“Acha Alama nzuri mioyoni mwa wale wanaostahili”***** Zamaradi Mketema

Reposted from @zamaradimketema Leo nilikutana na watu walikuwa wanajadili jambo japo katika hali ya masihara lakini nikagundua makosa makubwa ambayo huwa tunafanya sisi binaadamu

Zamaradi Mketema na binti yake Shubi Ruge Mutahaba

Watu wengi husema ukipendwa Ringa, mi nasema hapana, Ukipendwa THAMINI, na ikiwezekana mkomeshe kwa kumpenda zaidi, wenye mapenzi ya kweli ni wachache mno Duniani, Make Sure ukimpata kuwa KILEVI chake, mfanye awe ADDICTED na wewe, mzoeshe ama weka utaratibu ambao hata itokee mmekosana ashindwe kukaa siku moja mbili kakaza, sababu kuna kitu tu anakosa, kuna watu wanahisi pozi ndio Ujanja, Pozi ni ushamba!! Especially kwa mtu anaekupenda, kama wanavyosema Dawa ya Moto ni Moto kwenye mabaya basi hata mazuri ni hivyohivyo, mtu akikupenda mpende zaidi, haupotezi unawekeza, hata kesho akiwa mbali, kitakachomuumiza ni hiko, lakini kama wewe ni mtu wa headache kilasiku hakuna atachokumbuka

Beautiful Zamaradi Mketema

Na hii haiapply kwa mume/mke ama mpenzi peke yake, ila hata rafiki na watu wema tunaokutana nao, Acha Alama nzuri mioyoni mwa wale wanaostahili kiasi kesho na kesho kutwa hiyo ndio silaha yako pale mtakapokuwa mbalimbali, ukijiangalia una chochote ulichowekeza kwa wale wakupendao!!? Unahisi wewe ni kilevi chao ama headache!!? Kuna Alama umeshaweka ama ndio Upepo utakapopita umepita!? Tafakari halafu chukua hatua

Nimejisikia tu kuongea hiki, Muwe na Usiku Mwema!! – #regrann

Usiogope kuanza upya!

? Huo ni ujumbe wa Jacqueline Mengi siku ya leo!

Siku ya leo Jackie aliandika post mbili ya kwanza iliwakumbusha watu kua katika dunia hii ambayo unaweza ukawa kitu chochote kile basi chagua kua muungwana / mkarimu! “in a world you can be anything be kind”! Ni maneno machache lakini mazito sana! Sasa ujumbe wake wa pili ndio huo ? halo juu, ambo wenyewe unawasihi watu waaiogope kuanza upya kwani hiyo ni njia ya FURSA mpya kwao na kufanya kile kitu ambacho roho yako ilikua siku zote inatamani!

Nikweli kabisa, usiogope kuanza upya eti kwasababu ulishindwa mara ya kwanza au maamuzi ya mara ya kwanza hayakuzaa matokeo uliyo tarajia! Niliupenda ujumbe bila kuwa na swali lolote kichwani mpaka pale nilipo kutana na post ya Faraja Nyalandu Murugenzi wa ‘Shule Direct’ mke wa Mh. Lazaro Nyalandu. Yeye aliandika ujumbe huu ????

Mrs Faraja Kota Nyalandu

Reposted from @farajanyalandu May this new month remind you, you have all it takes to start and start again. That greatness awaits, that your little steps will lead you home. May you have eyes that see opportunities, a mind that seeks to build and hands that never destroy. May you overcome all that is holding you back. May you overcome you, if need be. May you find the peace to come back to the center of what truly matters. And find the Purpose that is above all. Happy New Month! – #regrann

Faraja ni kama alikua ametilia mkazo zaidi ujumbe wa Jacky! Naweza sema kama Jacky aliweka mbegu basi Faraja yeye akaweka mbolea na kumwagilia maji ili zao liote vizuri! Kwa kifupi Farajaja amesema tunapo anza huu mwezi mpya basi na uweze kukumbusha kuwa unacho kila kitu ambacho kinahitajika kuanza upya! Kwamba mambo makuu yanakungojea, hatua zako hizo ambazo ni ndogo ndogo zitakufikisha kwenye nchi ya ahadi! Basi na ukajaliwe macho yakuona FURSA mpya, fikra za kujenga na mikono ambayo kamwe haita bomoa! Na ukajaliwe ujasiri wa kushinda yale yote yanayo kukwamisha, na uishinde nafsi yako kama itahitajika kuishinda! Pia ukajaliwe amani ya kukuwezesha kutullia katika kile ambacho ni muhimu sana kwako na kuliko vyote!

Huo ujumbe wa Faraja Nyalandu ukaniwekea maswali kichwani mwangu! Je, Jacqueline Mengi anataka kuanza maisha upya?! Au hii ilitokea tu ujumbe zikagongana?! Wenye lugha zao wanasema “coincident”! Sina uhakika na maswali yote japo nimependa sana jumbe zote mbili kwani zina ujumbe mzuri sana wa kutia moyo!

Nachoweza kusema ni kua Jacky anaweza kufanya kitu chochote kile ambacho anatamani kufanya. Umri wake bado unamruhusu kufuta na kuanza upya! She’s too young kuvaa kofia ya “mjane”! Yes, mzee wetu kafariki lakini Jacky bado mbichi sana kukaa single! She needs a shoulder to lean on jamani! Anaweza omboleza mpaka pale atakapo jisikia yupo teyari kuanza familia mpya na mtu mwingine! Hilo halina ubaya kabisaaa! Ni baada ya muda gani; hiyo ni juu yake yeye kwani yeye ndio aliye vaa hivyo viatu anajua vinapo mbana! Ndio maana nikasema hawezi kukalia kiti cha mzee Mengi!

Jackie, wewe ukimpata Billionaire mwingine wewe tualike tu kwenye harusi sisi tutakuja bila shida ?? na picha zako mie nitapost ?? Au ukijipatia mzungu fulani wewe tupe tu mualiko tutakuja! You are very free, and don’t let people victimize you kuvaa kofia ya ujane sijui kwa miaka kumi?! Nope! This is your “prime time” use it correctly!

Kikubwa wewe unabiashara zako nyingi tu zisimamie my dear ili siku watoto wako waje kuwa proud na wewe. Those little Billionaires (the twins) wana haki zote kwenye kila kitu ambacho kina jina la marehemu baba yao! Huu ni mtihani kwa Regina na Abdiel tuone kama watawatunza wadogo zao au la! Hao watoto ni jukumu lao kuwatunza kwa kila kitu! Yes, wewe mama yao upo lakini kama wataamua kuvaa viatu vya baba yao basi hao watoto ni jukumu lao kwa asilimia 100%! Mpaka watakapofika miaka 18 basi wapewe haki zao zote! Wao ndio wataamua nini cha kufanya! Na wakumbuke kuwa hao watoto wamezaliwa baba yao akiwa Billionaire teyari, hivyo hayo maisha ndio walio zaliwa na kuyakuta na ndio maisha wanayo yajua, hivyo hiyo ndio level ya style ya maisha tunayotegemea kuona wakiishi! Sisi wapembeni tutakua tunatizama kama kweli wana kee-up the standard! Huu utakua muda muafaka wa public kuwajua vizuri Regina na Abdiel ni watu wa namna gani kwa kutizama jinsi watakavyo wajali wadogo zao!

Kwakumalizia nasema, ndio unaweza kuanza upya nasi washangiliaji tutakua hapa kukushangilia! Unakila kitu cha kuanzia na kila sababu ya kuanza upya! Huwezi kuwa mjane forever! You are too young for that!

“Wanaume wenzangu! To spare maneno tusiongee kila kitu. Kwa wake zetu” *** Harris Kapiga

Reposted from @harriskapiga Huu ni waraka kwa Wanaume! Walio kwenye ndoa! Wasio kwenye ndoa! Na walio na wachumba!

Familia ya Harris Kapiga katika picha

Si kila kitu cha kuonge na mkeo / mchumba wako, hasa mapungufu ya wazazi wako! Walezi wako, jamaa zako wakaribu ndugu zako, Boss wako! Kazini / kwenye biashara yako! Wanaume wengi huwa tunadhani tunanogesha penzi kumbe tunaharibu.

Unaanza mama yangu bana omba omba sana, una mwambia mkeo hapo au mchumba! Dada zangu bana waongeaji sana! Wana madeni kila kona. Boss wangu bana ananionea wivu anafanya fitina nifukuzwe kazi. Sisi bana, tumezaliwa kila mtu na baba yake! Mama aliachaga shule kakimbilia kwa bwana! Bi Mkubwa bana wanamsemaga mchawi! Kuongea kila Kitu hasa mapungufu ya wazazi na jamaa zako wakaribu unaharibu mahusiano kati ya mkeo na hao unaowasema vibaya kwake!

Lazima tukubaliane kila mtu anamapungufu , hata wewe unaeongea unayo yakwako! Baada ya kuongea nakudhani unanogesha Penzi! Kumbuka mwanamke kiukweli wale sio ndugu zake! Hana feelings nao kiviile kama wewe! Sababu ni wazazi wako, na umemjaza sumu mkeo / mchumba wako, anajiweka mbali sasa! Unageuka mwanaume unataka mke apeleke watoto kwa bibi yao! Akawasalimie na wewe ulimjaza masumu Bi Mkubwa mchawi! Bi Mkubwa ana mdomo; Bi Mkubwa ni mama yako unataka uonekane mwema, umpelekee wajukuu! Mke kagoma sababu ulimjaza masumu na mapungufu ya kwenu! Mgogoro unaanza, ooo mke jeuri, hapendi mama, haendi kwa mama! Kumbe wewe ndo ulikuwa mbaya ukamharibu (mazungumzo mabaya huharibu tabia njema)

Wanaume tumeumbwa na koromeo ina maana kuna vitu tuvihifadhi pale! Nieleweke hasa mapungufu ya jamaa zako, wazazi, boss wako na ndugu wakaribu!

