Peter Sarungi: UPANDE WA GIZA NA MWANGA WA BINADAMU

Na Peter Sarungi (The Next Speaker)

UPANDE WA GIZA NA MWANGA WA BINADAMU.
Binadamu ameumbwa katika ukamilifu ulio kusudiwa na Mungu na ndio maana akiwa kichanga anakuwa mtupu asiye tambua baya wala zuri. Binadamu huyu anaanza kuondoa ukamilifu wake pale anapo ona, kusikia, kusoma na kutenda mambo yaliyo najisi.

Akisha tambua baya na zuri ndipo anapo kuwa sio kiumbe kikamilifu. Binadamu huyu sasa anakuwa na pande mbili ya maisha yake. Kuna upande wa mwanga wenye matendo mazuri yaliyo wazi kwa watu na upande wa giza wenye matendo mabaya yaliyo fichwa gizani yasionekane kwa watu.

Kila binadamu ana maovu yake ila kinacho saidia ni kufichika kwa maovu hayo, ninacho shangaa ni kuwepo kwa tabia ya kuhukumu, kudharau na kutoa adhabu kwa binadamu ambao uovu wao umefichuliwa. Sijui logic hapo ni ipi ikiwa anaye toa adhabu na kuhumu naye ni mwenye maovu yaliyo jificha???

Leave a Reply