s pre wedding photos moment

Magreth, bibi harusi mtarajiwa siku ya tarehe 27 December, 2018 alipiga picha za kumbu kumbu akiwa na ndugu zake pamoja na marafiki zake wa karibu.

Magreth akiwa na dada yake Mrs Nyagilo

Magreth (pichani juu) anatarajia kufunga ndoa takatifu hivi karibuni, tunamuombea Mwenyezi Mungu awatangulie katika safari yao.

Picha hizi zimepigwa na Rhevan studio, hivyo shukran zetu za dhati ziwafikie.

Kwa picha zaidi tembelea Rhevanstudio.com

Nawatakieni kheri ya kufunga mwaka 2018 na baraka za kufungua mwaka 2019!

Katika mwaka 2018 kuna mambo mengi sana yametokea, mengine yalikuwa mazuri sana, mengine ya kuhuzunisha na mengine japo yalikuwa ni changamoto za kutesa moyo na hisia lakini yamezidi kutuimarisha sisi kama familia. Shetani alitujaribu sana lakini ametukuta tupo ngangari imani yetu kwa Muumba wetu haitetereki. Kwajinsi tulivyo pitishwa kwenye hayo majaribu ambayo makali yake yalikuwa kama makaa ya moto nabado tukaishika imani yetu!? Basi nina kila sababu ya kusema kuwa kamwe imani yetu haitokaa kutetereka kwani tumeuona mkono wa Mungu hatuto uwacha milele! 

Kama nilivyo amua kuishi maisha yangu kwamba siku zote nita ipa nguvu mambo ambayo yananipa furaha na sio huzuni. Basi kwa mwaka huu wa 2018 vitu vingi sana vimenipa hufura lakini hivi ni vilinipa furaha zaidi. Kutembelewa na mama yangu mzazi, wadogo zangu, na mama yangu mdogo hapa kwetu Houston, Texas ni mbaraka wa peke sana. Nina kila sababu ya kusema Asante kweli wewe ni Mungu! Nitalisifu jina lako milele!
Jambo lingine ambalo limenifurahisha sana mwaka huu ni ujauzito wa my best friend, a sister near and deer to my heart. Mungu amembariki mtoto wa kike na amemuita jina Mercy sawa na jina la mwanangu mimi. Kwakweli namshukuru Mungu sana kwa huu mbaraka. Tunaomba amlinde na amkuze mwanentu. Atupe hekima na busara za kuweza kulea vyema watoto wetu 🙏🏾

The road to Nyasungu’s Nite

Kioo hakidanganyi mama umejipodoa umepodakaa 😍😍 mambo ni 🔥🔥
Mama mama mamaaa mama huyo 💃

Blog