1Petro 3;7…… Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa Akili. Kwa akili ni pamoja na kuchagua mambo yakuongea kuendeleza familia kwa Amani; Mwandishi ka endelea kusema Na kumpa mke Heshima; mtu unaemheshimu huezi mwambia kila kitu utachagua vya kuongea!

Wanaume wenzangu! To spare maneno tusiongee kila kitu. Kwa wake zetu! Vingine tunaharibu! Sasa pale umejiachia umemwambia mkeo sisi tumezaliwa kila mtu na baba yake!Halafu akakufuma na sms ya mapenz! Akakasirika ukasikia! Malaya kama mama yako! Aliewazaa kila mtu na baba yake! Usirushe ngumi! Uliongea kila kitu – #regrann

Ujumbe mzuri sana! Hii tabia ipo sana hata kwa wanawake! Unakuta mwanamke anaongelea vibaya sana ndugu zake tena watumbo moja akifikiri kwamba mwanaume atamuona yeye ni watofauti sana kumbe hajui anajichimbia kaburi lake mwenyewe! Mimi huwa naamini mtu ambaye anaongelea mtu katika njia ya kutaka kumfanya yule mwingine aonekane hana thamani au ni mtu wa ovyo mara nyingi hua kuna mapungufu mengi ndani yao hivyo wanajaribu kuondoa attention kutoka kwao kwa kuamini kwa njia hiyo watu hawato ona mapungufu yao na kutokujiamini kwao. (trying to diverge attention from their weaknesses / insecurities by pointing other people weaknesses and flaws). Hivyo hiyo ni njia yao ya kujihami! Ni guilty ya kutokujiamini ndio inawasumbua. Japo wengine ni mashetani na mapepo ndio yamewajaaa.

Mwenyekiti wa Dr. Ntuyabaliwe foundation asaidia kugawa vitabu mashuleni!

Mwenyekiti wa Mfuko wa Dr Ntuyabaliwe Mrs Jacqueline Mengi

Reposted from @j_n_mengi Yesterday I as the chairperson of @drntuyabaliwe_foundation had the pleasure of attending the launch of books for English Medium schools as well as Braille books for blind children organized by Tanzania Institute of Education. It’s a great step for the betterment of the education of our children and we @drntuyabaliwe_foundation congratulate Tanzania Institute for Education @taasisiyaelimu and our Government for this very significant achievement. – #regrann

Hongera sana Jacqueline kwa kufanya kazi za jamii! Sasa hapa ndio mahala pako pa.

kujinadi na kuonyesha “woman power”! This is your “THRONE” babe! Go girl and make your family proud! Kule kwa IPP na Bonite na mazaga zaga yao yote waachie wenyewe. Wewe kua sehemu yao lakini let them be the front runners! Kuwa sehemu yao kwani ni part of the Mengis’ but at the same time you are not the Mengis’ ?? (nafikiri unanipata my dear). Wewe uliolewa na mzee wetu Dr Mengi na una watoto ambao ni damu ya mzee Mengi lakini kutokana na mazingira ya mambo usijiweke mbele.

Kazi nzuri na hongera sana!

NIMECHOKA, SITAKUBALI KUENDELEA KUONA WANANGU WAKISONONEKA NA SITAKAA KIMYA.” *** JACQUELINE MENGI-2

Jacqueline mpendwa, naomba uwelewe kua hakuna anayepinga maamuzi yako ya kuolewa na marehemu mzee Mengi, nawala hakuna anaeweza kuleta ubishi kwenye hilo kwani ni maamuzi ambayo marehemu aliyaafiki na kuweka wazi akiwa katika utashi wa akili zake timamu! Hilo halina mjadala! Naamini hata watoto wa marehemu walikubaliana na hiyo hali, ndio maana kuna siku ulituwekea video mkiwa Hyatt Regency Kilimanjaro hotel mkila brunch wote kama family! Hata mimi nilikua shabiki mkubwa wa “the Billionaire family” ? Honestly, I miss those moments nikiwapost humu!

Late Dr Reginald Mengi

Sasa basi, tatizo ninalo liona hapa nikitendo cha wewe kutaka to sit on the “throne” representing the “face” of Mengi’s family tena kwa dharau na kiburi! Woman! You must have lost your mind!! Who made you the ‘Queen of the castle’ to begin with?! Kwakweli, hapo UMEKOSEA SANA TENA SANA!! Hivi unajua hakuna familia iliyo simama bila MAMA!! nafahamu ili mji wa mtu fulani usimame na kuhesabiwa lazima kuna mwanamke jembe fulani nyuma yake??! Wewe umekuta mji huo umesimama, kuna maziwa na nasali, dhahabu na lulu; hivi unafikiri viliokotwa tu bara barani?! Unafikiri vilipatikana kwa kupaka makeup masaa 24 na kuweka kucha bandia?! Kuna watu waliosota kwenye huo mji ili kuakikisha hiyo empire inasimama! Kuna watu walifunga na kuomba dua kwa Mungu ili huo mji usimame! Kuna walio lia kwa changamoto mbali mbali walizopitia! Hivyo wewe kushupaza shingo lako na kutaka kukaa kwenye ‘throne’ ni uwendawazimu uliopitiliza!!

Haiwezekani, narudia kusema tena haiwezekani kuongelea Legacy ya mzee Mengi bila kumtamka mke wake mkubwa mama Mercy Mengi! Kama kweli ulimpenda marehemu kwa dhati basi lazima uheshimu jina la huyu mama! Tunafahamu kwasasa hayupo, lakini ana wawakilishi wake ambao ni Regina na Abdiel! You have obligation to respect watoto wa mke mkubwa kwani sio tu wanamuwakilisha mama yao bali na baba yao pia. Hao watoto ni chimbuko na kiini cha Dr. Mengi’s legacy! Waheshimu!

Makaburi ya ukoo wa marehemu mzee Mengi

Jacqueline, haiwezekani kamwe ukaongelea legacy ya mzee Mengi bila kutaja ndugu zake watumbo moja! Haiwezekani! Hawa ndungu ni watu ambao marehemu aliwapenda, aliwajali, na kuwaheshimu mpaka mauti ilipo mfika! Sisi tulio bahatika kusoma kitabu chake tumeona jinsi gani marehemu alivyo ongelea mchango wa ndugu zake katika mafanikio yake toka akiwa shule ya msingi! Yeye hakuwatenga wala kuwadharau sasa inakuaje wewe unaenda kinyume?

Post ya Jacqueline leo

Mmh! Sasa wewe ulitegemea nini ulipo iwekea pingamizi familia?! Haya makaburi yapo ndani ya family property hivyo wanahaki ya kukufukuza! Hata mimi ningekufukuza! Jacqueline, ngoja nikwambie, at this point you have proven to be nothing but one of the 21st century classic “homewreckers”!! And as usual Homewreckers wanatumia watoto kama kigezo cha uhalifu wao! Hawana uchungu na kuvuruga familia za watu kwani they care less for the people who “paved” the way! Nia yao huwa ni moja tu; kuchuma na kuvuruga familia za watu!! Homewrecker huwa haonagi shida kuvunja legacy ya mtu kwani hawajui vilianzaje na hata wakijua hawajali ili mradi wamepata wanachotaka! Ndio maana ni rahisi sana kwako wewe Jacqueline kuongelea huu mtafaruku kwenye mitandao kuliko watoto wa marehemu!

Nilikua nakupenda nabado nakupenda ila kwa hili?! Gal! You are deadly wrong! Halafu, acha kabisa kutumia watoto kuichafua hii family! Hao watoto wanauwezo wa kwenda kwao na kuona hayo makaburi muda wowote ule, usitumie watoto kwa hila zako! Hizi “bongo movie” zako hazita kusaidia kabisa! Usifikiri watu hawaoni mambo unayofanya! People are paying attention and they are puzzled!!

Ushauri wangu kwako, tafuta upatanisho na watoto wa marehemu pamoja na ndugu zake wa damu! Hauwezi kukalia kiti cha mzee Mengi eti unawakilisha familia ya Mengi na ukoo wake wakati ulikuta kuna mji umesimama! Hiyo itakuwa dharau kubwa sana na kuwavunjia heshima si tu watoto wa marehemu bali ukoo wote! Learn to humble yourself!

The Mengis’

“Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.” *** Jacqueline Mengi

Naam! Hayo ni maneno yake mwenyewe Jacqueline Mengi aliyekua mke wa marehemu Billionaire Dr Reginald Mengi. Ujumbe huo aliandika kupitia account yake ya Tweeter na pia ku-share kwenye Insta-story yake! Kuna wengi wamemsapoti na kuhuzunika naye kitu ambacho kinaonekana kimemfariji Jacqueline hata kuandika tena ujumbe mwingine wa kushukuru leo hii kwa kutumia Insta-story yake (soma ????),

Ujumbe wa Jacqueline leo hii kwa Insta-story yake

leo hakupeleka Tweeter ?? najiuliza kwanini huu ujumbe wa shukrani haupo Tweeter leo? ?? nafikiri jibu lako halitakua na tofauti sana na lakwangu! ??

Jacqueline mpendwa, unajua kuishi na Wamarekani kumenifundisha mambo mengi sana na moja ya vitu ambacho nimejifunza na nimeamua kukitumia katika maisha yangu ya kila siku ni kua ‘kama kweli unampenda mtu kwa dhati basi lazima utamwambia ukweli mchungu’! Umwambii mtu ukweli ili kumnyanyapaa la asha! Ni ili umfungue macho na akili aone vitu kwa mapana na katika uhalisia! Wenye lugha zao wanasema “help them to see outside the box”!

Sasa mpendwa Jacqueline, mama wawili, Ooh! How I miss calling you muke ya Billionaire ?? naomba nikwambie ukweli but you have to understand it comes from a very place of nothing but PURE LOVE! Najua naweza nikawa nalugha isiyo kupendeza, unisamehe tu kwani somehow I’m taking it very personal kwa kuvaa viatu vya watoto wa marehemu Dr. Mengi na ndugu zake! Na pia hii mikasa inatokea kwenye familia nyingi za Kiafrika hivyo kwa upande mmoja au mwingine inanigusa!

Unasema umenyamaza kimya kwa mengi sana?! Ni mengi yapi hayo? Maana huku social media sisi ambao tunakufatilia hatujawahi kuona ukilalamika kuhusu jambo lolote juu ya watoto wa marehemu wala ndugu zake, hivyo kuandika ujumbe kama huu bila kuelezea japo kwa kifupi tu ili watu wajue kama wanakusapoti wanakusapoti kwa misingi hipi?! Unasema umechoka, hutokubali na hutokaa kimya?! ?? mmh! Hivi watoto wa marehemu mzee Mengi nao wakisema hayo maneno na wakaamua kuvunja ukimya wao hivi itakuaje??! Hivi utaweka sura yako wapi?!

Marehemu Dr Mengi akiwa na watoto wake Regina na Abdiel wakati wa msiba wa mke wake marehemu Mercy Mengi!

Labda nikuulize, hivi unajua watoto wa marehemu wamenyamaza kimya kwa muda gani sasa?! Toka wazazi wao walipo farakana nakutenga mpaka mauti ilipo watenganisha kama ahadi ya kiapo walichokula mbele za Mungu, na hatimaye sasa ni yatima, hao watoto umesha sikia wanaongea wapi kwenye hizi media?! Unafikiri wanamangapi mioyoni mwao ambayo yanawaumiza kimwili, kiroho, kiakili hata kisaikolojia lakini wamenyamaza nayo wanalia nayo huko ndani ya nyumba zao wakati taa zikiwa zimezimwa, madirisha yamefungwa, na pazia likiwa limeshushwa?! Na hayo yote wanavumilia kwasababu wanalinda heshima ya familia yao pamoja na Legacy ya baba yao ambayo wao wenyewe walimsaidia baba yao kuijenga!!

Marehemu Dr Mengi namke wake wa kwanza marehemu Mercy Mengi

Hivi, unajua Regina na Abdiel wanamaumivu kiasi gani ndani ya mioyo yao, kutoka kuzaliwa na kukua katika familia walioaminishwa kua inafuraha na amani mpaka wazazi kutengana, mara baba kuishi “single life” na hatimaye kuoa msichana ambaye ana umri sawa na “Mjukuu” wake?! Unataka kweli nao waseme wamechoka na ni muda sasa wa wao kuvunja ukimya?!! Jacqueline take that chip off your shoulder and learn to humble yourself!! Hao watoto wamenyamaza na mengi sana ndani ya mioyo yao, wanamaumivu makali sana only people with EXTRAORDINARY kind heart will understand maumivu yao! So, don’t play a victim card because it doesn’t give you any justice!!

***Itaendelea***

MAMA SALMA KIKWETE UMEKOSEA SANA! HIYO INAITWA INSTITUTIONALIZED DISCRIMINATION!-2

Hon. Jakaya Mrisho Kikwete and his daughters!

Mama yangu, ninacho jaribu kukwambia ni kwamba fungua macho yako utazame hii hoja yenu kwa macho mapana utaona jinsi gani imejaa ubaguzi na unyanyapaaji wa hali ya juu kwa mabinti wanao pata mimba wakiwa shuleni! Kama mmeamua kufukuza shule wanafunzi basi mfukuze wote wanaofanya ngono wakike na wakiume kwa ujumla wao na siyo kubagua wanaopata mimba tu! Hivi mama Salma, kweli unataka kusimama hapa na kuiambia dunia, mbele za Mungu kuwa huyu binti yako mwenye gauni jeusi bado ni bikira?! Au kwasababu hajapata mimba kwahiyo unamuona mtakatifu?!!

Kumbuka kabla ya kutunyooshea kidole sisi hakikisha kucha zako ni safi! Maana lazima tutazikagua!! Hizi sheria mnazoziweka bila kutafakari madhara yake katika jamii ipo siku damu zenu zitazilipa tu! Yawezekana leo hii haitamkuta binti yako lakini huenda kesho yakamkuta mjukuu wako! Oh! Nimekumbuka nyie ni “high profile” people, you do “high profile crimes” bila sisi walalahoi kujua, mama kumbuka Mungu anawaona!!Kumnyima mtoto yoyote haki ya ku-access education ni kinyume na haki za binadamu. Kwani kupata elimu ni haki ya msingi ya binadamu wote! Wanafunzi wanaopata mimba wanatakiwa waachwe waendelee na masomo yao kama kawaida bila kubaguliwa na mtu yoyote yule. Kama hiyo ni ngumu basi wapewe “sick leave” wakisha jifungua waendelee na masomo yao.  Au kama hizo mimba zinawakera sana basi wafungulieni Abortion clinics ili wawe wanakwenda kuzi-abort huko, labda roho zenu zitafurahia!!

Kumbuka kuwa unapomnyima mama moja  haki ya kuelimika inamaana unatengeneza jamii / community ya watu wasio na muelekeo wa maisha na kuendeleza mila ambazo hazina tija kwa taifa! Mama ndio nguzo za familia nyingi haswa Africa. Hakuna njia mbadala katika hili swala zaidi ya kuwaacha waendelee na masomo yao bila ubaguzi wowote ule kwa faida zao binafsi, vizazi vyao, na taifa kwa ujumla!Ngoja nimalizie kwa kusema kuwa, tatizo wazazi wengi wa Africa wanataka waonekane kuwa wao ni malaika hawajawahi fanya mistakes yoyote ile maishani mwao! Ndio maana wako guilty na busy kuwahukumu watoto kwa kuwapa adhabu za ajabu ajabu badala ya kuwaelekeza juu ya maisha. Unajua yale mambo ya kila mzazi anajifanya alipata ‘A’ darasani, alikuwa wakwanza siku zote, na kila mwanamke aliolewa akiwa bikira! Just a bunch of nonsense (Excuse my language)!. Uongo mwingi kwa watoto zenu bila sababu yoyote ya msingi!  Btw, hii ni karne ya 21, mama yangu where have you been?! Unaona statistics za dunia zinavyo kwambia yani karne hii wazazi nmnatakiwa kuongea na watoto / wajukuu zenu juu ya sex / elimu ya kujamiiana kabla ya miaka 10! Kwani watoto wa miaka 10 siku hizi wako sexually active na wengine wanabeba mimba! How? I don’t know usiniulize mimi lakini hiyo ndio hali halisi ya sasa, just get with the program mama!!

***FBF*** Hii story yangu niliandika May 17th, 2017 wakati Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza mjadala juu ya hitimisho la elimu kwa watoto wakike wanao pata ujauzito wakiwa shuleni!****

MAMA SALMA KIKWETE UMEKOSEA SANA! HIYO INAITWA INSTITUTIONALIZED DISCRIMINATION!

Hivi ule usemi wako wa “mtoto wa mwenzio ni wako” uliufuta baada ya kuvua kofia ya u-FirstLady!! Bado najaribu kukutafakari nia yako haswa ni nini?! Wahenga walisema “uchungu wa mwana aujuae ni mzazi” lakini mimi saa nyingine napingana na huu usemi kwani kuna watu hawajawahi onja machungu ya uzazi wala malezi lakini wanaumizwa na kuguswa na watoto wa wengine kuliko baadhi ya wanawake walio zaa! Hapa simuongelei  mwingine bali ni aliyekuwa mkuu wangu ya shule ya Kowak Girls Secondary school Sister Magdalena (R.I.P). 

Miaka 23 iliyopita, nilipopata ujauzito nilikuwa form 2 pale Kowak Girls Secondary school Wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara. Shule ilikuwa inaongozwa na wamishonari wa Catholic na huyu Sister Magdalena ndio alikuwa Headmistress (yeye alikuwa Mmarekani) na msaidizi wake alikuwa Sister Nyambosa  ambaye alikuwa Mtanzania. Sasa Sister Nyambosa kulingana na the so called “mila na desturi, sheria za Tanzania na dini” alitaka nifukuzwe shule!! Eti hiyo ndio adhabu yangu nikajifunze! But guess what?!! Sister Magdalena akasema NO! Hato hidhinisha hiyo barua ya mimi kufukuzwa shule kwani haoni logic ya hizo mila na desturi, pamoja na sheria za Tanzania. Yeye aliamini kuwa kitendo cha mimi kuwa mama kwa umri ule ni adhabu tosha! Pia nilikuwa mmoja ya wanafunzi wazuri pale shuleni hivyo hakuona kwanini aniharibie future yangu kwa kunifukuza shule ambayo technically angekuwa anaharibu future ya watoto wawili (mimi na kiumbe kilichokuwa tumboni mwanangu wakati ule).

Kufupisha story hii, wakafikia makubaliano yakunipa sick leave mpaka nitakapokua tayari kurudi shule basi wao walikuwa tayari kunipokea au kunipa uwamisho kwenda shule nyingine! Miezi sita baada ya kujifungua nilitafuta shule nikahamia, uhamisho wangu ulitumwa bila tatizo!! Shule niliyo hamia ilikuwa ni Nurulyakini Secondary school pale Mwembe Yanga, Temeke. Nilirudia form 2 kwani nilikuwa sijafanya mtihani wa form 2 nilipokuwa nimetoka Kowak. Wanaonijua vizuri wanaweza kushuhudia kuwa hata siku moja sijawahi kuwa ashamed kusema kuwa mimi nina mtoto. Kwani miezi mchache tu hapo shuleni nilianza kuwaambia wanafunzi wenzangu na hatimaye story zikafika hadi kwa walimu wote wa shule! Guess what?! Hakuna aliye jali wala kunifanya nijisikie vibaya kuwa mimi ni mama katika umri ule!! Walichojali ni academic records zangu! Tulipoingia form 3, nikachaguliwa kuwa Assistance HeadGirl, na nipofika form 4 wakanichagua kuwa HeadGirl na hiyo yote ni kwasababu ya jinsi nilivyo kuwa hapo shuleni walimu walipenda sana na kuniona as a blessing to their school.

Nakumbuka siku moja dada aliyekuwa ananiangalizia mtoto alikuwa anaumwa hivyo hakuweza kukaa na mtoto siku hiyo. Ilikuwa ni wiki ambayo tunafanya final exams review kwa ajili ya kuanza final exams za form 4!! Nilikuwa na 2 choices; ama nisiende shule nibaki nyumbani nimuangalie mwanangu au nimbebe mwanangu niende naye shule! Sikiliza mama, jinsi walimu wangu na wanafunzi wenzangu walivyo nifanya nijisikie wakawaida kama wao, yani wala sikufikiria mara mbili!! Nikamuogesha mwanangu nikajiandaa nikaendanae shuleni. Nipo darasani nasoma na mwanangu yupo pembeni yangu! Hakuna aliyeniona waajabu wala nini!  kila mtu alikuwa anamfurahiya mwanangu!! And for the records nilifaulu vizuri sana form 4!

Hon. Salma Kikwete

Mama yangu sikiliza, tatizo lolote lile hata liwe kubwa kiasi gani ilikutafutiwa suluhisho la kudumu inategemea na attitude ya jamii husika na viongozi wake! Embu tafakari kama Sister Magdalena asingeweka msisitizo kuwa hato hidhinisha hiyo barua ya kunifukuza shule mimi ningekuwa wapi leo?!! Vipi kama walimu na wanafunzi wa Nurulyakini wangenibagua na kunitenga je mimi ningeweza endelea na masomo yangu?! Je, maisha yangu na ya mwanangu yangekuaje kama nisingepatiwa nafasi ya pili ya kufanya matengenezo?! Maana hivyo vyeti vyangu I mean my academic records ndio vilivyonileta hapa nilipo leo hii!! Labda nikwambie tu kuwa Nurulyakini ni shule ya Waislamu!

Hii tabia ya kutokutoa nafasi ya pili kwa “wakosaji” ndio inaleta matitizo mengi ndani ya Tanzania kama mambo ya vyeti feki, na forgeries nyingine! Viongozi wenye mtazamo kama wako ndio wanao changia matatizo kama hayo niliyo yataja katika jamii yetu!

By no means, siungi mkono maswala ya wanafunzi wa kike kupata mimba wakiwa mashuleni. Hata mwanangu analijua hilo kwani niliongenae mapema mno nilipo ona anaakili za kutosha kuelewa kile nitakacho mueleza. Lakini naomba uwelewe kuwa tatizo si kupata mimba, tatizo ni familia, jamii, na serikali imeshindwa kuelewa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuelimisha familia pamoja na jamii nzima kuhusu swala la kujamiiana na changamoto zake haswa kwa watoto wakike! Leo hii unasema waliopata mimba wasiruhusiwe kuendelea na shule, ok! Fine! Vipi wanao adhirika na magonjwa Kama HIV, gonorrhea, genital herpes, syphilis, n.k  hao mnawafanyaje?! Kwani hayo pia siyanatokana na ngono??! Hauoni kama kuna haja ya kuwataka madaktari wawataharifu shule mara tu wampatapo mwanafunzi anaugonjwa wowote wa zinaa ili nao wafukuzwe shule?? Mbona mnawaonea wanaopata mimba peke yao?! Ooh! Au mnaonaje muanzishe sheria ya watoto wakike kukagualiwa kama wako sexually active au bado kabla ya kuingia shule katika kila muhula?! Labda hiyo ingetoa fursa sawa kwa mabinti wote! Na wanaume je mgewafanyaje?!!! Acha ubaguzi na unyanyapaaji mama yangu?!

***ITAENDELEA……… ***

***FBF*** Hii story yangu niliandika May 17th, 2017 wakati Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza mjadala juu ya hitimisho la elimu kwa watoto wakike wanao pata ujauzito wakiwa shuleni!****

Simulizi za maisha ya mzee Igogo kwa maneno yake mwenyewe!

MATUKIO YA LEO 19.02.2020 KWA MFADHILI:- 1. Bi Mole Akungo, mjane wa marehemu Akungo fundi magari, aliyekuwa Mwajiri wa Mkurugenzi John Orwanda. Anaumwa kisukari na kasikia tuna dawa ya Jufeel, pamoja na kukosa uwezo wa kujikimu.

2. Dada yangu wa kihindi Bi. Dirishan mlemavu wa Kibiongo aliniita kumtembelea kwake, ndiye aliyekuwa mwenye ofisi ya mtaa wa mshihiri na eneo la kurasini, nilipoanzia kampuni ya Utegi. Walinisaidia mno nilipokuwa naanza kampuni.

3. Rafiki yangu Bi. Zainabu Mbuguni, mlemavu wa macho (KIPOFU KABISAA), Aliniletea zawadi ya kazi ya mkono wake, kikapu cha ukiri, aliyoitengeneza mwenyewe kuanzia kusuka ukiri na kushona kapu hilo, ili nimpelekee mama Igogo kwendea sokoni, pia kaniletea zawadi ya miwa anazolima shambani kwake huko Kibamba.

Pichani yupo na Mwanasheria Asha Nassoro Mwanasheria wangu, na Maria Patrick Kagose, Mfadhili wangu nilitumia tiketi yake ya Bus na treni akiwa mdogo, kuijia jijini Dar, kwa upendo wa Mama yake, Dada Theresia Olung’a Igogo, aka Mama Maria.

***Imeandikwa na Sir O.O Igogo na kuleta hapa na Alpha Igogo (Blogger)***

Simulizi za maisha ya mzee O.O Igogo kwa maneno yake mwenyewe!

Za asubuhi marafiki wapendwa. Natumai soote tumeamka salama na hao wadogo wasiyoweza kuwasiliana kwenye group. Jana ilikuwa siku yangu ya kumbukizi ya mambo ya ujanani, kama alivyosema Mama ni kweli niliwahi kushiriki kanywaji kati ya mwaka 1972 hadi 1979. Nilishuhudia matukio mengi ya kuchekesha na kuhuzunisha ndani ya kipindi hicho. Nakubaliana fika na Rais Mstaafu wa Nchi ya Merekani OBAMA, alichokiandika kwenye kitabu chake kilichompa Umaarufu kiitwacho THE DREAM FROM MY FATHER. Aliota njozi toka Baba yake, na wala siyo ndoto!!!Nami mwaka wa 1979, nikiwa kazini wilaya ya Geita enzi hizo, kwenye machimbo ya dhahabu Nyarugusu, nikiwa Msimamizi wa Ujenzi wa mitambo hapo mgodini na Shirika la NECO Ltd. Nilienda kijiji cha jirani kumtembelea Mama yangu mdogo, aitwaye Leokadia Ombwa Olwengo, mdogo wake Rhoda Nyolwengo. Yeye na Vijana wake walikuwa wachimbaji wadogo wadogo. Nilikuwa na gari la Shirika na ikawa shangwe ya hali ya juu nilipofika hapo kwake. Kuku wawili walipoteza uhai ghafla kuwa kitoweo rasmi. Mama alikuwa mtengenezaji maarufu wa pombe ya kienyeji iitwayo APELO, yaani CHANG’AA?? Ile furaha ya kukutana na ndugu zangu, nao kuniona nimekuwa Bosi naendeshwa na gari la Shirika, ikazua unywaji wa kilevi Apelo bila kipimo. Nilivyorudi kambini na kuingia chumbani sikujuwa. Ila usiku huo wa tarehe 7/6/1979, nilijiwa njozini na Marehemu Baba yangu Mzee William Olung’a Igogo. Aliniita kwa sauti ya juu sana nami nikamuitikia, nilikuwa napepesuka kwa ulevi, manano aliyoniambia ni:- MBONA UNAHARIBIKA KWA POMBE?? ACHA ULEVI, UNAPOTEA!! ACHA KABISA?

Asubuhi yake nilipoamka, nilikuwa hovyo, hovyo kweli, kweli!!! Nilijikuta nimelala kwenye matapishi yangu yanayonuka kama taka teke teke ya chooni. Mchovu kupindukia, kichwa kinawanga na kugonga kama nyundo!! Ilinilazimu kujifanyia usafi huku nikiitafakari hayo maneno ya njozini, niliyohaswa na Marehemu Baba!! Sikuweza kwenda kazini siku hiyo, ilipofika mchana nilipata mlo kwenye kantini ya hapo Camp, na hatimaye nikaamwambia dereva anipeleke Geita mjini, nilikwenda moja kwa moja kwenye duka la Vitabu, na kununua kijitabu kidogo cha Agano Jipya. Nikaanza kuisoma msitari kwa msitari, kurasa hadi kurasa ifuatayo hadi mwisho, na nikairudia mara kadhaa.Ni kweli tangia siku hiyo hadi leo hii, zaidi ya miaka arobaini sijaweka kinywaji cha aina yoyote kinywani mwangu. Naamini bila mashaka ya aina yeyote kwamba Maandiko matakatifu isemavyo kwamba Baba na Mama yako ndiyo Mungu wako wa Duniani, ni kweli haswaa.

Mzee Igogo na mjukuu wake Cecilia Chaulo

***imeandikwa na mzee O.O Igogo (muhusika) na kunukuliwa hapa na Alpha O.O Igogo (blogger)***

“Life can be a rollercoaster and you will never know where you’ll end UP.” >>> Zari the Bosslady

Life can be a rollercoaster and you will never know where you’ll end up

From studying my Cosmetology course in the UK ( which hasn’t helped me) while doing house girl work to pay my accommodation (yes I’ve been a maid before) to running through buses to get to my next stop woodgreen where I worked as a Cashier and sometimes as an Isle packer in Sainsbury. Friend, I started out early wasn’t even sure why me. But the inner voice in me wanted better.

My dad had left, my mom was doing tailor jobs day and night I couldnt stand seeing her struggle I couldn’t stand her pain. I was living with my aunt in the UK who treated me like a step child. Gooosh?
Been through boutiques, long economy flights to china in between building a school and having babies. My music and tv career is a story for another day. Phew? All I’m saying, consistency is key. Doesnt matter where you are or what you do. Just do it.

I am the author of my life, my story, don’t rewrite it for me.! Let me be the one to tell it.
Throwbacks are good, reminds us of where we’ve come from and I think that kinda keeps you grounded.

William Ernest Mjee Oucho: Ndoto yangu ya kua Engineer

William Ernest Mjee Oucho
Napenda nishee na nyie story ya safari yangu ya kutafuta kuwa muhandisi tangu nimekua na mpaka sasa nilipofika. Twende sambamba utajifunza kitu hapa.

Mwaka 1993, Jumatano moja ya tarehe 09 mwezi wa Sita, mama angu alinizaa na kunileta duniani, na kunibarikia jina la William, ambaye alikua ni marehem baba yangu mkubwa. Nikaishi na wazazi wangu wote baba na mama, kaka yangu (JUMA SELA), dada yangu (Zainabu), na mdogo wangu Benadetha(R.I.P) katika kijiji cha Utegi, wilaya ya RORYA (kama mnavyoniita), mkoani Mara.

Familia ilikua ya hali ya kawaida sana. Ilipofika mwaka 2000, nilijiunga na shule ya msingi Utegi, iliyopo kwa kukadiria ni kama Km 4 kutoka home. Nikasoma na kuhitimu 2007. Nilianza kuonekana kama taa, baada ya kuwa nafaulu vizuri katika masomo yangu, na kupelekea kujulikana kwa waalimu na baadhi ya watu. Mwaka 2003, nikapewa uongozi (Kiranja) kwenye darasa la watu (188). Nikawakilisha vyema shule yangu katika uandishi wa Insha uliohusisha wilaya nzima ambao uliuletea shule yangu ya Utegi sifa nzuri. Walimu walianza kuniona mbali tangu hapo na kuniombea sanaa ndoto zangu zitimie.

Ilipofika December 10, mwaka 2004, baba yangu alifariki nikiwa darasa la tano. Akatuacha na mama na familia ya baba mkubwa (Olambo Oucho) kama baba yetu mlezi! Tulisikitika na kuhuzunika sana ila tuliyasahau na kumuona baba yetu mkubwa kama baba yetu mzazi. Mwaka 2006, nilihitimu shule pale pale utegi Primary school. Chakushangaza ni kwamba hata kufaulu sikufaulu, mbali na kujitahidi sana darasani (sijui nini kilitokea), ila mwaka huo (awamu ya kwanza) walifaulu wanafunzi 12! Nilikasirika sana, nikasema nitarudia shule na nitafaulu kwa alama za juu sana. January 8, 2007 nikarudi shule kurudia darasa la saba nijaribu bahati yangu tena. Haikuchukua muda sana March 01, 2007 matokeo ya awamu ya pili yakatoka nikawa nimo kati ya watahiniwa waliofaulu kwa alama za chini 159/250? na kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari PASTOR RAPHAEL ODUNGA, ilioko kijiji cha Buturi, umbali wa Km kama 18 kutoka nyumbani.

Sikua na namna nilitamani sana kusoma na wenzangu form One, nikamwambia mama yangu akatafuta njia kwa kushirikiana na baba mkubwa wakanihamishia NYANDUGA Secondary iliyoko kwenye Kata yetu. Jumatatu ya tarehe 07 March, nilianza shule nikiwa nimebeba jembe, ndoo ya maji, kwanja, rim paper (double A) na shilingi 26,000/= nikaanza masomo. Wiki iliyofuata Jumatatu ya tarehe 12/03/2007 tulianza mitihani ya mid-term test nikiwa na siku tano tuu shuleni, nilipata alama za kushangaza watu sanaa ndio ukawa mwanzo mzuri! Nilipenda sana Maths, Physics, Chemistry na Biology ndipo nikaona mimi naweza kuwa Engineer baadaye maana masomo hayo nayaweza vizuri.

Mbali na kwamba baba angu mkubwa alisomea uhandisi (Engineering) nlipomgusia kuhusu nia yangu mimi ya kusomaea fani hiyo pia alinitia moyo sana, na kuniambia nikazane kwani kuna chuo kipo Dar kinaitwa DAR TECH, wanachukua watu wanaopasua sana masomo kama hayo! Akanipa dondoo za raha ya chuo hicho; wanavyokula, chuo kipo katikati ya jiji la Dar, wanalipwa hela, hakuna kufanya usafi, ? basi nikaona huko ndo patanifaa, nikasema wacha nikomaeee na shule kwanzaa.

MAISHA YA NYANDUGA SEKONDARI:
Nilijitahidi sana kusoma na kukazania masomo ya sayansi nikijua nikimaliza naenda chuo cha Dar Tech. Baba mkubwa alituwekea hazina ya vitabu vya kujisomea, nikapambana hadi mwaka 2010 ilipo maliza form four hapo Nyanduga Secondary, matokeo yalitoka yakiwa mazuri kwangu, na kwa rafiki zangu wengine. Tuliofaulu na kuchaguliwa technical school tulikuwa watatu; David Kajode alipelekwa Arusha Tech, David Kimira alipelekwa Ubungo Maji na William Ernest Mjee Oucho.

Hutaamini, nilichaguliwa moja kwa moja kujiunga na CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA Dar es salaam (Dar Tech), kusomea Shahada ya Uhandisi mitambo kwa miaka mitatu.????? ndoto ikawa imetimia kwa namna moja. Nilifurahi sanaa! Mama na kila mtu aliyejua walifurahia sanaa. Namshukuru hata Mbunge wangu wa jimbo (MH. LAMECK O. AIRO, Lakairo) aliniona kwa jicho lingine na kunitia moyo na kuniahidi kushikamana nami bega kwa bega mpaka nitakapofika.

SAFARI YA KUJA DAR:
Ilifika siku ya kutoka nyumbani kuanza safari ya kuja chuo, nikiwa mwenyewe kwa mara ya kwanza ? nilipofika tuu Tarime Km 14 kutoka home nikaibiwa pesa zangu zote, na nikarudi home tena kutafuta pesa nyingine. Nikapata pesa nikaanza safari kwa mara nyingine na kuja mpaka Dar. Nilipofika Dar nilipokelewa na mama mkubwa (Mrs. Cecilia Igogo), kisha kunipeleka nyumbani kupumzika. Kesho yake asubuhi mama alinisindikiza chuoni kufanya usajili na baadaye kuhamia chuoni kwani nilikua natakiwa nikae chuoni. Mama mkubwa ni mama mwema sana, alikua akipita kunisalimia na kuniombea kwa Mungu, alinambia niamini katika ninachofanya nitafanikiwa. Nilitii na nikamuahidi sitamuangusha. Nilisoma na hatimaye 2014, nikahitimu.

William na mama yake mzazi wakati wa sherehe za kumaliza chuo, Dar Tech

Ikawa furaha nyingine kubwa kwangu, kwa mama yangu, baba yangu mkubwa na kila mtu aliyetamani kuniona nafika hapo.
Nilitamani kuunganisha kuendelea kusoma ila kuna somo moja lilinifanya nisiweze kuunganisha, kwani matokeo yetu yalicheleweshwa kupelekwa NACTE, ikanibidi nikae mtaani kwa miaka miwili. Katika kipindi hicho cha miaka miwili nilitumia kupata uzoefu wa kile nilichosomea, ambapo baba yangu mkubwa (Mr. Otieno O. Igogo) aliniona na kunipeleka kiwanda kimoja cha kutegeneza juice cha (U-fresh food), Tegeta. Nilifanya kazi pale kama fundi mchundo wa mashine hizo. Baadaye milango ya kazi ilifunguka na kujiunga na moja ya kampuni kubwa hapa nchini ya Kuzalisha Umeme na Kusambaza gesi (Songas Power Plant), iliyopo Ubungo. Nilifanya kazi pale huku nikiwa najitegemea sasa, naishi kwenye chumba changu cha kupanga.

Ilipofika mwaka 2016, nikasema lazima nijiunge kumalizia masomo yangu ya Shahada ya kwanza. Nilifanikiwa kufanya hivyo, nikapata chuo kile kile, fani ile ile, na nikaanza masomo rasmi ya kuitwa Engineer. Nilianza masomo yangu ya shahada ya kwanza mwaka 2016, na nikadumu kwa miaka mitatu, hadi kufikia june 10, 2019 nilipohitimu rasmi na kuweza kufaulu na kupata nlichokua nakitafuta kwa muda mreeefu! New Mechanical Engineer in Town.

Changamoto kila mtu anazo ndio maana hata sijaziongelea hapa, msije mkadhani nilikua nasona kwa raha raha, weee! ???? Ila natumia fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu wa Mbinguni, muumba wa Mbingu na nchi kwa upendo na uhai alionikirimia. Pia napenda kushukuru kila mmoja kwa nafasi yake alivyoshirikiana na mimi kuniwezesha mimi kuwa hapa. Wanadarasa wenzangu, kuanzia darasa la kwanza hadi chuo Kikuu, ?!

? Mama yangu mzazi kapambana sana na mimi, kuhakikisha sikati tamaa, hata kama Inakuja gharika gani.

?Baba yangu mkubwa, Kwa kunionyesha njia na kutupatia elimu hakika, aliweza kutupa vitabu na sasa tunaona raha yake.

?familia ya Mr &Mrs Otieno Olung’a Igogo, mbarikiwe mpaka shetani aje awaulize mmewezaje wezaje???

? Lameck O. Airo, Erasto Airo bro asanteni kwa kila kitu kwa kipindi chote nilivokuwapo skuli.?Mbogi yangu ya Rorya, Robhin Edson, Edina Ziporah, Kajode, Mary, Triza, Omara, Vicky, Triza Wuod nam, Emma Lucas, na wengineo wengi ambao sitamaliza kuwataja hapa tumeshikana vyema na tuendelee hivi hivi?

Niwakaribishe katika mahafali ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza ya uhandisi Mitambo, tarehe 28/11/2019 katika viwanja vya chuo chetu, tufurahie kwa pamoja maana nikishinda nanyi mmeshinda…NB: wanaosoma au una mpango wa kusoma, tia bidii sanaa utafanikiwa tuu, Mungu ni mwema na ni wa kwetu sote.NAWAPENDA SANA WOTE. ? THE END?

Golden BBQ point- nyote mnakaribishwa!

Tafadhali jumuika nasi kwenye ukurasa wetu wa Instagram na karibuni sana Golden BBQ point kwa BBQ zenye ladha na ubora wa kimataifa, vyakula vitamu vilivyo pikwa kwa umahiri mkubwa sana, mazingira mazuri na bora ya kula huku akili ikiwa imetulia, huduma nzuri sanaaaa, na gharama zake ni nzuri mno.
Private Barbeque service can be arranged. Tupigie tuje tukuchomee kwenye sherehe yako. Tupo Masaki, Bains Avenue, Off Mwaya Road, Msasani Peninsullar, Masaki, Dar es Salaam, Tanzania, nyote mnakaribishwa ??

“Inawezekana mno ukiamua” ~~ Zamaradi Mketema

Reposted from @zamaradimketema – Unaweza ukawa na rafiki au jamaa unaemuamini sana au mlietengeneza Bond kubwa lakini ukaja gundua kuna mambo anafanya nyuma yako yasiyofaa dhidi yako/sio mtu mzuri ila UKASHINDWA KUJITOA KWAKE.

kwa kuogopa kumpoteza ukajikuta unajitafutisha hata sababu mwenyewe za kukataa ubaya wake alioufanya, na hata kugoma kuuona (kutafuta excuses/kuwa In Denial) kutokana na ile Bond iliyopo kati yenu.

Zamaradi Mketema, TV / Radio presenter

Na watu wa namna hii mara nyingi unakuta ni mtu ulieshare nae vingi, anakushauri ama ana siri zako nyingi sana hivyo inakutanda hofu ya kumpoteza bila kujali ule ubaya wake ambao unaweza kuwa na athari kubwa mbele.

Kwanza kabisa fahamu hakuna sababu yoyote kati ya hizo juu zinazotakiwa kukufanya ukeep mtu mbaya, kama hofu yako ni SIRI ULIZOMPA mwache ajue azimwage na kuzitangaza, hakuna jipya Chini ya jua, na ni bora kukata kuliko kumpa nafasi ya kujua mengine asiyostahili, na jiulize una uhakika gani kwamba hajamwambia hata mtu mmoja hivi hivi mkiwa mnaongea, hivyo usiendelee kuwa mtumwa wa mtu kwa kuogopa eti atatoa siri zako, mwache atoe tu, sidhani kama litakuwa jambo jipya Duniani.

Kuhusiana na swala la BOND YENU, Ukishaona mtu ni mbaya train yourself not to associate with them katika namna yoyote ile kwa kujifunza kusolve matatizo yako mwenyewe kidogo kidogo, itakuwa ngumu mwanzo lakini utaweza, itafika kipindi utaona kabisa humuhitaji tena, na usiendeshwe sana na hisia unapokumbwa na kitu, maana inaweza kutokea jambo na ukaona kabisa yeye ndio anaeliweza na huenda ni kweli lakini kumbuka ni kwakuwa tu uliamua kuamini hivyo, yes utamkumbuka lakini kumbuka tatizo ni la siku moja linapita, sasa kwanini tatizo la siku moja linalopita likufanye uendelee kumkeep mtu asiefaa milele, maana the more unavyoendelea kumshirikisha ndio the more utakavyoshindwa kujitoa kwake, usijiendekeze.

Na zaidi angalia MADHARA yanayoweza kutokea kutokana na ubaya alionao, kisha kubali kuwa huyo mtu hakufai, na hii inapaswa ianze na wewe, kumbuka HAUPOTEZI kama unaempoteza ana hasara zaidi kuliko faida, hivyo Kata, na jifunze kudeal na vitu mwenyewe, inawezekana mno UKIAMUA. – #regrann

Zari amekosea sana!

Kumpenda mtu siku zote utakuwa mkweli kwake hata kama yeye mwenyewe hapendi ukweli wako! As much as I Iove Zari, but I have to tell her this beater-truth! Kuwa Zari kwa hili umekosea sana!

Kwanza nianze kwa kusema simsapoti Diamond kwa udhalilishaji wake anao wafanyia wanawake kila siku! Hii ya Zari ni series ya matukio mengi ambayo amewafanyia wanawake ambao wamekuwa kwenye mahusiano naye.Amegeuza wanawake ndio mtaji wake wa kuongeza nguvu kwenye kazi zake! Which is very very wrong! However, despite all the evilness he has done, when comes to this issue ya kumdhalilisha Zari, personally I kinda understand where his pain is coming from! But again it doesn't justify what he did.

Kwanini nasema Zari amekosea? Ni kwasababu moja kuu ya kuamua kufanya udhilishaji kwa baba wa watoto wake bila kufikiria kuwa the real victims here are her own children! Tendo alilofanya Zari linamuweka level moja na Diamond, yani hakuna tofauti kati yao and two wrongs can't make it right! ..Kitendo cha Zari ku-move on na maisha yake ni kizuri sana! Tena sana! Nampongeza kwa hilo. Lakini kitendo cha yeye kuleta mwanaume mwingine kwenye nyumba ya mwanaume mwingine ni kukosa heshima sio tu kwa Diamond kama baba wa watoto wake bali pia kawakosea heshima watoto wake!
Zari, The Bosslady

Ule mji ulinunuliwa kama mji wa familia.That’s a place where her children as long as they live they will always remember and call it home! Home is small sanctuary, Zari has dishonored her children sanctuary! Hivi unajua ipo siku watakuwa wakubwa na sidhani kama watakuwa so impressed with their mom decisions! Haswa Tiffa, unajua jinsi watoto wakike walivyo na baba zao, Mungu atupe uzima kushuhudia yajayo!..Sijui kama Zari anajua anachofanya ni kosa au ndio maisha ya u-celebrity yamemuingia kwani hii sio mara ya kwanza kufanya hivyo. Tunaona hata alipo achana na marehemu Ivan Ssemwanga alikua anamleta Diamond kwenye nyumba ya watoto zake! Na marehemu hakufurahishwa na hili! ?? wanasema malipo ni hapa hapa duniani eeh! So Diamond got what he deserves!!.. Inajua mimi nashindwa kuelewa sijui ni Usabato wangu au ujaluo ndio unanifanya nishindwe kuelewa hii celebrity lifestyle!

Hivi wanawezaje kuleta mtu mpya kwenye nyumba au chumba ulichokuwa unatumia na your Ex-girlfriend / boyfriend? Nashindwa kuelewa haswa kwa wanawake! Majasho ulioweka kwenye makochi na mwanaume mwingine ndio hapo hapo unamleta mpenzi wako mpya ? Dah! Mie sielewi hii lifestyle! Labda ushamba umenizidi can’t think right ?‍♀️?‍♀️

Diamond ni mwanaume mshezi tu (sorry to say that) lakini hapa Zari kampa sababu na nguvu ya kumdhalilisha kwa kitendo cha kuleta mwanaume mwingine kwenye nyumba yao ambayo walinunua kwaajili ya familia. Ndio maana nimesema naelewa hasira za Diamond japo sifurahii alicho kifanya! Hii imekuwa ni desturi yake kudhilisha Exs wake toka wakina Penny, Wema n.k wote kawafanyia huu ushenzi! Ila amini usiamiani Tanasha anatmnyoosha Diamond wewe weka macho yako utayaona!

Mama Tiffah, the Bosslady

Kama kweli Zari anataka amani na kuishi maisha yake bila bugudhi yoyote basi Zari, you need to move to your own house, period! Let those men who desperately need you move to your house ili wakikuletea ujinga unamwomba aondoke kwenye mji wako. Lakini kitendo cha kuendelea kuishi kwenye mji wa wanao ambao baba yao kawanunulia haitakupa uhuru ambao unautaka! Just get your own place hata kama ni kubaya kama kwangu lakini ni kwako! Ni chakwako hakuna wakukwambia kitu! Please!

Halafu, I don’t know about you Zari maybe because you’re living that “celebrity lifestyle” but a man who dishonors his fellow man’s home like that?! Ain’t a man for me! Because it comes down to his morals and ethics! I hope he won’t turn around to be like the one you just dumped or even worse!..Hapa ndipo Tanasha kawazidi, unaona ametaka nyumba mpya kabisaaa ambayo hakuna Ex-girlfriend yoyote wa Diamond amewahi kulala wala kufika hapo! Msichana wa Kijaluo akili kwa kichwa ?? Nani anataka kulalia vitanda au kukalia makochi yenye majasho ya mikosi ya mtu mwingine? ?

Anyway, just prepare for the worst and hope for the best ?? I saw somewhere you said you are about to say ‘I do’, my advice to you is take your heart with you but don’t forget your brain!! And prayer is key to every battle! Otherwise wishing you the best in everything you do! ❤

Dina Marious: Je, marafiki walio tuzunguka ni wa aina gani?

Reposted from @dinamarious – Leo nimeamka kichwa kiko mbio maana zimebaki siku 4 tu niwe nawe katika Maisha Class Seminar.

Lakini nimemkumbuka rafiki yangu mmoja wa toka udogoni.Hatuonani sanaa ila tunaongea sana kwenye simu.Nikakumbuka namna walivyokuwa wakiishi maisha mazuri sana.Wao ni miongoni mwa watu wa kwanza wazazi kuporomosha mijengo huku Mbezi beach.Miaka ya 90 wana hadi boat ya kucruz kwenda visiwa hivyo vya bongoyo sijui mbudya ambavyo sie ndio twaenda leo.

Dina Marious; Mtangazaji, Mfumbuzi na Mkurugenzi Mkuu wa Dina Marious Coconut Oil, Founder of Mwanamke wa Shoka and Kitchen Party Gala

Mama yao aliwazaa mapema sana na baba yao akafariki mapema pia.So walilelewa zaidi na mama.Mama alikuwa na pesaa alikuwa mrembo sanaa na alikuwa na marafiki wengiii mno.Na pia alikuwa mzuri wa sura na wa roho kujitolea kwa marafiki na ndugu sanaa.Wadogo zake kama watatu aliwawezesha kwenda kuishi nje.Yeye safari za nje ya nchi kama sijui kitu gani.Party za babakyu na marafiki safari na marafiki za kula bata nyumbani kwake palikuwa hawakauki watu.
Yule mama alikuja akaanza kuishiwa akaanza pia kuumwa aliugua kwa muda kidogo na kwa wakati huo rafiki yangu na mimi tupo kidato cha pili.Ndugu walikula kona,marafiki ndio usiseme.Alibaki yeye na watoto wake tu na hadi anafariki alimfia mwanae huyo shoga angu mikononi hivi akimhudumia maana ndio wa kwanza.

Dina Marious; Mtangazaji, Mfumbuzi na Mkurugenzi Mkuu wa Dina Marious Coconut Oil, Founder of Mwanamke wa Shoka and Kitchen Party Gala

Kuna mengi yalitokea sanaa lakini hili jambo huwa silisahau.Maana mie ndio nilikuwa shoga ake namna ndugu zake walikuwa wakimfanyia nilishuhudia kwa macho.Na huwa namkumbuka sana huyo mama na sasa nimekuwa mtu mzima ishu hiyo huzunguka sana kichwani kwangu.

Je marafiki waliotuzunguka ni wa aina gani?una marafiki kweli au una wapambe?Ni wangapi katika mafanikio tunakuwa na marafiki wengiii ambao kiukweli wapo hapo kwa manufaa yao?Wapo na wewe sababu una nafasi fulani,wadhifa fulani kupitia wewe mambo yao yatanyooka?Kwa sababu una mkono wa kutoa labda utatatua shida zao,utasikiliza hofu na nyakati ngumu wanazopitia. Utawalisha,utawanywesha,utawapa pesa,nguo,viatu inshort unarahisisha maisha yao.Ngoja pesa ikate ndio wa kwanza kukusema umefulia na kukukimbia.
Ngoja cheo/nafasi uliyonayo ipotee ndio utawajua walimwengu au wali nyama!Sitasema sana ila Mungu atujaalie watu sahihi katika maisha yetu.

MaishaClass #NenoLangu – #regrann

**Imeandikwa na Dina Marious**

Unapokutana na mtu mwenye mafanikio usimuombe pesa. Muulize amefanyaje kufikia hapo alipo!

“When you meet a person with means, a person that is well-off you think is successful  that you always wanted to be; don’t go there asking  for money” Hayo ni maneno yake Comedian na TV host Steve Harvey kwenye Oprah Master Class. Master Class ni show ambayo watu wengi waliofanikiwa katika nyanja mbali mbali za maisha wanaelezea mafanikio yao kwa undani zaidi toka walivyokuwa wadogo mpaka walipo fikia. Changamoto zipi walipata, vipi waliweza kuvumilia, kumudu hizo changamoto, na hata kufanikiwa bila ya kukata tamaa. Unapopata nafasi ya kukutana na mtu au watu ambao unawaangalia kama  “role mode / icon”  katika maisha yako usiwaombe pesa waombe wakuelimishe nini walifanya kufikia hapo walipo. Watu wengi wapo wepesi wa kuomba pesa kwa mtu aliyejaliwa kuwa nazo kwa ajili ya kujikimu na hiyo shida aliyonayo. Nautakuta muda mwingi shida hiyo haiishi ni kaituliza tu kwa muda. Hii yote nikwasababu wengi tunapungukiwa hekima ya kujua kuwa ni kheri mtu akupe elimu ya maisha ya nini alikifanya mpaka kufika hapo ili uone kama na wewe unaweza tumia njia hiyo kufikia malengo yako au kujikwamua kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Au utakuta wengine tumepingukiwa hekima ya kuona mafanikio ya watu ni maovu mbele zetu nakuanza kutafuta njia ya kumuangusha bila kujua kuwa anguko lake ni maafa kwako pia. …….Hivyo tuwe waelevu kama nyoka na wenye hekima kama Solomon ili tuweze kujifunza kutoka kwa wengine haswa ambao tunaona wana tija katika maisha yetu. Pale watu wanapokukatisha tamaa wewe piga moyo konde usiwasikilize. Kwanza mimi kwa experience yangu binasfi watu wengi wenyekukatisha watu tamaa ni watu ambao hawajiamini na pia hawapendi kuonekana kuwa wao wameshindwa katika kufikia kile wakitakacho hivyo hamna la zaidi zaidi ya kupiga makelele ili uwe muoga. Wakati ukweli wanatamani wangekuwa na ujasiri kama wako. Utaona wanakuja na maneno mengi ya kejeli ikishindikana wataingilia personal attack “hajaolewa”, “mnene”, “hana nywele”, “mbeba mabox” yani ukishaona mtu anaenda kwa personal attacks jua maumivu yamemuhelemea ?? . . Nasiku hizi social media, basi watatafuta kila event au tukio lenye viongozi waende kupiga picha ili warushe kwa Facebook / Instagram basi tu ufikirie kuwa there really happy and making it, wakati rohoni wanatamani wawe na kipaji au nafasi kama yako. ?? Wanasaikolojia wanasema mara nyingi watu wanao ongelea wengine vibaya muda wote huwa kuna mambo ambayo hayopo sawa kwa upande wao sasa kwasababu hawataki watu wajue huo upande wao hauwapendezi, basi dawa inakuwa ni kugeuza attention kwa wengine! Na huo ndio ukweli! Wewe usikate tamaa na mapicha yao! Nawala usiache mashauzi yao yasio na kichwa wala miguu yakuumize au yakutoe kwenye malengo yako. Mimi nilivyoanza hii blog yangu nimetungiwa uzushi wa kila namna; ooh huyo muhuni anatafuta mwanaume, huyo FBI, huyo kada wa CCM (utafikiri walishaniona na kadi ya CCM au nimevaa gwanda la CCM ??), mara anatafuta umaaharufu, mara mkabila, mdini, yani maneno mengi mno wengine wakadiri hata kwenda kwetu kuchunguza maisha ya kwetu nakuja kuongea kwenye magroup yao. Mara kazi yake kudhalilisha watu. Eti huyo anagombania mali za wazazi wake ?? Wengine wakazunguka kuwaambia watu wasiweke picha zao kwa hii blog. Yani hayo yote walifikiri nitaacha kublog!! Lakini nipo hapa and I’m here to stay! Mimi najua ninachofanya na ninako kwenda hivyo sijali. Waliokua wanasema mimi kazi yangu ni ku copy and paste ndio hao hao wanakosa raha kwani wanatamani niwaweke humu kwa blog yangu nami hata habari nao sina ??  Ni maumuvi makali sana wanapata. Wewe songa tu, wakikwambia huwezi wambie wewe ni nani hata useme hivyo! Kitu kingine usiamini kila rafiki. Yani ukiona mtu ambaye ni rafiki yako anachukia maendeleo au mafanikio ya mwingine achana na huyo rafiki mara moja. Kwani inamaana wewe ni rafiki yake Kwasababu haujamzidi kimaendeleo lakini siku ukitaka kunyanyuka atakuwa wakwanza kukuangamiza! Niamini nimeyaona! Siku zote kuna mtu mmoja ambaye atakuelewa na ambaye atakuwa yupo teyari kukusaidia kufikia malengo yako. Mungu huwa hamtupi mja wake! Kama nipesa basi huyo mtu anaweza kusaidia, kama ni mawazo yanini ufanye ili ufanikiwe basi huyo mtu atakuwa yupo tayari kutoa ushauri. It means that person believes in you and truly cares about you! When it looks like nobody cares trust me someone is out there who really cares about you! Muda ukifika Mungu atamleta kwako. Usikate tamaa!

**Imeandikwa na Alpha Igogo** **#TBT #Sept.2017**

Mwanamke ni mtu shujaa, mwenye hekima nyingi, na muerevu sana!

Embu leo tuongelee hichi kiumbe ambacho Mungu alikiumba baada ya kuumba kila kitu! Mungu aliumba vyote lakini akaona kuna mapungufu mahala yani kwa lugha zingine naweza sema hakuridhika na kazi yake ya uumbaji mpaka alipo muumba mwanamke akaona vyote ni mema sana na uumbaji wake ukaishia hapo!

Labda niseme kwa siku ya leo nia yangu si kuongelea uumbaji wa Mungu bali nataka kuongelea moyo au nguvu ya ushujaa, hekima, na uwerevu ambao mwanamke amepewa na Mungu mwenyewe lakini bado tunajiona wadhaifu, hatuwezi kufanya kitu bila nguvu ya mwanaume kwanini? Kwakweli hata mimi sijui sababu bado najiuliza kwani kitu ambacho wanawake karibia wote tuna “struggle” nacho hata mimi mwenyewe- hello! Yes, me too ? Msema kweli ni mpenzi wa Mungu!

Hivi umeshajaribu kutafakari kuwa Mungu baada ya kumuumba mwanaume akaona kuwa hajakamilika kuna kitu kinahitajika ili huyu mwanaume aweze kufanya kazi kamili na kuishi kama mwanadamu? Na kitu hicho ni mwanamke! Hivyo, ukitaka kulinganisha utagundua kuwa mwanaume anahitaji nguvu ya mwanamke zaidi ili kuwa kitu kamili lakini mwanamke anaweza akafanya kazi na kuishi bila kumtegemea mwanaume sana (mnaojua maandiko ruksa kunikosoa). Naomba nieleweke, sijasema mwanamke hamuhitaji mwanaume la asha! Kila kitu ili kifanye kazi vizuri lazima kuwe na nguvu za hasi na chanya (mkono wa kulia na kushoto) ambazo zimeunganishwa pamoja katika kuleta nguvu kamili! Lakini saa nyingine utakuta upande wa kulia hautoi joto / nguvu sawa na kushoto hivyo inailazimu upande wa kushoto kutoa nguvu zaidi ili kuweka balance!

Zari The Bosslady

Nguvu ya ushawishi na hekima ambayo mwanamke amepewa ni kubwa sanaaaa! Tukiacha kisa cha Eva alivyo mshawishi mumewe Adamu kula tunda la mti waliokatazwa na Mungu, embu tuangalie kisa ya Malkia Esther kwenye Biblia! Jinsi Esther alivyotumia ushujaa na hekima ya hali ya juu kumshawishi Mfalme (mumewe) mpaka kuokoa watu wakwao! Kutokana na sababu mbali mbali watu wote waliogopa kumfata mfalme, lakini Esther alipoambiwa akasema lazima nifanye kitu kwani alijua kunyamaza kwakwe kungetoa tafsiri ya kuwa ameunga mkono maadui. Esther akajua wakati ni sasa kama ni kufa basi acha nife lakini lazima nikamuone Mfalme na kuweza kuongea naye juu ya jambo hili. Esther akatumia uerevu wake na hekima kupanga nini cha kusema, mahali pakusema, na muda wa kusema! Namwishoe akashinda na kuonekana shujaa kwa watu wa kwao!

Labda nifupishe hii story kwa kusema kwanini nimeandika, nia yangu nikutaka kuwakumbusha wanawake kuwa sisi ni viumbe vya kipekee sana ambavyo tumebarikiwa sana na Mungu lakini muda mwingi tumekuwa tukijikatisha tamaa sisi wenyewe aidha kwa kujua au kuto kujua! Tumekuwa waoga wa kutoa sauti zetu zisikike mbele ya wanaume. Tumekuwa hatutaki kueleza hisia zetu halisi na kujikuta tunaishi maisha yasio na uhalisia na kile kilichopo moyoni mwetu! Tumeshindwa kutumia nguvu ya ushujaa na ushawishi ambazo tumepewa na Mungu kuleta mabadiliko mbali mbali ndani ya maisha yetu na katika jamii zinazo tuzunguka! Tumekuwa viumbe dhaifu wakati Mungu alituumba kama mashujaa mkombozi wa mwanaume!

Japo kwasasa wanawake wengi wanaanza kuamka na kutambua hii siri ambayo ipo ndani yetu lakini bado inabidi tuamke zaidi! Mapinduzi yakweli yataletwa na mwanamke! Si unaona jinsi Eva alivyoweza mshawishi Adamu kula tuna na dunia yote sasa wanawake wanazaa kwa uchungu na wanaume wanaishi kwa jasho lao ?? Basi kama mnataka mabadiliko ya kuachana na siasa mbovu, kutokomeza ukatili wa aina zote, mazingira bora na salama ya kuishi n.k lazima muamke usingizini!

Usijione wewe hufai eti kwasababu unatabia kama za “Wema Sepetu” (sorry Wema I picked you), hapana! Mungu anapenda watu wote na anaweza mtumia mtu yoyote yule kufanya mabadiliko kwaajili ya utukufu wa jina lake! Kwa wale Wakristo kumbuka kisa cha Rahab au Ruth kwenye Biblia! Wanadamu tunatizama vitu kwa macho yetu haya ya dhambi hivyo nirahisi kuhukumu watu na kuona kuwa hawafai na hawana thamani lakini siku zote kumbuka kila mtu anathamani sana mbele za Mungu! Na kama Mungu ataamua kukutumia hakuna atakaye weza kuzuia! Kikubwa ni wewe kusikiliza ile sauti ‘ndogo’ inayo nena nawe kwa upole ndani ya nafsi yako kuwa badili njia zako!

Wanawake tunaweza kuibadilisha hii dunia kuwa mahala salama pakuishi tena kama hatuta waachia wanaume peke yao! Wanatuhitaji ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli! Siku zote kumbuka kuwa wewe ni shujaa, mwenyewe hekima, na muerevu sana!

****Zari’s picture has nothing to do with the story**

**Imeandikwa na Alpha Igogo

“Unakichaa mimi nakuita mwendawazimu”!

Hicho kichwa cha ujumbe / somo la leo nimetoa kwenye ule wimbo wa ‘Yamoto Band’ lakini sipo hapa leo kuzungumzia huo wimbo wala band. Nimeyachukua tu kwasababu yameendana na ujumbe wangu!

Unasema humpendi mtu fulani (labda tuchukulie Zari, the Bosslady) lakini anafungua FEKI AKAUNTI ya social media kila siku haipiti hata masaa sita bila wewe kuangalia ame post nini?! Wewe unakichaa na ninakuita mwendawazimu!! Haiwezekani mtu mwenye akili zake timamu anayejitambua akaishi maisha ya kujidanganya na kujiumiza hisia zake mwenyewe!! Wewe lazima utakuwa punguani!! I’m sorry, but no thanks!

My twin sister and I

Hivi unajua ni ngumu kiasi gani kuishi maisha ambayo yanaumiza hisia zako? Kuishi maisha yanayo kupa hasira na chuki na watu wengine tena ambao hata huwajui undani wao zaidi ya kile unachokiona kwenye social media! Sasa tabu yote hiyo yanini? Ni kitu gani kinakufanya unaishi maisha yanayo kutesa? Kumfatilia mtu kwa kila kitu afanyacho hiyo ni zaidi ya ajira? Na kwenye ajira kuna mapato mtu anatakiwa kupata baada ya kazi ngumu, sasa wewe ni mapato gani unapata baada ya kumfatilia? Maana sio tu unapoteza muda wako, bali pia umetumia fedha yako kulipia internet, umeacha kufanya jambo lingine ambalo kwa namna moja ama nyingine lingekusaidia kuona mbele zaidi, yote hayo hukujali ukaamua kumfuatilia mtu usiye mpenda?! Halafu bado utatoka hapo unapoteza muda kumsengenya na wendawazimu wenzako ?? Wonders shall never end!

Mimi binafsi sina muda wa kumfuatilia mtu ambaye ananikwaza, yani sikufungulii account fake hata mara moja nakupa block nasonga mbele! Embu nawe jaribu hii njia ninayo tumia mimi huwenda ikakusaidia. Hakuna haja ya kufungua account Feki kumfatilia mtu usiye mpenda! Maisha ni mafupi sana sasa usipotaka kuwa wewe katika hualisia wako ukaishi maisha yako sasa angali unapumua lini utaishi na watu wakakujua kua huyu ni fulani?!

Kamwe kataa kuishi chini ya kivuli cha mtu mwingine! Life is too short to blend in or to be someone else! Be real! Be you! We only live once!

Mtangazaji Maduhu aupa mkono wa kwaheri ‘ukapela’!

Beyonce sang it well “if he liked it he should have put a ring on it”! Basi ndivyo Mtangazaji maharufu toka Morning Star Radio ajulikanaye kwa jina la Maduhu alivyo fanya, he put ring and sealed it before God on Sunday April 7th, 2019.

Ndoa hii TAKATIFU ilifungwa katika kanisa la Wasabato la Nations Of Praise liliopo ndani ya jimbo la Houston, Texas inchini Marekani siku ya Jumapili majira ya saa kumi jioni saa za Marekani.
Mnaona neno “Takatifu” hapo juu ☝️ nimeweka kwa herufi kubwa na wino mwingi eh?! Nikuwakumbusha walevi na “mashakunaku” kuwa “alicho kiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe”!! Wale walevi wasiyo na haya huyu ni mke wa mtu muogopeni! Na wale mashakunaku wenye macho juu juu kama tunguli za mchawi nawakumbusha huyu ni mume wa Sule peke yake hachangii na mtu wala hamkodishi tafuteni wenu! ?? kama nawaona mnavyo nisonya ???

Ndoa ilifungwa inchini Marekani kwasababu Bibi harusi yeye ni Mmarekani mwenye asili ya Kitanzania. Ambapo kule Tanzania anatokea maeneo ya Upareni.
Bwana na bibi harusi kwa furaha wenye nyuso za tabasamu baada ya kula kiapo kitakatifu!
Wapambe walikuwepo! Walipendeza sana.
Kwamara nyingine naomba niwapongeze sana Mr and Mrs Maduhu kwa kufunga ndoa takatifu! Wamesema wanaotaka ndoa za “mkeka” nyie fanyeni tu lakini sisi tunakwenda kula kiapo kitakatifu mbele za Mungu wetu aliye umba Mbingu na dunia! Mbarikiwe sana na nawatakieni furaha na amani isiyo na kikomo ??

**Shukrani zangu za dhati ziwaendee wadau wote waliotuma hizi picha kwenye lile group la “Harusi tunayo”. Mbarikiwe sana ??**

Blog